Je, mbunge wako anawakilisha kile ulichomtuma bungeni?

Wild fauna

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
461
189
Heshima kwenu wakuu,
Hivi mbunge wako uliyempa kura yako anatimiza kile ulichomtuma pale bungeni?

Binafsi mbunge wangu mzee Lyatonga Mrema naona anajitahidi japo haendani na spidi ya sasa ila ananipa matumaini,anasinzia bungeni ila halali kama wabunge wengine ninaowaona.

Vipi kuhusu mbunge wako? Ni vizuri ukamtaja kwa jina ili akipita huku aweze kujirekebisha.

wakuu naomba kuwasilisha.
 
Mbunge wangu ni Mnyika wa Ubungo. Si kumbuni ni lini amewahi kupeleka jambo lolote bungeni kuhusu Ubungo. Amekuwa ni mbunge wa taifa. Yeyey ni mtu wa hoja binafsi na kuomba miongozo. Kuwa mbunge usie obsessed ukadhani sasa wewe ni mkuu wa nchi unajua kila kitu mawazo yako binafsi ni muhimu kuliko mipango ya nchi inayoandaliwa na wataalamu waliobobea. Ajwahi kuonekana jimboni zaid ya kuja kufungua matawi ya CHADEMA. Ametulate down sana huyu kijana na asubiri maamuzi yetu mepesi uchaguzi mkuu ujao.
 
Umeniwahi aisee, mi pia ni mkazi wa jimbo la ubungo.kwakweli nadhan tulimchagua mbunge wa miongozo.bila ushabiki kwakweli mnyika hajafanya matarajio ya wapiga kura wake.
 
Heshima kwenu wakuu,
Hivi mbunge wako uliyempa kura yako anatimiza kile ulichomtuma pale bungeni?

Binafsi mbunge wangu mzee Lyatonga Mrema naona anajitahidi japo haendani na spidi ya sasa ila ananipa matumaini,anasinzia bungeni ila halali kama wabunge wengine ninaowaona.

Vipi kuhusu mbunge wako? Ni vizuri ukamtaja kwa jina ili akipita huku aweze kujirekebisha.

wakuu naomba kuwasilisha.

Mbunge wangu Mwigulu Nchemba, binafsi nilishiriki kwenye kampeni 2010, yeye hapa mimi hapa.....tulitoa sana rushwa makanisani na n.k.....nakumbuka kule Mgongo, Shelui na Ntwike tulivyotisha kwa rushwa ya makanisani tukiipa jina la sadaka......Sasa nikaamini mbunge wangu atatubu haya kwa kuleta maendeleo kwa Wanaramba, ila waaaapi mpaka sasa bado tunasubiri, Wananchi wananiuliza ''kuwadi'' wake kuwa BOSI WAKO TULIMTUMA KUWA MBUNGE, MBONA AMEJIPA UWAZIRI NA ANAISEMEA SANA SERIKALI, WAKATI TULIMTUMA KUIHOJI?
 
Mbunge wangu ni Mnyika wa Ubungo. Yeyey ni mtu wa hoja binafsi na kuomba miongozo. ....... Ametulate down sana huyu kijana na asubiri maamuzi yetu mepesi uchaguzi mkuu ujao.

Mkuu pengine unadhani ikiitwa hoja binafsi, basi ni yake na familia yake, HAPANA ni hoja binafsi kwa ajili ya jimbo lake na taifa kwa ujumla....hoja binafsi ya maji haikuwa kwamba maji yajae kwenye madiaba yake nyumbani bali Dar, Ubungo na Bongo pia
 
Mbunge wangu Tibaijuka.Mama huyu niwakimataifa na ya kienyeji yanamkwaza.Kwenye kata yetu Muleba Kusini eneo la Kasharunga na Kyamiorwa alituhaidi mengi na angalau kuna mafanikio tatizo ni wapambe wake tunaomba angalau awe anatutembelea kabla ya bunge.Akicheza kiti kitamponyoka.Katika uongozi wako wa sasa serikali inaleta umeme jimboni mwako kupitia Mamlaka ya Umeme vijijini-REA mama jitahidi kata yetu ipate transformer manake ukiondoka na umeme utaondoka.Kuhusu maji safi hilo sitalisemea ingawaje tunataabika sana na mito yote inakauka.Mama kama wapambe wanazuia tusikuone tupe cimu zako au barua pepe tuwe tunakutwangia.Mungu awe nawe
 
