Je kupenda kuwa alone ni ugonjwa?

Braza Kede

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
1,819
3,492
Mtu haumwi homa yoyote ya kuonekana.

Hana tatizo la afya ya akili (Ukichaa).

Anafanya kazi zake vema tu.

Sio mgomvi/mkorofi

Anajihisi huru mwenye raha na furaha anapokuwa yuko mwenyewe "alone"

Je mtu kama huyo yuko sawa au ana shida ya namna yoyote ile inayohitaji matibabu?
 
Ugonjwa ni nini ?

Inawezekana waliomzunguka ni incompatible; wanamzingua tu bora akae na mawazo yake
 
Mtu haumwi homa yoyote ya kuonekana.

Hana tatizo la afya ya akili (Ukichaa).

Anafanya kazi zake vema tu.

Sio mgomvi/mkorofi

Anajihisi huru mwenye raha na furaha anapokuwa yuko mwenyewe "alone"

Je mtu kama huyo yuko sawa au ana shida ya namna yoyote ile inayohitaji matibabu?
Kama hafanyi chukizo lolote kwa wanaomzunguka na jamii na anafanya mambo yake yanaenda au anaendelea kupambania na haumwi hiyo fresh tu
 
Mara nyingi huwa ni tatizo la kisaikolojia(afya ya akili)

Kuna levels mbalimbali za tatizo hilo, kuna wengine inaweza isionekane madhara yake moja kwa moja kwasababu maisha yao yanakwenda fresh na hana matatizo na mtu

Kiasili binadamu ni social animal yaani maisha yetu ni maisha ya kujumuika na tegemezi kwa wengine

Mtu anayependa kuwa peke yake muda wote anakua na tatizo la kisaikolojia
Mara nyingi sana anakua HAJIAMINI anajihisi hayupo SAWA anajihisi Tofauti au anajiina ANAUDHAIFU fulani na anaogopa hicho anacho hisi kinaudhaifu kitawakwaza au kitajulikana na wengine.

Lakini pia fear of rejection nayo ni shida kubwa inayo wakabili watu wapweke
Yaani anaona akitongoza, akitaka urafiki na mtu, akijieleza, akiomba kitu ATAELEWEKA NA KUKUBALIKA?
Kuepuka hayo anaamua kua mpweke

Kuna sababu nyingi ila kimsingi ni tatizo la Afya ya akili
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom