Je kwanini tunafoka?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,968
156,214
Mwalimu Mbobezi wa Saikolojia akiwa anafundisha kuhusu mahusiano, aliwauliza wanafunzi wake. Kwanini tunafokea na kukaripia tunapokuwa tumekasirika? Kwanini watu wanafokeana na kukaripiana kwa sauti kubwa?

Wanafunzi wakafikiri kwa muda, mmoja akasema, ni kwa sababu tunakuwa tumepoteza utulivu wa nafsi na hasira inakua juu sana. Lakini Mwalimu akauliza tena, sasa kwanini ushauti na kupiga kelele kwa nguvu wakati yupo hapo jirani yako na hayuko mbali?

Je haiwezekani kuongea nae kwa utaratibu na kwa sauti ya chini? Kwanini unapiga kelele kwa mtu akiwa amekuudhi?

Wanafunzi waliendelea kumjibu lakini hakuna hata mmoja alietoa jibu la kumridhisha Mwalimu.

Baadae, Mwalimu akawaelezea hivi, "pale watu wawili wanapokua na hasira kila mmoja na mwenziwe, kisaikolojia kunakuwa na umbali wa mioyo yao.

Kuweza kucover huo umbali, lazima wafokeane kwa nguvu na kwa sauti ya juu ili waweze kusikilizana. Jinsi wanavyokua wanazidi kupata hasira na ndio jinsi watazidi kupaza sauti zao kwa sababu na umbali wa mioyo yao unaongezeka.

Baada ya hilo jibu Mwalimu akauliza tena, "Inatokea nini pale watu wawili wanavyopendana? - akajijibu kwa kusema kwamba "hawawezi kukaripiana ila wataongea taratibu na kwa lugha laini, kwanini? Ni kwa sababu kisaikolojia mioyo yao ipo karibu kabisa.

Distance ya mioyo yao ni ndogo mno. Mwalimu akaendelea, "pale watavyozidi kupendana zaidi, nini kinatokea? Hawataongea, watanong'ona tu hata kama wakiongea kwenye simu, na watazidi kuwa karibu mno katika mapenzi yao.

Na mwishowe hawatahitaji kunong'ona tena, bali wataangaliana tu na basi kila mmoja atapata ujumbe kutoka kwa mwenzake hasa kwenye tendo la ndoa.

Hivyo basi, mtambue kwamba pale mnapogombana na wapenzi wenu mnatengeneza kaumbali fulani kati ya mioyo yenu na ya wapenzi wenu. Na ndivyo taratibu mnavyoua mahusiano yenu.

Kukwaruzana kwenye mahusiano hakukosekani, ila ni vema mkasuruhishana mapema na kurudi katika hali ya kawaida.

Mungu akabariki mahusiano yenu, akawaondolee kila aina ya kikwazo, mkaishi kwa furaha na upendo huku mkizikumbuka zile nyakati za mwanzo wakati mapenzi yenu yakianza!!

Si vibaya tukisema 'AMEN!
 
Ubarikiwe mleta uzi, hizi ndizo aina za makala zinazopaswa kuwepo hapa JF mara kwa mara, makala zinazoweza kubadilisha tabia na maisha ya watu. Mkuu nina hakika kuna asilimia fulani ya waliosoma makala hii itakuwa imepungua ya wenye tabia ya kufoka ovyo baada ya kuwa wamejifunza kitu fulani hapa. Hongera Mkuu
 
mijitu inakera sana wacha tu tufoke, hebu fikiria MTU unamfokea halafu anacheka, utajisikiaje.
Ahahahahahahaa wengine tupo tofauti Ni Bora tukae unieleze makosa yangu nitakuelewa na nitaomba samahani, lakini ukifoka nitacheka tu, hadi utajiona mjinga
 
Sasa kwanini mbwa wanabwekeana? Na wenyewe mioyo iko mbalimbali? Na kama mioyo ikiwa mbali watu wanafokeana, vipi kuhusu maini?
 
Back
Top Bottom