Je, ni Halali kwa Wananchi kusema "Asante Rais" kwa mafanikio yaliotendwa kwa nguvu za baadhi ya wananchi?

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Kumekuwa na wimbi kubwa hususani Tanzania la baadhi ya watu na viongozi kumshukuru Rais kwenye mambo ambayo yametendwa na Raia.

Mfano Jana Usiku imepigwa mechi baina ya Tanzania na Algeria kwenye michuano ya kufuzu Afcon kwenda Nchini Ivory Coast (Cote D'Ivoire). Lakini cha kushangaza Sifa zote zinamwagwa kwa Rais. Tazama post ya Mbunge "Babu Tale" hapo chini.

kwenye sekta ya michezo tumeona ndani ya mwaka mmoja namna ambavyo mama umefanikiwa.. Tuliiona Simba ikicheza Robo fainal CLUB BINGWA AFRICA na tukashuhudia Yanga akicheza FAINAL KOMBE LA SHIRIKISHO.. nasasa tunaenda kuiona Taifa stars ikiwa ni miongoni mwa timu 24 zitakazo wakilisha mataifa yao pale IVORY COAST/kiukweli Mama unaupiga mwingi kutokana na hamasa yako kwenye mpira wetu.. nikiwa kama mdau wasoka naanza kukupongeza wewe.. naipongeza TFF ikiongozwa na Karia..​

Nawapongeza wachezaji wetu,navipongeza vyombo vya habari vyote vya hapa nyumbani.. namwisho nawapongeza wananchi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwanamna ambavyo wanaendelea kuisapot timu yao..​

Huu upuuzi uwezi kuuona Nchi zilizoendelea, hata hapo Kenya uwezi kuona huu upuuzi kwamba Wananchi wanafanya kazi yao, alafu Sifa zinaenda kwa Rais. Marekani au Uingereza uwezi kuona Timu ya taifa inashinda alafu Wananchi wanasema "We thank president Joe Biden" au "We thank Queen Elizabeth". Hata Kenya ni nadra sana kuona rais anapongezwa kwa kitu kilichofanywa na Raia.

Ikumbukwe kusema neno "Asante Rais kwa kufanya hivi" ni kama vile Rais ametoa msaada, wakati kiuhalisia hile ni nguvu ya Umma. Chochote anachofanya Rais ni Mali ya Umma, hata Fedha anazotoa ni Mali ya umma. Anachofanya Rais sio msaada bali ni wajibu wake kama Rais, kama vile Mwalimu anavyofundisha, Mwenyekiti wa mtaa anavyosaidia mtaa, Daktari anavyotibu na jinsi ilivyo kwa watumishi wengine wa serikali. Kitendo cha kusema asante Rais kwa kitu fulani, utafikiri asingekuwepo yeye tusingeweza ni ujinga wa watanzania ndio maana wanasiasa wanaendelea kujifanya miungu watu, kwa sababu wanapokea sifa ambazo kimsingi ni wajibu wao na kazi yao kuyafanya hayo kama ilivyo kwa watumishi wengine. Ndio maana hizi Asante uwezi kuziona kwenye Nchi zinazotambua Wajibu na Kazi (Duty and Responsibility) ya Raisi.

Pesa tumpatie sisi kupitia kodi, na akifanya maendeleo kwa Kodi zetu, tunaanza kumramba miguu na kusema Asante. Utafikiri Pesa ni zake, au alichofanya ni msaada. Rais anakuja kutuomba kura ili akatekeleze haya anayoyafanya, ni moj ya majukumu yake ambayo ndio yamemuweka madarakani na hasipoweza kuyafanya hayo basi ataondolewa madarakani kwa kushindwa kuyafanya. Hivi ndivyo nchi za demokrasia ufanya kazi, na si kushukuru serikali wakati ni wajibu wake kuwezesha kila sekta kupiga hatua.
 
Kumekuwa na wimbi kubwa hususani Tanzania la baadhi ya watu na viongozi kumshukuru Rais kwenye mambo ambayo yametendwa na Raia.

Mfano Jana Usiku imepigwa mechi baina ya Tanzania na Algeria kwenye michuano ya kufuzu Afcon kwenda Nchini Ivory Coast (Cote D'Ivoire). Lakini cha kushangaza Sifa zote zinamwagwa kwa Rais. Tazama post ya Mbunge "Babu Tale" hapo chini.

View: https://www.instagram.com/p/Cw6KDfdorC2/?igshid=MzRlODBiNWFlZA==

Watanzania kwa eneo kubwa wanaumwa ugonjwa wa MNYONG'ONYO

Kupona kwake ni CCM itoke madarakani kwa amani
 
Inategemea na nchi husika.
Kama ni Tanzania bila shaka ni halali, lakini kwa nchi zilizoendelea huwezi jenga barabara au huduma za jamii ukatoa utegemee raia wakupe pongezi.
 
Sidhani kama Tanzania 🇹🇿 kuna uhalali huo, hiyo ni Tabia iliyoanzishwa na Wanasiasa kutafuta uteuzi. Sisi binadamu tukisifiwa sana uwa tunatabia ya kuwapa fedha au vyeo hao wanaotusifia, hivyo watu wengi wameona weakness hapo na ndipo wanatumia fursa hii kusifia, angalia wote wanaosifia ni wale wenye uteuzi au walioko chini ya rais... Na pia Chawa kama mwijaku na Baba levo wameibuka hapo baada ya kuona kusema asante na kusifia ni kuzuri. Lakini katiba yetu haisemi tusifie rais na kusema asante kwa kazi anazofanya, maana huo ni wajibu wake kama ilivyo kwa mwalimu
 
....Hata Nyumbani wanasema Asante kwa chakula..
Ili hali Ni jukumu lako Kama baba kuwapa chakula.
 
Si jambo geni kwa nchi zenye element za ukomunisti. Kiongozi anakuwa kama semigod
 
Tofautisha nyumbani ambapo wewe uchangii chochote, wewe ni kula kusoma na kulala...
Huku serikalini hawa wanalipwa kwa mishahara yetu wananchi, sisi ndio nguvu kazi... Sasa inakuwaje Sifa anapewa Rais wakati kazi zinafanywa na Raia, na pesa wanatoa Raia. Msanii akifanya vizuri kimziki utasikia asante Rais, utafikiri rais ndio katunga mashahiri
 
Si jambo geni kwa nchi zenye element za ukomunisti. Kiongozi anakuwa kama semigod
Ila sisi ni socialism (ujamaa), japo sera zinafanana na Communism (Ukomunisti), ila hata Urusi uwezi kuona Raia wanasema asante Putin, kwa Afrika hizi tabia naziona Tanzania tu maana hata jirani zetu sijawahi kuona hii ya kumtukuza Raia wakati ni wajibu wake
 
Kumekuwa na wimbi kubwa hususani Tanzania la baadhi ya watu na viongozi kumshukuru Rais kwenye mambo ambayo yametendwa na Raia.

Mfano Jana Usiku imepigwa mechi baina ya Tanzania na Algeria kwenye michuano ya kufuzu Afcon kwenda Nchini Ivory Coast (Cote D'Ivoire). Lakini cha kushangaza Sifa zote zinamwagwa kwa Rais. Tazama post ya Mbunge "Babu Tale" hapo chini.

View: https://www.instagram.com/p/Cw6KDfdorC2/?igshid=MzRlODBiNWFlZA==

Huu upuuzi uwezi kuuona Nchi zilizoendelea, hata hapo Kenya uwezi kuona huu upuuzi kwamba Wananchi wanafanya kazi yao, alafu Sifa zinaenda kwa Rais. Marekani au Uingereza uwezi kuona Timu ya taifa inashinda alafu Wananchi wanasema "We thank president Joe Biden" au "We thank Queen Elizabeth". Hata Kenya ni nadra sana kuona rais anapongezwa kwa kitu kilichofanywa na Raia.

Ikumbukwe kusema neno "Asante Rais kwa kufanya hivi" ni kama vile Rais ametoa msaada, wakati kiuhalisia hile ni nguvu ya Umma. Chochote anachofanya Rais ni Mali ya Umma, hata Fedha anazotoa ni Mali ya umma. Anachofanya Rais sio msaada bali ni wajibu wake kama Rais, kama vile Mwalimu anavyofundisha, Mwenyekiti wa mtaa anavyosaidia mtaa, Daktari anavyotibu na jinsi ilivyo kwa watumishi wengine wa serikali. Kitendo cha kusema asante Rais kwa kitu fulani, utafikiri asingekuwepo yeye tusingeweza ni ujinga wa watanzania ndio maana wanasiasa wanaendelea kujifanya miungu watu, kwa sababu wanapokea sifa ambazo kimsingi ni wajibu wao na kazi yao kuyafanya hayo kama ilivyo kwa watumishi wengine. Ndio maana hizi Asante uwezi kuziona kwenye Nchi zinazotambua Wajibu na Kazi (Duty and Responsibility) ya Raisi.

Pesa tumpatie sisi kupitia kodi, na akifanya maendeleo kwa Kodi zetu, tunaanza kumramba miguu na kusema Asante. Utafikiri Pesa ni zake, au alichofanya ni msaada. Rais anakuja kutuomba kura ili akatekeleze haya anayoyafanya, ni moj ya majukumu yake ambayo ndio yamemuweka madarakani na hasipoweza kuyafanya hayo basi ataondolewa madarakani kwa kushindwa kuyafanya. Hivi ndivyo nchi za demokrasia ufanya kazi, na si kushukuru serikali wakati ni wajibu wake kuwezesha kila sekta kupiga hatua.

Hizo ni tabia zinazotokana na mila zetu.

Labda nikuulize kwa mfano mdogo:
Je mtu akikuletea fedha "zako",
Akikuletea mke "wako",
Akikulipa deni "lako"
Akikukabidhi vitu "vyako"
Hauwezi kumwambia "ahsante"?

Kama utamwambia "ahsante", ni ya nini wakati ulicholetewa ni mali yako na ni halali yako?

Mimi ninavyofahamu, "ahsante" ni neno la pongezi ana shukurani ambalo hutolewa kwa "muwezeshaji" ili kumtia shime.

Hapo sasa mwenyewe utapima karika context hii kama hiyo "ahsante" inamhusu au ni ya kumlamba viatu!

Labda tuzilaani kauli zinazotolewa siku hizi za..."Rais katoa fedha"..."hela ya Samia" etc etc ni kauli potofu zisizostahili kutamkwa na watu wenye heshima zao!

Siku hizi hauwezi kusikia kiongozi akisema ..."serikali imetoa..." au ..."Serikali imechangia", ni mwendo wa kumtaja Rais moja kwa moja tena kwa jina!

Kauli hizi kutoka midomoni mwa viongozi zina maudhui ya upotoshaji wa makusudi na lengo lake ni kujipendekeza kulikopitiliza na huo ndiyo ulamba viatu tunaousema, cheo kikubwa kuliko cha uchawa!
 
Back
Top Bottom