Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 3,520
- 6,503
Jana nikiwa nimejipumzisha zangu nikajisikia kusikiliza Redio kidogo basi mara nyingi ikitokea Nataka kusikiliza matangazo ya Redio basi Tbc Taifa ndio sehemu muafaka kwangu Kule huwa napata kitu roho inapenda,maana hizi Redio za niaje niaje mtu wangu na collection ya miziki Yao ya kamata kiuno sijui shika bega aah zinaniboa Sana.
Basi nikakuta miongoni mwa mambo yaliyo kuwa yanajadiliwa katika kipindi kile ni pamoja na msemo unao wataka wasikilizaji kutoa maoni kuhusu "kumjua mtu kupitia mtu"
Ni msemo ambao unamaanisha kwamba ukitaka kumjua mtu basi utamjua kupitia labda rafiki yake wa karibu au mtu wake wa karibu ambaye wanafahamiana Sana. Ni kweli hiyo na njia moja ya kumfahamu mtu na kupata taarifa zake mbali mbali lakini Kwa maoni yangu unaweza vile vile usipate taarifa zake sahihi kutokana na mambo kadhaa.
Kwa mfano huenda unataka upate taarifa za ETUGRUL BEY kupitia Mokiti lakini kumbe hapo awali walikuwa marafiki Wazuri Sana,lakini baadae wakaja kutofautiana na kugombana kwahiyo utakapoenda Kwa Mokiti utake taarifa za ETUGRUL BEY lazima atatoa taarifa hasi na mbaya ili kumchafua mhusika kwasababu wameshakuwa mahasimu tayar.
Lakini kuna mazingira mengine,huenda unatafuta taarifa za Mademoiselle Kwa mfano labda unataka kumpa dili Fulani au kuna maslahi fulani anaweza faidika nayo Kwa kuulizia taarifa zake Kwa Kalpana kama best yake ni mfano tu,basi kuna uwezekano mkubwa Kalpana asitoe taarifa sahihi ili huyo mlengwa asifaidike na Jambo Fulani, jamani natoa mifano Tu hapa Kwa kutumia Id zenu sio kwamba ndio mko hivyo.
Kwahiyo Kwa kifupi wakati mwingine ni sahihi kumjua mtu kupitia mtu lakini na wakati mwingine inaweza kuwa kinyume chake kabisa,kwahiyo cha msingi wakati unataka kumjua mtu kupitia mtu basi jitahidi na Kwa upande mwingine kufanya utafiti wako binafsi halafu linganisha na data utazopata kutoka Kwa mtu wake wa karibu halafu upate majibu sahihi.
Ni hayo Tu!
Mamndenyi
baby zu
To yeye