Nimejiuliza sana na kutafakari maoni ya watu wawili ambao wote nawaheshimu kama wadau wenzangu japa jamii forums kwa muda mrefu na sio vizuri kukaa bila msimamo kwenye mijadala kama hii yenye tija.
Zitto anaweza kuwa sawa kwamba 10% ni muhimu kwa taifa letu kwenye kukuza demokrasia
Lakini P, naye anaweza kuwa sawa kwamba uongozi kwenye vyama vya siasa ni wakujitolea.
Mawazo yangu ni haya. Swali la msingi je tuko kwenye nyakati gani kwenye mfumo huu wa demokrasia mfano kwa demokrasia changa ambayo ndiyo inaanza Zitto yupo sawa kwamba ni muhimu kuwa na ruzuku ili tuweze kuibuia mawazo na kupata vyama vyenye ushawishi na matokeo yake kusaidia taifa. Lakini hatuwezi kuwa na mfumo wa ruzuku bila ukomo. Demokrasia ikikuwa na vyama vinatakiwa kupungua na ushindani ya kisiasa unatakiwa kuwa mkali
Zaidi na ndiyo maana nchi za demokrasia huwezi kuona vyama vinashinda kwa zaidi ya 60%.
Sasa ukweli ni kwamba Tanzania tayari tuna zaidi ya miaka 25 toka vyama vingi. Kwa mawazo yangu tatizo la Tanzania kwa sasa kubwa ni katiba na sheria nzuri na hakuna ushahidi kwamba idadi ya vyama inasaidia hili. Lowassa aliweza kupata kura karibu 40% na kwa mawazo yangu ingekuwa sasa angeweza kupata si chini ya 45% kwa mazingira kama yale kwa sasa. Hivyo Tatizo sio kukuwa kwa demokrasia lakini tatizo ni sheria mbaya za kukandamiza demokrasia. Demokrasia ikikuwa upinzani unakuwa karibu na 50%.
Pili sioni faida ya kuwa na idadi kubwa ya vyama Tanzania badala yake kuwe na vyama vichache vyenye nguvu na idara imara. Vyama vya kununuliwa au kutegemea ruzuku sana vimekuwa kero kwa demokrasia badala ya kuwa msaada.
Kwa tulipo kwa sasa na kufunguka kwa Watanzania kwa mawazo yangu Tanzania ingenufaika kama tungebaki na CCM, Chadema na ACT badala ya vyama ambayo havisaidii na mara nyingi vinatumia kama kukandamiza demokrasia.
Cha maana kubadilishwe sheria za kuchangia vyama bila kuogopa serikali. Vyama viruhusiwe kuwa na miradi au hata share kwenye makampuni.
Hivyo naungana na P kwenye hili kwa njakati hizi anachosema kina tija kuliko zitto ingawa Zitto ana nia nzuri na kwa njakati nyingine za huko nyuma angekuwa sawa. Nawaheshimu wote lakini kwenye hili nakubaliana na P lakini kuwe na sheria rafiki za kuchangia pesa vyama bila kutishiwa.