auferet dominus
JF-Expert Member
- Jul 18, 2017
- 1,805
- 1,286
Tatizo mmekaririshwa na wachungaji kuwa ubatizo ni LAZIMA kumwagiwa maji. Yesu alibatizwa akiwa na umri wa miaka kadiri ya 30, kwa hiyo na ninyi mnasubiri ifike miaka hiyo ndio mbatizwe? Kwa nini mnabatizwa mkiwa na umri wa miaka 20, au 23, au 25 au 27?
Yohana Mbatizaji alisema,
“7Naye alihubiri akisema, “Baada yangu anakuja mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, ambaye mimi sistahili hata kuinama na kufungua kamba za viatu vyake. 8Mimi ninawabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.” Marko 1:7-8
Sisi Roman Catholics tunatoa Sakramenti ya Ubatizo (kuondoa dhambi ya asili) kwa umri wa watoto wachanga, na watakapokua wanakuja kurudia kiapo cha ubatizo kupitia Sakramenti ya Kipaimara (mapaji ya Roho Mtakatifu), kukamilisha alichosema Yohana Mbatizaji kuwa "lakini yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu"
Wabatizeni Watoto wadogo
Tatizo mmekaririshwa na wachungaji kuwa ubatizo ni LAZIMA kumwagiwa maji. (Ubatizo lazima uwe wa kuzamishwa majini wala sio kumwagiwa maji. refer the word baptizmo la kilatini) Yesu alibatizwa akiwa na umri wa miaka kadiri ya 30, kwa hiyo na ninyi mnasubiri ifike miaka hiyo ndio mbatizwe? Kwa nini mnabatizwa mkiwa na umri wa miaka 20, au 23, au 25 au 27? (hili ni fundisho la kibiblia kubatizwa wakati watu wameshaelewa na kuamini sio kufata mafundisho ya kipagani. ref Marko 16:15-16: 15. Akawaambia, “Nendeni ulimwenguni kote, mkawahubirie watu wote Habari Njema. 16. Ye yote atakayeamini na kubatizwa ataokolewa),
Yohana Mbatizaji alisema,
“7Naye alihubiri akisema, “Baada yangu anakuja mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, ambaye mimi sistahili hata kuinama na kufungua kamba za viatu vyake. 8Mimi ninawabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.” Marko 1:7-8 (hapa umequote tu biblia lakini hatuoni hoja. hakuna panaposema ukawabatize watoto. hilo fungu linawahusu watu wanaotubu, kuamini na kubatizwa na hao ni watu wazima na sio watoto)
Sisi Roman Catholics tunatoa Sakramenti ya Ubatizo (kuondoa dhambi ya asili) kwa umri wa watoto wachanga, na watakapokua wanakuja kurudia kiapo cha ubatizo kupitia Sakramenti ya Kipaimara (mapaji ya Roho Mtakatifu), kukamilisha alichosema Yohana Mbatizaji kuwa "lakini yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu" (hakuna kitu kinachoitwa dhambi ya asili ndugu. hayo ni mapokeo ya kipagani na hayapo kibiblia. biblia ndio neno la Mungu linalofundisha mapenzi ya mungu sio kitabu kingine)
Wabatizeni Watoto wadogo (Msifanye ushetani huu mtapotea. watoto wako salama hata watakapo tambua baya na jema)