sun wu
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 2,020
- 1,419
Hata hapa bongo zipo benki nyingi ambazo ukiweka pesa hata kwenye account ya Savings kawaida kila muda fulani unapata interest.
Tatizo lenu mmeshazoea benki zenu hizo 3.
Mkuu ni Benki gani hizo naomba uniambie na sio interest inakuwa senti mbili alafu wanakata service charge mia tatu..;
ngoja nikupe mfano ukiweka hapa pesa zako lets say elfu 3000 (CRDB) na ukiziacha ukirudi baada ya mwaka utakuta pesa yako yote ishaisha (kwa service charge wanayokata kila mwezi)
Ukiweka pesa yako lets say hata pennies (50p) kwenye Benki UK (iwe barclays, HSBC, TSB au yoyote ile) ukirudi baada ya mwaka utakuta hio 50p yako imezaa vi-pennies vingine (that's what am talking about)
Benki ni biashara ya kukopesha watu na makampuni na pesa za kukopesha inatoka kwa watu kama mimi na wewe na wengine wanaoweka pesa Benki.., hivyo kutumia pesa yangu kukopesha watu alafu wanikati pesa kila mwezi eti service charge ni wizi (inabidi mimi ndio wanipe interest kwa kuwasaidia kuzalisha faida)