Je mke wa mwangosi aweza kuishitaki serikali kwa mauaji ya mumewe?

KIRUMO

JF-Expert Member
Sep 25, 2012
416
177
Zamani kidogo nilisoma kuwa mke wa hayati Jenerali Kombe aliyekuwa ameuwawa na Polisi kwa kumdhania ni jambazi alishitaki serikali kuwa imlipe mabilioni ya pesa. Alishitaki kwa kuwa waliokuwa wameuwa ni askari Polisi wa serikali, wakitumia bunduki na riasasi ya serikali wakiwa wamemfuatilia kwa kutumia gari la serikali. Marehemu Mwangosi naye aliuwawa na Polisi wa Serikali, kwa kutumia silaha za serikali, mbele ya RPC! Serikali yaweza kushtakiwa kumlipa fidia Mama yule aliyeuliwa mumewe, na watoto ambao wapoteza baba yao??
 
Kuishitaki serikali kwenye mahakama zipi, hizi hizi ambazo majaji wake wanateuliwa na Mkuu wa Magamba? Halafu Policcm inayoongozwa na shemeji wa M.k.w.e.r.e ndio ikajibu tuhuma mbele ya Jaji asiye hata na degree aliyepata nafasi hiyo kiushkaji? Labda akashitaki The Hague na siyo hapa! Wewe hujiulizi huyo mjane wa Kombe alishitaki? Na je, kwanini Zombe na Prof. Mahalu hawajaishitaki serikali kwa kuwachafua kwa kesi za kimagumashi? Ukipata jibu ndio ulitumie kujijibu!
 
Ndiyo, anaweza kuishtaki serikali lakini aonane na wanasheria wanawake wamsaidie,hakika atashinda......
 
Kuna uwezekano mkubwa wa kuishitaki serikali ili alipwe fidia kwa ajili ya madhara aliyoyapata kwa kuondokewa na mumewe kutokana na kitendo cha mauaji ya makusudi au uzembe wa polisi ambao wameajiriwa na serikali.
Hata hivyo ni muhimu kuwaunganisha polisi waliohusika, wakuu wao waliotoa taarifa mbalimbali, waziri na kamati yake pamoja na serikali kama mwajiri wao. Ushahidi utakuwa wazi kabisa!
 
Zamani kidogo nilisoma kuwa mke wa hayati Jenerali Kombe aliyekuwa ameuwawa na Polisi kwa kumdhania ni jambazi alishitaki serikali kuwa imlipe mabilioni ya pesa. Alishitaki kwa kuwa waliokuwa wameuwa ni askari Polisi wa serikali, wakitumia bunduki na riasasi ya serikali wakiwa wamemfuatilia kwa kutumia gari la serikali. Marehemu Mwangosi naye aliuwawa na Polisi wa Serikali, kwa kutumia silaha za serikali, mbele ya RPC! Serikali yaweza kushtakiwa kumlipa fidia Mama yule aliyeuliwa mumewe, na watoto ambao wapoteza baba yao??

Nimekuwekeeni hukumu ya Kesi iliyofunguliwa na Mke wa Jenerali Kombe ili iwe mwanga katika majadiliano yatayowezesha mke wa Mwangosi kupata haki. Isome na utaona ni jinsi gani haki ikitafutwa kwa nguvu inawezekana kupatikana.
 
Attachments

  • Kombe.doc
    50 KB · Views: 76
Nashukuru. Nimesoma leo kuwa familia ya marehemu Mwangosi wameanza kuchukua hatua ya kufungulia serikali mashtaka! THank U Caren!
 
Huyo mama atulie tu ajue ni jinsi gani ya kulea wanae
Huwezi kufananisha inshu ya kombe na mwangosi
Huyu ni mke wa aliyekuwa mkuu wa usalama wa taifa
Huyu ni mke wa aliyekuwa mwandishi wa habari (asiuejulikana) kajulikana baada ya kifo

Connection aliyokuwa nayo kabla na baada ya kifo cha mumewe mke wa kombe na connection aliyekuwa nayo na anayo mke wa mwangosi ni tofauti
 
HAki haiangalii rangi,uwezo au kujulikana kwa mtu.Uhai wa mtu haununuliwi binadamu wote tunahaki sawa.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom