Je, Marekani inawezaje kupata kuaminiwa tena na nchi za Afrika?

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111413952025.jpg

Mkutano wa pili wa wakuu wa Marekani na nchi za Afrika umekamilika hivi karibuni mjini Washington. Vyombo vya habari vya kimataifa vinaona baada ya miaka minane, Marekani inatupia macho yake tena katika bara la Afrika, madhumuni yake halisi ni kugeuza Afrika kuwa uwanja wa mashindano kati ya yake na nchi nyingine zenye nguvu haswa China.

"Wazo la kushindana" ambalo haliwezi kufichwa katika serikali ya Marekani inayoongozwa na rais Biden bila shaka litafanya watu kujiuliza kama nchi hiyo inaweza kuzingatia maslahi ya nchi za Afrika.

Tukiangalia ahadi alizotoa Bw. Biden wakati wa mkutano huo wa kilele, ni rahisi kuona kwamba sera ya sasa ya Marekani kuhusu Afrika haina kitu kipya wala udhati, na inaiga moja kwa moja mipango ya China ya kuhimiza maendeleo ya Afrika.

Kama mifano inayofuata: Marekani imedokeza kuwa itajadiliana na Afrika kuhusu upatikanaji wa soko chini ya Sheria ya Ukuaji na Fursa ya Afrika AGOA. Sheria hiyo ilipitishwa mapema mwaka 2000 kwa lengo la kuruhusu baadhi ya bidhaa za kiafrika kuingia Marekani bila ushuru.

Hata hivyo chini ya sheria hiyo, mauzo ya nje ya Afrika kwa Marekani yameendelea kupungua katika miaka ya hivi karibuni. Ikiwa imesalia miaka miwili tu kabla ya sheria hiyo kuisha mwaka 2025, kwa nini Marekani iliileta tena kwenye mjadala?

Kwa sababu unafiki wake umefichukuliwa kutokana na vitendo halisi vya China. Katika miaka ya hivi karibuni, kiwango cha biashara kati ya China na Afrika kimeendelea kukua, na China imejitahidi kupanua uagizaji wake wa bidhaa zisizo za maliasili kutoka Afrika.

Katika mwaka mmoja tu uliopita nchi 18 za Afrika zilizopatiwa hadhi ya kutotozwa ushuru kwa bidhaa zake na serikali ya China. Katika miaka mitatu ijayo, China itaagiza bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 300 kutoka Afrika.

Mwaka jana, China ilitangaza kuwa itatekeleza na Afrika kwa pamoja "miradi tisa" ikiwa ni pamoja na mradi wa uvumbuzi ili kuzisaidia nchi za Afrika kunufaika na maendeleo ya kidijitali. Katika mkutano huo wa kilele kati ya Marekani na Afrika, Marekani pia ilieleza nia yake ya kuunga mkono maendeleo ya kibunifu ya Afrika.

Bw. Biden naye alitangaza binafsi kwamba nchi yake itawekeza dola bilioni 350 barani Afrika kwa mabadiliko ya kidijitali. Lakini Ikulu ya Marekani baadaye ilirekebisha nakala ya hotuba ya Biden, ikisema uwekezaji halisi utakuwa milioni 350.

Kiwango cha pesa ambacho rais Biden alitaja kimepungua kwa mara elfu, wakati huu wa aibu tayari imeenea duniani kote na kwenye ripoti za vyombo vya habari vya Marekani. Wakati huo huo, ili kuibembeleza Afrika, Bw. Biden pia alieleza kuunga mkono Umoja wa Afrika kujiunga na G20.

Lakini halisi halisi ni kuwa katika mkutano wa kilele wa G20 wa mwaka huu, China ilikuwa nchi ya kwanza kuunga mkono hadharani kwa Umoja huo kujiunga na G20.

Ni dhahiri kuwa iwe katika nyanja za uchumi, uvumbuzi au uhusiano wa kimataifa, Marekani inatunga sera zake za Afrika kwa kuzingatia dhamira ya kuikabili China, jambo ambalo linasababisha kukosekana kwa mkakati wa muda mrefu, kauli mbiu kubwa na uwezekano mdogo wa kutimiza ahadi yake.

Safari hii, mkutano wa kilele kati ya Marekani na Afrika umefanyika katika muktadha wa kuzorota sana kwa uhusiano baina ya pande hizo mbili. Mwaka jana, dunia nzima ilikuwa katika hali mbaya ya janga la COVID-19. Nchi za Afrika zilikuwa na mahitaji makubwa kuhusu chanjo.

Hata hivyo hata kama ziada ya chanjo ndani ya nchi hatimaye ilipelekea kuisha muda wake, nchi za Magharibi zilisita kuipatia Afrika mwanzoni.

Baadaye kwenye mgogoro kati ya Russia na Ukraine, Marekani iliiwekea vikwazo Russia bila kuzingatia misukosuko wa chakula na nishati inayoweza kutokea barani Afrika, na hata kutishia kwamba nchi za Afrika zitaadhibiwa kama "hazitasimama pamoja" na Marekani.

Hatua hizo za Marekani zilizipuuza nchi za Afrika. Taasisi ya Afrika Kusini ya Institute For Global Dialogue hivi karibuni ilichapisha ripoti ikisema kwa Afrika, mvuto na ushawishi wa Marekani umepungua kwa kiasi kikubwa, na nchi za Afrika zina sababu ya kuwa na wasiwasi kwamba Marekani kurudi tena barani Afrika kunaweza kuvuruga siasa za Afrika.

Wakati huo huo, nchi na watu wengi wa Afrika wana matumaini zaidi kuhusu ushirikiano na China. Utafiti wa vijana wa Afrika wa mwaka 2022, unaonesha kuwa takriban asilimia 77 ya vijana wa Afrika wanaamini kuwa China ndiyo nchi ya kigeni yenye ushawishi chanya zaidi barani Afrika.

Ikiwa Marekani inatarajia kutumia mkutano huo kuunda fursa ya kuwasiliana tena na nchi za Afrika ili kupata kuaminiwa tena, basi inapaswa kuthibitisha kwa vitendo kwamba ufuatiliaji wake juu ya Afrika unatokana na nguvu za Afrika ambazo hazijatumiwa ipasavyo na kwa ajili ya mustakabali wa Afrika, wala sio kwa kuitegemea Afrika kujipatia maslahi katika ushindani wa kimataifa.

Kama alivyosema Cameron Hudson, mtaalam wa masuala ya Afrika katika Taasisi ya Masuala ya Kimkakati na Kimataifa ya Marekani" Ni kwa sababu ya China, kuna barabara nyingi barani Afrika, viwanja vya ndege vipya vinaibuka, na watu wengi wanatumia simu za mkononi. Mambo hayo yamehimiza maenedeleo halisi ya Afrika."
 
Hakuna nchi ya kijinga na ya kinafiki kama marekani, kimsingi iko kwa maslahi yake na kujijali wala sio win win.
Kwa sasa vitabya Ukraine imeilazimisha Marekani kuigeukia Afrika, jambo ambalo Afrika inatakiwa isinunue wazo la USA.

Mfano mzuri ni kuweka vikwazo kwa nchi za afrika isijipatie mahitaji toka Urusi huku yeye akiendelea kununua malighafi kama Uranium toka Urusi kama hitaji muhimu la nchi yake.

Afrika haikuwa na sababu ya kuendelea kilia kwa upungufu wa fuel wakati yao mafuta ya bei ndogo kule urusi, ifike sehemu Afrika ijitambue na kuwa na maamuzi, Afrika iache kujikomba bora tuishi kwa shida miaka kadhaa lkn tujipanga kwa maendeleo yetu na kwa uhuru.

D3mokrasia inayohubiriwa na Marekani si demokrasia ikiwa itaenda tofauti na matarajio ya USA yenye tija kwake
 
Hakuna nchi ya kijinga na ya kinafiki kama marekani, kimsingi iko kwa maslahi yake na kujijali wala sio win win.
Kwa sasa vitabya Ukraine imeilazimisha Marekani kuigeukia Afrika, jambo ambalo Afrika inatakiwa isinunue wazo la USA...
Wapi US wameweka vikwazo kwa nchi za Africa isipate mahitaji toka Urusi? Maneno mengi lakini bakuli la ombaomba wapeleka US na si China au Urusi.
 
Rejea mkutano wa waziri wa mambo ya nje wa Russia na rais wa Uganda kuhusu kununua mafuta ya Russia, na baadae Marekani kuweka tishio la vikwazo nchi za Afrika zitako nunua mafuta Urusi. Na zaidi ikamtuma balozi wake nchini Uganda aongee na Museveni na ndipo Uganda ikatoa kauli ya kutonunua mafuta kutoka Urusi.
 
View attachment 2453218

Mkutano wa pili wa wakuu wa Marekani na nchi za Afrika umekamilika hivi karibuni mjini Washington. Vyombo vya habari vya kimataifa vinaona baada ya miaka minane, Marekani inatupia macho yake tena katika bara la Afrika...
Hivi mbona sijawahi kusikia nchi za asia au America kusini Kwanini bado waafrika tunatumika hivi bado hatuamini kama tumefanywa kama chombo cha kuwavusha wengine Kwa nini lakini.
 
View attachment 2453218

Mkutano wa pili wa wakuu wa Marekani na nchi za Afrika umekamilika hivi karibuni mjini Washington. Vyombo vya habari vya kimataifa vinaona baada ya miaka minane, Marekani inatupia macho yake tena katika bara la Afrika, madhumuni yake halisi ni kugeuza Afrika kuwa uwanja wa mashindano kati ya yake na nchi nyingine zenye nguvu haswa China.

"Wazo la kushindana" ambalo haliwezi kufichwa katika serikali ya Marekani inayoongozwa na rais Biden bila shaka litafanya watu kujiuliza kama nchi hiyo inaweza kuzingatia maslahi ya nchi za Afrika.

Tukiangalia ahadi alizotoa Bw. Biden wakati wa mkutano huo wa kilele, ni rahisi kuona kwamba sera ya sasa ya Marekani kuhusu Afrika haina kitu kipya wala udhati, na inaiga moja kwa moja mipango ya China ya kuhimiza maendeleo ya Afrika.

Kama mifano inayofuata: Marekani imedokeza kuwa itajadiliana na Afrika kuhusu upatikanaji wa soko chini ya Sheria ya Ukuaji na Fursa ya Afrika AGOA. Sheria hiyo ilipitishwa mapema mwaka 2000 kwa lengo la kuruhusu baadhi ya bidhaa za kiafrika kuingia Marekani bila ushuru.

Hata hivyo chini ya sheria hiyo, mauzo ya nje ya Afrika kwa Marekani yameendelea kupungua katika miaka ya hivi karibuni. Ikiwa imesalia miaka miwili tu kabla ya sheria hiyo kuisha mwaka 2025, kwa nini Marekani iliileta tena kwenye mjadala?

Kwa sababu unafiki wake umefichukuliwa kutokana na vitendo halisi vya China. Katika miaka ya hivi karibuni, kiwango cha biashara kati ya China na Afrika kimeendelea kukua, na China imejitahidi kupanua uagizaji wake wa bidhaa zisizo za maliasili kutoka Afrika.

Katika mwaka mmoja tu uliopita nchi 18 za Afrika zilizopatiwa hadhi ya kutotozwa ushuru kwa bidhaa zake na serikali ya China. Katika miaka mitatu ijayo, China itaagiza bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 300 kutoka Afrika.

Mwaka jana, China ilitangaza kuwa itatekeleza na Afrika kwa pamoja "miradi tisa" ikiwa ni pamoja na mradi wa uvumbuzi ili kuzisaidia nchi za Afrika kunufaika na maendeleo ya kidijitali. Katika mkutano huo wa kilele kati ya Marekani na Afrika, Marekani pia ilieleza nia yake ya kuunga mkono maendeleo ya kibunifu ya Afrika.

Bw. Biden naye alitangaza binafsi kwamba nchi yake itawekeza dola bilioni 350 barani Afrika kwa mabadiliko ya kidijitali. Lakini Ikulu ya Marekani baadaye ilirekebisha nakala ya hotuba ya Biden, ikisema uwekezaji halisi utakuwa milioni 350.

Kiwango cha pesa ambacho rais Biden alitaja kimepungua kwa mara elfu, wakati huu wa aibu tayari imeenea duniani kote na kwenye ripoti za vyombo vya habari vya Marekani. Wakati huo huo, ili kuibembeleza Afrika, Bw. Biden pia alieleza kuunga mkono Umoja wa Afrika kujiunga na G20.

Lakini halisi halisi ni kuwa katika mkutano wa kilele wa G20 wa mwaka huu, China ilikuwa nchi ya kwanza kuunga mkono hadharani kwa Umoja huo kujiunga na G20.

