Elections 2010 Je, Mtanzania gani anafaa kuwa Rais wetu 2010?

Nani anafaa kuwa Rais wa Tanzania 2010-2015?

  • Jakaya Mrisho Kikwete (CCM)

    Votes: 591 23.9%
  • Willibrod Slaa (CHADEMA)

    Votes: 1,785 72.1%
  • Ibrahim Lipumba (CUF)

    Votes: 89 3.6%
  • Hashim Rungwe (NCCR-Mageuzi)

    Votes: 7 0.3%
  • Mutamwega Mugahywa (TLP)

    Votes: 7 0.3%

  • Total voters
    2,475
  • Poll closed .
hata mimi ZIMWI ninafaa bora tu niwatumikie wananchi katika maadili yanayostahiki, pia niifuate katiba na sheria, niwakomboe kutoka kwenye umaskini wao, ila kwakuwa sina fursa hiyo sasa, anaefaa kwa mwaka huu ni DR. SLAA
 
Mtannzania,mcha Mungu na anayetambua kwa umakini kuwa lazima awe na abki kuwa KIONGOZI wa jamii yake ya Watanzania.Raisi wangu nataka niwe na uwezo wa kumjua uwezo wake kiutendaji na usimamizi wa watendaji wake lakini kikubwa Raisi ni yule atakayeweza KUSema na kauli yake ikazaa.
Mwenye uwezo mzuri kiakili ili upeo huo umsaidie kutosahau kuwa Tanzania,na rasilimali zake zisizohesabika zitabaki kuwa za watanzania na kwa watanzania zitatumika ili kurejesha ustawi na uimarikaji wa maisha ya jamii ya watanzania uliolegalega nakupotea kabisa kuanzia miaka ya themanini na hata sasa,Raisi anayeogopa kubadilisha uthamani wa Utanzania wetu kwa kuwakumbatia wakoloni ambao mababu zetu kwa thamani ya maisha na uhai wao wametuachia somo kuwa Wakoloni ni "UKOMA" huyo ndiye ninayemzungumzia hapa.
Raisi anayeogopa kutangaa kwa mabango kuwa 'anawajali' wazee kabla hawajapewa stahili zao wale waliotoa mchango wao katika iliyokuwa jumuia ya Afrika Mashariki ambayo pia,Mungu wangu!,ilifanywa isisonge mbele kwa sababu zilezile ambazo hazijatatuliwa,leo WATAWALA wa nchi hii wameturejesha kulekule likiwa ni wazo la watu wachache ambao tu wanauwezo wa kuamua hivyo na jambo likawa hivyo...
Tunamjua,tumemwona na kikubwa tunaimani kuwa yeye huyo niliyemzungumzia hapa ndiye atakayetusababishia watanzania tunaoiamini historia ya Dunia kuwa Mapinduzi ya kweli hayaletwi na chama,hayahitaji silaha wala umwagaji damu,hayahitaji vikao vya kuomba fedha kuwezesha mapinduzi husika,na kikubwa hayahitaji matangazo ya vyombo vya habari kutawanya ushawishi kwa wahusika,lakini yanahitaji MUDA ,wakati ni huu.
 
Ni Dr, Willibroad Peter Slaa anayeweza tu kututoa hapa tulipo maana yupo tayari kula mhogo ikulu kwa kuwatanguliza watanzania.Jk hana tofauti na Rostam Azizi, Luwasa na Basil Mramba.Tumia busara tusonge mbele.
 
Fuatilia mwenendo wa kampeni tu uatapata jibu.ukiona ile mikutano
ambayo hata wagonjwa wanatoroka kwenda kuisikiliza ndio hiyo itakayokupa rais
na siyo ile ya kubeba watu kwa malori.
 
Wilbrod slaa ndio mtanzania na mwanakondoo pekee aliteuliwa na mwenyezi mungu kuja kuokoa kilio cha watanzania wengi masikini angalau hali yao ya kimaisha itengemae. mi ni ccm damu lkn cwezi kutetea upuuzi kisa mie ccm.nawaambia wa tz wenzangu kwamba its time for change.... lets change jmn
 
Kikwete anao uzoefu na uadilifu wa kutosha, apewe fursa ya kumalizia miaka yake mitano iliyobaki, 2015 ndio tuwajaribu wapinzani!
 
