Zamani kidogo nilisoma kuwa mke wa hayati Jenerali Kombe aliyekuwa ameuwawa na Polisi kwa kumdhania ni jambazi alishitaki serikali kuwa imlipe mabilioni ya pesa. Alishitaki kwa kuwa waliokuwa wameuwa ni askari Polisi wa serikali, wakitumia bunduki na riasasi ya serikali wakiwa wamemfuatilia kwa kutumia gari la serikali. Marehemu Mwangosi naye aliuwawa na Polisi wa Serikali, kwa kutumia silaha za serikali, mbele ya RPC! Serikali yaweza kushtakiwa kumlipa fidia Mama yule aliyeuliwa mumewe, na watoto ambao wapoteza baba yao??