Elections 2010 Je, Mtanzania gani anafaa kuwa Rais wetu 2010?

Nani anafaa kuwa Rais wa Tanzania 2010-2015?

  • Jakaya Mrisho Kikwete (CCM)

    Votes: 591 23.9%
  • Willibrod Slaa (CHADEMA)

    Votes: 1,785 72.1%
  • Ibrahim Lipumba (CUF)

    Votes: 89 3.6%
  • Hashim Rungwe (NCCR-Mageuzi)

    Votes: 7 0.3%
  • Mutamwega Mugahywa (TLP)

    Votes: 7 0.3%

  • Total voters
    2,475
  • Poll closed .
"Nafurahi kwamba asili yangu ni kijiji hiki kidogo masikini,nataka kusema hili kwa ajili ya historia,najisikia fahari kuzaliwa katika familia masikini na naahidi kwamba nitaishi maisha ya kimasikini na nitakufa nikiwa masikini".

Maneno hayo hapo juu yalitamkwa na mjamaa wa Kiarabu Abdul Nasser(rais wa kwanza wa Misri) akihutubia wananchi kijiji kwao.Nimenukuu maneno hayo kwa makusudi sana ili kuonyesha taswira ya kile nitakachokiandika katika makala hii.

Maneno hayo yanaweza kulaaniwa vikali na vijana wengi toka barani Afrika,wanaopenda kuwa matajiri wa haraka pasipo hata kufanya kazi kwa bidii na maarifa.Ukimuuliza kijana wa Afrika katika maisha yake angependa awe nani,haraka angesema,nyumba nzuri,gari nzuri,mke mzuri n.k.Ukimuuliza zaidi anapenda afanye kazi gani,bila shaka angetaja,uhasibu,uanasheria,udaktari,uinjinia n.k

Bila shaka kazi ya ualimu au pengine ukulima haiwezi kutajwa na jibu lake ni jepesi sana,vijana au Waafrika wengi wanapenda sana shughuli za utanashati na si za kuchafua mikono kama wakulima.Kazi za mikono na jasho hazipendwi kabisa batrani Afrika.Wakulima si tu wanapuuzwa na kudharauliwa bali pia wananyanyaswa na kukandamizwa na kikundi kidogo cha watu.

Katika hali ya joto kama Dar suti au makati hayabanduki kwenye miili ya maofisa,utathani pengine nchi kama Tanzania hamna shida kabisa,mbwembwe za mahakimu na mawakili wa serikali na wakujitegemea,ungethani pengine ndani ya mahakama kuna haki,utakuwa unajidanganya.

Askari wa barabarani ni mzaha mtupu wako tayari wapate Tshs 500 toka kwa makondakta kwa gharama ya vifo.Hapa Tanzania twaweza hasa kutangaza kuwa ajali za barabarani ni janga la kitaifa.Tumepoteza ndugu wengi kwa ajali za barabarani,lakini sijaona hatua madhubuti zikichuliwa na wateule wetu.

Kifupi kuna matatizo mengi katika maisha yetu ya kila siku,na pengine kutokana na uelewa wangu mdogo,sijaona hatua zozote zikichukuliwa.Nani anaweza kuwa kama Abdul Nasser wa sasa,nani aweza kuwa kama wana halisi wa Afrika kama Nyerere,nani ana uchungu na maisha ya watanzania,nani anaumizwa toka moyoni na hali za masikini waliotapakaa kote Tanzania.

Vipi wenzangu mnaonaje?naomba mnisaidie nimchague nani kuwa rais wa Tanzania,atakaye kuwa tayari kunywa mvinyo na sifongo na watanzania wote.Kwa kweli naomba msaada ndugu zangu.
 
Umebisha hodi hapa jamvini mkubwa? Ungeanzia kwenye juwaa la utambulisho mkubwa! Anyways, karibu!
 
Yaani wewe unachekesha wakati jibu unalo!
Wakatoliki wachache wasio na upeo watakwambia panga ndiye anafaa(yaani unajaribu jinsi ya kutumia rungu katika vita vya nyukilia!)Tusije mpa mbu kazi ya kutibu malaria.
Kumpa Padri madaraka ya urais katika nchi isiyo na dini(ila watu wake wana dini) ni sawa na kumpa mbu kazi ya kutibu malaria au fisi kulinda mizoga!
Ndugu yangu akili kichwani kwako hakuna atakaye kuja kukushikia kisu wakati wa kupiga kura,hao wote wanaolonga humu wengi wao hawatapiga kura kabisa wao wanakuzuga tuu eti chagua Padri kwavile tunasali naye kanisani lakini wakati wa matatizo hutowaona wakikusaidia!
 
Mchunguzi.

Junior Member
Join Date Tue Aug 2010
Posts 2
Thanks : 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power 0


Usiufunue upumbavu wako kwa kiasi hicho.... Ni ushauri wa bure tu.
 
