Je, kwa Wakristo yawezekana kumbatiza mtoto ambaye amezaliwa pasipo wazazi kufunga ndoa?

Pablo Blanco

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
7,328
6,591
Hivi inawezekana kumbatiza mtoto wa nje ya ndoa???? Kwa mfano Mimi na single mother wangu tunaweza kwenda kumbatiza mtoto ambaye tumemzaa bila kufunga ndoa?????
 
Hivi inawezekana kumbatiza mtoto wa nje ya ndoa???? Kwa mfano Mimi na single mother wangu tunaweza kwenda kumbatiza mtoto ambaye tumemzaa bila kufunga ndoa?????
Ndio kama huyo ni mtoto wenu wa kwanza au wa pili kwa wakatoliki. Kule wanauliza mmefunga ndo? Je huyu ni mtoto wenu wa ngapi? Ukishindwa kumbatiza sasa angali mtoto unasubiri mtoto akifikisha miaka kumi na kitu anaenda kubatizwa mwenyewe na kupewa sakramenti za ubatizo, komunio ya kwanza na kipaimara siku moja. Nayo hii ya pili sio ajabu kwani historia inaoneshwa wakristo wakatoliki walikuwa wanabatizwa wakiwa watu wazima hadi karne ya tatu ndio kanisa likaanza kubatiza watoto kwa mashariti yabkuwa na wasimamizi wa ubatizo au walezi wa kiimani na pia wazazi lazima wawe watu wa imani kama mtu anabatizwa akiwa mtoto. Pia kama mambo magumu mtoto akikaribia kufa kabla hajabatizwa basi katekisimu katoliki inasema kanisa linaruhusu mtu yeyote hata asiyekuwa mkristo anaweza kumbatiza mgonjwa afe akiwa mkristo alietubu. Mwisho nakukumbusha yapo makanisa mengi ya kipentekoste hubatiza waumini hadi wanapokuwa watu wazima wanajitambua. Yesu mwenyewe alibatizwa akiwa mtu mzima na Yohane Mbatizaji.
NB: Funga ndoa acha uzinzi na michepuko.
 
Mi nafahamu ktk ukristo wangu kuwa mtoto amabaye hajajua mema na mabaya habatizwi na kama alibatizwa haimaanishi chochote kwa huyo mtoto. Anayetakiwa kubatizwa ni mtu ambae ametubu. Tubuni mkabatizwe. Tena ni katika maji mengi. Haya mkristo mwenzangu mi ndo nshapita hapo
 
Ndio kama huyo ni mtoto wenu wa kwanza au wa pili kwa wakatoliki. Kule wanauliza mmefunga ndo? Je huyu ni mtomto wenu wa nagapi? Ukishindwa unasubiri mtoto akifikisha miaka kumi na kitu anenda kubatizwa mwenyewe na kupewa sakramenti zote. Nayo hii ya pili sio ajabu kwani historia inaoneshwa wakristo wakatoliki walikuwa wanabatizwa wakiwa watu wazima hadi karne ya tatu ndio kanisa likaanza kubatiza watoto kwa mashariti yabkuwa na wasimamizi wa ubatizo au walezi wa kiimani na pia wazazi lazima wawe watu wa imani kama mtu anabatizwa akiwa mtoto. Pia kama mambo magumu mtoto akikaribia kufa kabla hajabatizwa basi katekisimu katoliki inasema kanisa linaruhusu mtu yeyote hata asiyekuwa mkristo anaweza kumbatiza mgonjwa afe akiwa mkristo alietubu. Mwisho nakukumbusha yapo makanisa mengi ya kipentekoste hubatiza waumini hadi wanapokuwa watu wazima wanajitambua. Yesu mwenyewe alibatizwa akiwa mtu mzima na Yohane Mbatizaji.
NB: Funga ndoa acha uzinzi na michepuko.
mstari wa7 kutoka chini umeongopa!
 
Ndio kama huyo ni mtoto wenu wa kwanza au wa pili kwa wakatoliki. Kule wanauliza mmefunga ndo? Je huyu ni mtoto wenu wa ngapi? Ukishindwa kumbatiza sasa angali mtoto unasubiri mtoto akifikisha miaka kumi na kitu anaenda kubatizwa mwenyewe na kupewa sakramenti za ubatizo, komunio ya kwanza na kipaimara siku moja. Nayo hii ya pili sio ajabu kwani historia inaoneshwa wakristo wakatoliki walikuwa wanabatizwa wakiwa watu wazima hadi karne ya tatu ndio kanisa likaanza kubatiza watoto kwa mashariti yabkuwa na wasimamizi wa ubatizo au walezi wa kiimani na pia wazazi lazima wawe watu wa imani kama mtu anabatizwa akiwa mtoto. Pia kama mambo magumu mtoto akikaribia kufa kabla hajabatizwa basi katekisimu katoliki inasema

kanisa linaruhusu mtu yeyote hata asiyekuwa mkristo anaweza kumbatiza mgonjwa afe akiwa mkristo alietubu.
sasa muislam /budha n.k(asiye mkristo) anambatizaje mkristo?,katekisimu gan uliyosoma wewe hiyo hebu weka hapa
 