This thing kenyan people being the most ugliest in Africa .hii ni upumbavu tupu lets have respect for one another
 
Mimi nafikili mtanzania anayefa kuwa rahisi kwanza awe nauchungu wa rasimali zetu,hamasa ya mandeleo,awe na huruka ya kutetea masirayi ya wantanzania ajuwe wapi tumetoka na wapi tuna enda na mwisho kuheshimu mila na dini za mtanzania
 
1. Hadi sasa naamini kuwa Rais J.K Kikwete :A S thumbs_up: bado anahitajika katika kipindi kingine kwa sababau zifuatazo;
- Serikali yake imeonesha uthubutu mkubwa wa kusimamia rasilimali za Taifa ipasavyo na hivyo kujiongezea idadi ya maadui waliokuwa na hesabu za kutumia kipindi chake kujineemesha hususan suala zima la kusitisha uingiaji wa serikali katika mikataba mipya hadi pale utaratibu mpya wenye maslahi kwa taifa utakapokuwa tayari. Sitisho hilo lilikuwa pigo kubwa kwa mafisadi waliokuwa wametum ia fedha nyingi wakati wa uchaguzi wa 2005 wakitarajia kuzirejesha kwa kutumia mikataba mibovu kwa maslahi yao binafsi. huo ulikuwa mwanzo wa kuanza kumchukia JK.
- Serikali yake imeopanua wigo wa uhuru kuongea na kuropoka kwa Wananchi kiasi cha kuwafanya wengi waonekane kama wehu na hata kusimama kukashfu Serikali yenyewe na Taifa bila woga.
- Masuala ya huduma za jamii kwa ujumla yameboreshwa ijapokuwa kuna mchwa wengi kupindukia katika ngazi ya serikali za Mitaa na halmashauri na manispaa ambao wamejijengea himaya ya kutafuna kila senti inayokwenda huko kwa ajili ya kuoboresha huduma za jamii hususan afya, elimu na Maji na hata kilimo pia.
- Ameongeza kasi kubwa ya uimarishaji wa miundombinu hususan barabara na umeme. kwa uzoefu kipindi hiki kuelekea November tungelikuwa tumeanza kutahadhalishwa juu ya mgao wa umeme na nchi kuingia gizani
- nk.
kimsingi, tatizo kubwa lililopo siwezi kulitofautisha sana na kipindi cha mwalimu Nyerere ambapo wakati yeye anasimamia kidete kubuni njia mpya na bora za kuwakomboa wananchi, alikosa wasaidizi wazuri wenye elimu na ujuzi katika ngazi zote kusaidia kusimamia mipango yake mizuri. Kwa kikwete yeye ana watalaam wengi wazuri ambao wanashindwa kutumia taaluma zao kusaidia kuinua uchumi wa nchi na sasa wamegeuka wasaliti na mchwa wakubwa. Wanasoma ili waweze kupata nafasi za kuhujumu nchi. Hii ni elimu ya wendawazimu. Wasomi wetu hawasaidii taifa lao. badala yake Wanalitafuna na kulidhalilisha. Natamani kuwatembezea bakola.
2. Nampa nafasi ya pili Slaa huku nikiwa na hasira naye. hasira zangu juu yake ni kuwa mbinafsi kwa kuamua kuacha nafasi muhimu ya ubunge na kuingia kwenye kinyang'anyiro cha urais huku akijua kuwa chadema ilikuwa bado haijawa na mtandao mpana wa kuweza kuingia ikulu. Ameniudhui kwa kuwa wananchi tutakosa bunge ambalo ameshiriki kwa kiwango kikubwa kurudisha hadhi yake kutokana na uwezo wake wa kutoa hoja zenye tafiti na kuzisimamia kidete. nina hasira naye kwa kuwa najua ni rahisi kwa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko yeye kuingia Ikulu kupitia chadema ambayo haijasimisha wabunge kwenye majimbo mengi. Sitaki kuwa mnafiki katika hili kwani hata mgombea urais wa UPDP akiwa kitandani leo asubuhi BBC anaeleza kuwa anauhakika atashinda huku akijua kuwa bado mgonjwa na hajaanza kampeni ambapo kampeni zinaelekea wiki ya mwisho.
3. Lipumba akiwa na chupa ya maji mkononi sina maoni naye hasa kwa bara kwa kuwa yeye amezoea kushindwa. katika hili amekomaa kwani hata yeye mwenyewe anajua ni wa kushindwa.
 
wengi wanakaa wana jiuliza kuwa matanzania gania anafaa kuwa rais hata kikwete anafaa hatata slaa anafaa kamami sina ubaya na kikwete wa slaa bali kuhusu kikwete kweli baada ya kuapishwa kama kweli ulisikia spech yake kwamba usimwone usoni kwamba anacheka lakini moyoni makali.kumbe fix miminilimpa kura yangu ila sasa hapati kwani biashara ya ubesti kwenye madaraka ndiyo kitu ambacho nimemwona hafai kwani ulimuliza kuna watuwangapi wanalala njaa,hawanakazi,hawana pembejeo,hawana nyumba ,hawana na bararara hajui.kituambacho ungemwambia magufuli hatakama amelala atakuambia kwanini ukiwa rais usiwape watu kama hao uongozi wajuuu kama waziri mkuu ambaye anaweza kukemee vitu.unakuja kumpa pinda ambaye anaendeshwa kwa fungu na bwana munduli kwani badao anapawa .nakuhakikishia kwamba kikwete akipita safarihii 2015 lowassa rais kwani ccm itamchagua lowasa chama kitagawanyika nahapo huyo jamaa anavyopenda kuwa rais hatamsimsaidie kwenye kampeni kama walivyo mkacha kikwete kipindihichi hatakubali kunyanganywa tonge mdomoni kwani anaurohoo wa madaraka
abuu
 
Anayefaa kwa huu ni Dr. aliyesomea, siyo Dr. wa kubandikwa kofia??? Watanzania tuamke, tubadilike maana dunia nzima imeshabadilka sasa. Hata hao wahisani wameshaona kama ni ujinga basi Mjomba amefanya ujinga wa ziada, kama wamefikia mahala pa kusema hatutoi hela maana mnachezea hamuoni wathungu wametuona sisi ni mapambaf wa kutupa? hiyo ni kazi ya mjomba JK, hana maana kabisa...kuliko mumpe JK tena leadership bora mumupe huyu jamaa aliyelala kitandani ambaye hajafanya kampeni, mtakuwa mmefanya bora kuliko kumpa tena JK. Msinielewe vibaya, simpigii kampeni mgonjwa ila ninachojaribu kusema ni kwamba JK ni useless kuliko huyo jamaa aliyelaa kitandani sasa hivi, na hata hivyo tunamjua ni mgonjwa maana ameshaanguka sio mara moja watu wakafanya juju zao hapo akaendelea, usimwone anatembea hakuna mtu hapo ni hewa inatembea. Bora huyu jamaa mgonjwa ni mtu ila ana tatizo na linajulikana na madaktari, sasa kinachomwangusha JK mnakijua??? Usitake kujua... Sala ~ "EE BABA TUNAKUOMBA USHUKE BONGO KESHOKUTWA TAREHE 31 OCT 2010 USHIKE MASANDUKU YA KURA MWENYE, YEYOTE ATAYEJARIBU KUFANYA LOLOTE KINYUME NA UTARATIBU NA APOOZE MKONO HADI KUFA KWAKE :amen:"
 
Wadau,

Nimekuwa nikifuatilia mijadala inayoendelea katika forum hii. Nataka kutoa changamoto kwa wadau wenzangu ili tujadili swali lifuatalo:


Je, ni mtanzania gani ana SIFA na VIGEZO vya kuiongoza Tanzania? Wachangiaji wanaweza kupendekeza majina MATATU.


Itakuwa vyema kama wachangiaji watatoa sababu zinazowafanya watoe mapendekezo hayo?


Nawasilisha hoja:

UPDATE:

Majina Matatu (makubwa) Yaliyopendekezwa:

  1. Jakaya Kikwete - CCM
  2. Willibrod Slaa - CHADEMA
  3. Ibrahim Lipumba - CUF

willibrod slaa
 
Mtanzania mwenye mtazamo wa maendeleo, asiyetetea rushwa, anayetumia akili za kuzaliwa na sio akili za kushikia na binadamu wengine, anayeweza tofautisha nchi yake na za wenzie kila mara anapoingia nchini kwakwe kutoka nchi endelevu,,,,asiyetetea uzembe wa watenda kazi wake........na nyingi ambazo marahisi wetu wa Africa especially nchi yetu hawanazo/hanazo!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Naungana Mkono na Himawari, yule anayeonekana anafaa machoni mwa wengi, ndani ya chama cha mafisadi anaonekana ni traitor. Mwana JF mmoja hapo juu amemtaja MAGUFULI kuwa mwenye guts and any other atrtibute you can mention, lakini nikueleze kuwa huyo mheshimiwa Dr. J.P. Magufuli hayupo kwenye list yao ya potential candidates kwa sababu jamaa ni mkali, atazima mirija yao yote. Kikubwa hapa (nionavyo mimi) nguvu ya umma pekee ndiyo itakayolikomboa taifa hili kutoka kwenye uozo huu wa CCM.

Naomba kuwasilisha
 
Utii bila Uhuru wa Kufikiri ni Utumwa
I like this slogan
yaha tukapige kula kikweli
 
Back
Top Bottom