Je ni kweli kwamba Condoms ziazuia UKIMWI?

Mkombozi

JF-Expert Member
Feb 19, 2008
806
426
Wakuu,naomba tujadili.Kila mwaka maambukizi yanaongezeka licha ya elimu ya kutosha na utumiajia wa condoms.

Mbaya zaidi waathirika huwezi kuwajua kwa mwonekano kama zamani baada ya kuja kwa ARVs. Sasa je ni kweli Condoms zinasaidia?Najua humu jamvini kuna Madaktari,Watumiaji wenye uzoefu wa kutosha,wauzaji wa condoms,viongozi wa dini,watafiti,waelimishaji na wasiiamini condoms.

Je tunasemaje kuhusu uthabiti wa condoms?
 
Condoms zinasaidia sana kuzuia maambukizi ya VVU isipokuwa watu wengi wanao ambukizwa ni wale wanao jamiiana kavukavu kaka,si unajua sisi wa bongo tunavyopenda kusikilizia ile kitu,tunapenda ku-feel zile maeneo zinagongana without protection.
 
Usiamini kondoms kwa 100%.

Kwanza condoms zikifanyiwa majaribio sio zote 100% ni salama, inawezekana siku moja ukakutana na defective one. Halafu nyingine zinapungua ubora wake kutokana na utunzwaji wake km. joto au baridi kupita kiasi. Wakati mwingine unapoivua baada ya kuitumia unashika yale majimaji ya ukeni, na ukiwa umechubuka kidogo tu kwenye vidole unaweza kupata maambukizi. (kuna wengine wana tabia ya kupapasa na hata kutia kidole katika u*e ili kufahamu kama mwenza yuko tayari).

Pia wakati wa tendo la ndoa na ukiwa umetoka kfyeka kamsitu kako, basi yale majimaji yanaweza kukugusa eneo hilo na ikawa nooma.
NJIA ILIYO SAHIHI KULIKO ZOTE NI KUACHA ZINAA, UTAKUWA SALAMA HAPA DUNIANI NA AKHERA.
 
Wakuu,naomba tujadili.Kila mwaka maambukizi yanaongezeka licha ya elimu ya kutosha na utumiajia wa condoms.Mbaya zaidi waathirika huwezi kuwajua kwa mwonekano kama zamani baada ya kuja kwa ARVs.Sasa je ni kweli Condoms zinasaidia?Najua humu jamvini kuna Madaktari,Watumiaji wenye uzoefu wa kutosha,wauzaji wa condoms,viongozi wa dini,watafiti,waelimishaji na wasiiamini condoms.Je tunasemaje kuhusu uthabiti wa condoms?

Are you sure maambukizi yanaongezeka mkuu? Umefanya karisechi kidogo kujiridhisha juu ya maongezeko ya hii kitu Boss?
 
Back
Top Bottom