sasa muislam /budha n.k(asiye mkristo) anambatizaje mkristo?,katekisimu gan uliyosoma wewe hiyo hebu weka hapa
Mkuu kama hoja yenyewe ndio hii wala sijakosea. Kwanza tafuta uzi humu kuna mdau analipongeza kanisa katoliki la huko Arusha kwa kukataa kumzika tajiri wa Naura Springs na Impala hoteli. Mdau kalizungumzia hili jambo kwa urefu. Pili mimi ninacho kitabu kidogo kinacho zungumzia kuhusu ubatizo wa watoto. Na tatu kama unao muda kasome katekism kamili sio kile kitabu kidogo ulichopewa wakati unasoma mafundisho. Kile ni summery tu ya katekism yenyewe ambayo ni kitabu kikubwa hasa page zaidi ya 300. Nne pitia hii link hapo chini:
Can only Christians administer baptism? | Catholic Answers.
Maelezo ya hiyo link yapo kama ifuatavyo
Full Question
Can only Christians administer baptism?
Answer
No. Anybody—even an atheist—can administer baptism if he has the proper intention. According to the Catechism of the Catholic Church (CCC 1256) "the intention required is to will to do what the Church does when she baptizes, and to apply the Trinitarian baptismal formula." The reason anybody can baptize is that it is, in fact, Jesus Christ who performs the baptism. Once again, baptism is God’s grace to us, not our work for him.
 
Watoto wadogo hawabatizwi ni upagani ulioingizwa ndani ya kanisa na watu wanaufuata bila kujua na wengine wanajua ila hawajui cha kufanya.

Anaebatizwa ni mtu mzima anaeweza kumwamini Yesu, akamkubali na akatubu dhambi zake . Je mtoto mdogo aweza kufanya hayo???
 
Mkuu kama hoja yenyewe ndio hii wala sijakosea. Kwanza tafuta uzi humu kuna mdau analipongeza kanisa katoliki la huko Arusha kwa kukataa kumzika tajiri wa Naura Springs na Impala hoteli. Mdau kalizungumzia hili jambo kwa urefu. Pili mimi ninacho kitabu kidogo kinacho zungumzia kuhusu ubatizo wa watoto. Na tatu kama unao muda kasome katekism kamili sio kile kitabu kidogo ulichopewa wakati unasoma mafundisho. Kile ni summery tu ya katekism yenyewe ambayo ni kitabu kikubwa hasa page zaidi ya 300. Nne pitia hii link hapo chini:
Can only Christians administer baptism? | Catholic Answers.
Maelezo ya hiyo link yapo kama ifuatavyo
Full Question
Can only Christians administer baptism?
Answer
No. Anybody—even an atheist—can administer baptism if he has the proper intention. According to the Catechism of the Catholic Church (CCC 1256) "the intention required is to will to do what the Church does when she baptizes, and to apply the Trinitarian baptismal formula." The reason anybody can baptize is that it is, in fact, Jesus Christ who performs the baptism. Once again, baptism is God’s grace to us, not our work for him.
Ndo maana nasemaga Catholics are not Christians. Kwa imani yangu Ubatizo unamaana kubwa sana kwa Mkristo, sio swala rahisi rahisi kama wanavyofanya hawa waroma. Kanisa la roma nimebadilisha misingi mingi ya bibilia ili kuendana na matakwa yao ndo maana mambo mengi wanafanya kutokana na vitabu vyao tofauti na bibilia. Swala la kubatiza watoto halipo popote kwenye bibilia au swala la kubatiza mgonjwa kabla hajafa ili awe mkristo halipo kwenye bibilia.
Marko 16:15-16
15. Akawaambia, “Nendeni ulimwenguni kote, mkawahubirie watu wote Habari Njema. 16. Ye yote atakayeamini na kubatizwa ataokolewa,

Kwanza inaanza na kuamini, kisha ndio kubatizwa, kwamaana nyingine hakuna kubatizwa mpaka kuamini, Wanatakiwa waamni nini? wakaamini habari njema. Sasa mtoto mdogo awezaje kuamini habari njema ndo akabatizwa?

Matendo 2:38 ''Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake YESU KRISTO,

Mtu akisha amini anatakiwa atubu, kisha ndo abatizwe, Je mtoto anatubu nini ili abatizwe?

Neno ''ubatizo'' linatokana na Neno la kigiriki ''Baptizo'' ambalo katika kiingereza ni ''Baptism'' Lenye maana ya Zamisha kwenye maji.

Yohana 3:23 ''Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa.'' (maji tele sio maji kwenye kikombe, watu wakamwendea sio watoto wakapelekwa).

Marko 1:9-10
9 Baadaye Yesu akaja kutoka Nazareti katika sehemu ya Gali laya, akabatizwa na Yohana katika mto wa Yordani. 10 Yesu alipo toka kwenye maji aliona mbingu zikifunuka na Roho wa Mungu anam shukia kama njiwa.
 
sasa muislam /budha n.k(asiye mkristo) anambatizaje mkristo?,katekisimu gan uliyosoma wewe hiyo hebu weka hapa
Mkuu nakuongezea maarifa. Ninayo katekismu yenyewe nimekupigia picha uone kama kiingereza kina shida nitakutafutia kwa kiswahili. Ona picha za kama ushahidi uliodai.
20170919_094726.jpg
20170919_095024.jpg
 
Back
Top Bottom