Ni dhahiri kuwa iwe katika nyanja za uchumi, uvumbuzi au uhusiano wa kimataifa, Marekani inatunga sera zake za Afrika kwa kuzingatia dhamira ya kuikabili China, jambo ambalo linasababisha kukosekana kwa mkakati wa muda mrefu, kauli mbiu kubwa na uwezekano mdogo wa kutimiza ahadi yake.

Safari hii, mkutano wa kilele kati ya Marekani na Afrika umefanyika katika muktadha wa kuzorota sana kwa uhusiano baina ya pande hizo mbili. Mwaka jana, dunia nzima ilikuwa katika hali mbaya ya janga la COVID-19. Nchi za Afrika zilikuwa na mahitaji makubwa kuhusu chanjo.

Hata hivyo hata kama ziada ya chanjo ndani ya nchi hatimaye ilipelekea kuisha muda wake, nchi za Magharibi zilisita kuipatia Afrika mwanzoni.

Baadaye kwenye mgogoro kati ya Russia na Ukraine, Marekani iliiwekea vikwazo Russia bila kuzingatia misukosuko wa chakula na nishati inayoweza kutokea barani Afrika, na hata kutishia kwamba nchi za Afrika zitaadhibiwa kama "hazitasimama pamoja" na Marekani.

Hatua hizo za Marekani zilizipuuza nchi za Afrika. Taasisi ya Afrika Kusini ya Institute For Global Dialogue hivi karibuni ilichapisha ripoti ikisema kwa Afrika, mvuto na ushawishi wa Marekani umepungua kwa kiasi kikubwa, na nchi za Afrika zina sababu ya kuwa na wasiwasi kwamba Marekani kurudi tena barani Afrika kunaweza kuvuruga siasa za Afrika.

Wakati huo huo, nchi na watu wengi wa Afrika wana matumaini zaidi kuhusu ushirikiano na China. Utafiti wa vijana wa Afrika wa mwaka 2022, unaonesha kuwa takriban asilimia 77 ya vijana wa Afrika wanaamini kuwa China ndiyo nchi ya kigeni yenye ushawishi chanya zaidi barani Afrika.

Ikiwa Marekani inatarajia kutumia mkutano huo kuunda fursa ya kuwasiliana tena na nchi za Afrika ili kupata kuaminiwa tena, basi inapaswa kuthibitisha kwa vitendo kwamba ufuatiliaji wake juu ya Afrika unatokana na nguvu za Afrika ambazo hazijatumiwa ipasavyo na kwa ajili ya mustakabali wa Afrika, wala sio kwa kuitegemea Afrika kujipatia maslahi katika ushindani wa kimataifa.

Kama alivyosema Cameron Hudson, mtaalam wa masuala ya Afrika katika Taasisi ya Masuala ya Kimkakati na Kimataifa ya Marekani" Ni kwa sababu ya China, kuna barabara nyingi barani Afrika, viwanja vya ndege vipya vinaibuka, na watu wengi wanatumia simu za mkononi. Mambo hayo yamehimiza maenedeleo halisi ya Afrika."
Ivi vitu vyote ni msaada kutoka USA:-
1. ARV ( Drugs for inhibit virology growth)
2. Coca cola (
3. WhatsApp
4. Facebook ( Meta)
5. Instagram
6. Gmail address
7. Window operating system
8. IOS
9. iPhone
10. Android
11. Shazam
12. Vaccine for human being, animals & plants

Bado unaongea upuuuzi wa kujitegemeea na wakati ivyo vyote USA anatupa Kama msaada na kufanya spy ya nguvu
 
Bila shaka wewe ni zao la kipofu kwenye uzao wa viziwi.
 
Ivi vitu vyote ni msaada kutoka USA:-
1. ARV ( Drugs for inhibit virology growth)
2. Coca cola (
3. WhatsApp
4. Facebook ( Meta)
5. Instagram
6. Gmail address
7. Window operating system
8. IOS
9. iPhone
10. Android
11. Shazam
12. Vaccine for human being, animals & plants

Bado unaongea upuuuzi wa kujitegemeea na wakati ivyo vyote USA anatupa Kama msaada na kufanya spy ya nguvu
Humu jamii forum watu huwa wanajiropokea tu kama walevi wa mataputapu.
 
Back
Top Bottom