Mbunge wangu ni Mnyika wa Ubungo. Si kumbuni ni lini amewahi kupeleka jambo lolote bungeni kuhusu Ubungo. Amekuwa ni mbunge wa taifa. Yeyey ni mtu wa hoja binafsi na kuomba miongozo. Kuwa mbunge usie obsessed ukadhani sasa wewe ni mkuu wa nchi unajua kila kitu mawazo yako binafsi ni muhimu kuliko mipango ya nchi inayoandaliwa na wataalamu waliobobea. Ajwahi kuonekana jimboni zaid ya kuja kufungua matawi ya CHADEMA. Ametulate down sana huyu kijana na asubiri maamuzi yetu mepesi uchaguzi mkuu ujao.

Mwaisoba hebu muogope mungu , hivi suala la maji halihusu jimbo la ubungo ?
 
Mi mbunge wangu ni yule anaeshtuliwa usingzini kila siku bungeni, anaitwa NTUKAMAZINA. Yeye huwa anaenda bungeni kuchukua posho na kuchapa usingizi. NGARA to RULENGE HOYEEEEEEEE!
 
Mimi mbunge mwenyewe hata sijawahi msikia akiongea chochote na alishatukana sisi wananchi wa segerea kwamba hatujamchagu(ni kweli kwani alichakachua)makongoro......
 
Mbunge wangu ni Mnyika wa Ubungo. Si kumbuni ni lini amewahi kupeleka jambo lolote bungeni kuhusu Ubungo. Amekuwa ni mbunge wa taifa. Yeyey ni mtu wa hoja binafsi na kuomba miongozo. Kuwa mbunge usie obsessed ukadhani sasa wewe ni mkuu wa nchi unajua kila kitu mawazo yako binafsi ni muhimu kuliko mipango ya nchi inayoandaliwa na wataalamu waliobobea. Ajwahi kuonekana jimboni zaid ya kuja kufungua matawi ya CHADEMA. Ametulate down sana huyu kijana na asubiri maamuzi yetu mepesi uchaguzi mkuu ujao.

daa huo ni unafiki mtupu ukisia hoja binafsi ujue ni kwa maslahi ya jimbo lako tatizo ulilonalo wewe ni uelewa mdogo wa mambo ya kibunge mfano wa hoja ya juzi ya mnyika kuhusu maji ilikuwa kwa ajiri ya maji ambayo ni tatizo kwa wakazi wa ubungo
 
Mbunge wangu Mh. Wenje yupo cool sana bungeni.....
mara ya mwisho sijui ilikuwa lini kumuona!!!
 
Mzee wangu wakiraracha anajitahidi kupiga mzigo na pale bungeni wamemfanya kama mtu wa kuchangamsha na kuchekesha halaiki.huwa hana jipya yeye huzungumziaga zile zile stor zake za kuwa naibu wazir mkuu wa kwanza,amekamata dhahabu airpot,amepandisha bei ya kahawa huku marangu,
 
Mbunge wangu vincent nyerere,amejitahidi sana kutekeleza ahadi zake jimboni hasinzii bungeni tunamshukuru kwa kuisimamia serikali mradi mkubwa wa maji uneanza pia ujenzi wa hosp ya kwangwa!mungu azidi kumbariki
 
Mbunge wangu ni mheshimiwa Joseph Selasini, kwa kiasi fulani anajitahidi ila bado hajafikia kasi ya B.P. Mramba katika shughuli za maendeleo.Tatizo lake kubwa selasini kahamia DAR na haji Rombo kuhimiza suala la maendeleo, itabidi vijana wa CDM waanze kujipanga kutafuta mbadala wake 2015!
 
Mimi mbunge wangu nilimsikia siku moja tu akiuliza swali na baada ya hapo hata la nyongeza hakuuliza natamani kuwa na wabunge kama mnyika, zito, lema, lisu sema sasa jamii inayonizunguka sioni jinsi ya kuwapata wabunge kama hao
 
Mbunge wa jimbo langu mwigulu nchemba aka mzinzi-kazi yake ushirikina na kukomaa na wake za watu.
 
Back
Top Bottom