Hii guys

whom do you think the best between Jakaya and Siraha.

Sarufi, sarufi Mkuu. Sintaksia na semantiki za wapi hizo? Hivi hao wanaowatuma hapa huwa wanawakusanya na kuwapa mafunzo wapi? Inaelekea ninyi, kiongozi wenu na walimu wenu hakuna tofauti khaaaaaaaaaaaaa
 
"Kikwete (mgombea urais wa CCM, Jakaya), yupo kundi la kwanza la watu wenye akili kubwa si la tatu wala la pili (wenye akili za kawaida), ndiyo maana mpaka sasa amezunguka Mwanza, Kagera, Kigoma, Rukwa na Mbeya, anachofanya anaelezea Ilani ya chama, tumefanya nini tangu 2005 na tutafanya nini, si kuzungumza watu," alisema Makamba.
 
"Kikwete (mgombea urais wa CCM, Jakaya), yupo kundi la kwanza la watu wenye akili kubwa si la tatu wala la pili (wenye akili za kawaida), ndiyo maana mpaka sasa amezunguka Mwanza, Kagera, Kigoma, Rukwa na Mbeya, anachofanya anaelezea Ilani ya chama, tumefanya nini tangu 2005 na tutafanya nini, si kuzungumza watu," alisema Makamba.
Lakini mbona hajakataa kwamba hao watu ni mafisadi? Alafu ujue kwamba hawa majamaa wana miezi miwili kukuchosha na ahadi ambazo zitatekelezwa sio longolongo. (Mbona nimeskia eti uwanja wa ndege ya kimataifa sijui wapi tena, wakati Nyerere road ya kuelekea uwanja wa taifa Dar ina shida? - Ahadiism)

Naomba tushulikie vitu realistic kama mafisadi...
 
Dr Slaa.JPG
 
Yaani wewe unachekesha wakati jibu unalo!
Wakatoliki wachache wasio na upeo watakwambia panga ndiye anafaa(yaani unajaribu jinsi ya kutumia rungu katika vita vya nyukilia!)Tusije mpa mbu kazi ya kutibu malaria.
Kumpa Padri madaraka ya urais katika nchi isiyo na dini(ila watu wake wana dini) ni sawa na kumpa mbu kazi ya kutibu malaria au fisi kulinda mizoga!
Ndugu yangu akili kichwani kwako hakuna atakaye kuja kukushikia kisu wakati wa kupiga kura,hao wote wanaolonga humu wengi wao hawatapiga kura kabisa wao wanakuzuga tuu eti chagua Padri kwavile tunasali naye kanisani lakini wakati wa matatizo hutowaona wakikusaidia!

Ungali kijana hivi unaanza kuwa muflisi kwa kiwango hiki, ukizeeka si utatisha!
 
Raia Wa Tanzania, mwenye miaka zaidi ya 35, ana akili timamu, hajawahi kushtakiwa kwa uhalifu, na anayependekezwa na chama cha siasa.

MKJJ; hapo si sawa; chama kinaweza kuwa na sera mbovu, mlengo mbovu, matakwa mabovu, malengo mabovu ila kikatimiza masharti yako; je tumpe kura kwa kuwa ameletwa na chama? naomba uende deep kidogo nahisi hujajibu swali kama mlengwa anavyotaka;
 
ama kweli JF Chadema wamedominate, yangekuwa kwenye medani yako hivi pia ningewapa hongera




ila wapi, wapiga domo hapa tu. huko wana lolote walifanyalo
 
ama kweli JF Chadema wamedominate, yangekuwa kwenye medani yako hivi pia ningewapa hongera

Wamedominate si JF peke yake bali katika polls zote toka Daily News, Mwananchi, IPPmedia, Tanzania Daima hadi Michuzi blog. Kwa Watanzania wote wenye uelewa jibu la swali la Mtanzania gani anafaa kuwa Raisi wetu 2010 liko wazi wala halina mjadala. Ukweli ndio huo.
 
Mwaka huu Wagombea Wote Hawafai-


  1. Jakaya Kikwete - CCM "Ahadi nyingi"
  2. Willibrod Slaa - CHADEMA "Huyu Mchungaji Over Rated hana lolote huyu"
  3. Ibrahim Lipumba - CUF"King`ang`anizi wa Madaraka"
SIPIGI KURA!
 
Unataka majina au sifa? Kama ni sifa, turejee makala ya Ulimwengu na Hotuba ya Mwalimu Nyerere ya 1995 pale Mbeya. Kama ni majina, hapo tena ni kasheshe!

Mkuu kwa bahati mbaya wapiga kura wengi wanachagua sura si sifa!! Ingekuwa ni sifa basi mwaka huu wangefanya mabadiliko.

 
Back
Top Bottom