Je kuna umuhimu wowote kumuandalia Chakula mumeo wakati housegirl yupo?

Mapenzi ni zaidi ya kufanyiwa hiki na kile maana hiyo ni conditional love. Mfano wengine waume zetu hawapendi mikono yetu iwe migumu na sura ziharibike maana mama ndo pambo la nyumba. Kuepusha hayo wao pia husaidia kufanya kazi, so twafanya kwa kusaidiana na kurahisisha baadhi ya mambo kwa ku mechanise nyumba through various machine pale uwezo unaporuhusu. Mama na baba huwa viongozi kwa nyakati tofauti na wakati mwingine kwa pamoja pale wawapo nyumbani. Housegirl ni part ya watoto wetu ila yeye huwa mkubwa wa watoto maana yu mkubwa ki umri na wote hufanya haya kwa upendo bila one kuwa mtumwa na wengine kuwa mabwana.

he kwani mdada ulivyokuwa kwenu ulikuwa hufanyi hata kakazi kidogo? mie nadhani ni makubaliano/mlivyozoeshana wanandoa.
 
Ndo maana mimi nasema wanawake hawapaswi kutulaumu sisi wanaume pindi unapo amua kuchukua mtu mwingine azibe nafasi yaani utakuta housegirl ndie anae fua na kukunyoshea,anakuwekea maji bafuni,anakuandalia chai nzito, anakuandalia msosi bab kubwa,ndie anae ratiba shughuli zote za home pale usafi kumwagilia maua, ana wabembeleza watoto na kushinda nao kazi ya wife nini hapo kama sio bed room tu.
Jamaa nilimpongeza sana kwa kuchukua house girl na kumtimua wife maana wife alionekana hakuna kazi anayo ifanya nyumbani hata kuosha vyombo anashindwa kila kitu house girl yeye ni kugombeza tu house girl kwa nini umevunja glass kwa nini kochi kitambaa kimedondoka aaah akapigwa chini chini.

kwangu mie napenda zaidi kumuandalia mr kila inapowezekana, cwezi kuwa home then house boy ndio mtayarishie chakula na mambo mengine kumuhusu mr wangu, kama kupac nitapac na mengineyo!kama cpo sawa.
 
Tabu ni pale mume anapoanza kuzidai huduma hizi kwa nguvu kama vile ni haki kwake kutumikiwa mfano kama ndo ulikuwa unamfulia nguo zake za ndani siku waumwa, umesafiri basi ukijarudi hata kama ni wiki utakuta zimerundikwa bafuni jamani hivi kweli ukiingia kuoga na kufua utakatika mikono?

Ah mengine mmazidisha bwana hapana.
 
Wakuu ebu nisaidieni kuna umuhimu wowote kumwandalia chakule mumeo wakati housegirl/houseboy yupo na analipwa kwa ajili ya kuhakikisha kila kitu kuanzia usafi hadi chakula kinaenda vizuri?

...hakuna umuhimu wowote, fanya ile kitu roho inapenda.
 
Kumwandalia kama huna kazi nyingine ya kufanya. Kama watoto wanalia na wanahitaji kuogeshwa basi beki tatu inaanda msosi wewe unadeal nahizo totozi. la sivyo mwenyewe apeleke maji kwani hana mikono. Msiwandekeze hao wanaume ooh! mimi wangu anafanya bwana na hivi anajua ninavyonyonywa damu na mwajiri wangu. ila weekends ndiyo nafanya yote peke yangu beki tatu na watoto wanaenda kutembea.
 
...mnh, :) haaaaya!...
 
Nadhani mwelekeo wa changamoto zote zinaelekea kwenye "gender issues" - mara nyingine mtoto wa kiume katika familia nyingine hafanyi kazi e.g. hafundishwi kupika, kufua, kupasi nguo, kusafisha nyumba etc. hata kama anasoma boarding school, akirudi likizo kuna tendency ya wazazi wengine kumfundisha mtoto wa kiume MFUMO DUME - na hii inamjengea hali fulani kuwa kazi za nyumbani ni za dada zake (watoto wa kike) anakuwa nayo hiyo hali hadi anapofikia wakati wa ndoa - na hapo utaona wengine akitoka kazini - anakaa sebuleni - viatu anaacha hapo hapo, soksi etc. mentality ya kuwa kazi za nyumbani zote ni za mwanamke sio sawa. Ukisoma katika Biblia - kitabu cha Mwanzo - Mungu akasema "si vyema mtu huyu (adamu) awe peke yake; nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye" .................... hivyo mwanamke ameumbwa awe msaidizi wa mwanaume - majukumu mengi ni ya mwanaume ila mwanamke ni msaidizi - ndio maana she is more delicate, more soft etc. Katika ndoa (upendo) inatakiwa mambo ya-balance - swala ni kupendena na kusaidiana - sio mmoja kufanyiwa kila kitu - mwanaume gani utapenda mkeo achoke wakati wewe hujachoka? kuna wanaume wengine wanajua kupika kuliko hata wanawake - kiasi cha kutumia recipes mbalimbali za kupika - inapendeza kukaa mezani na kula chakula kilichopikwa na sometimes baba sometimes mama - by the way katika nchi nyingine - especially scandavian countries - wana ndoa hupika kwa zamu - how about that - shida ni pale mmepanga rooms - baba akianza kupika kwenye kundi la wanawake wengine ............ haipendezi - ila kama mko kwenye nyumba yenu wenyewe - mna uamuzi wa kusaidiana kama Mungu alivyokusudia. La sivyo mama akae nyumbani (atawe tu) na mwanaume ahangaike kutwa nzima alete chakula na mahitaji na atakuta mwanamke amepika, amefua etc. Kitu ambacho ni kigumu kwa wakati huu kwani wanawake wengi wana elimu, madaraka, biashara etc. kama wanaume - kikubwa ni UPENDO na yote yanakuwa marahisi.
Nawasilisha
 
Last edited:
kwangu mie napenda zaidi kumuandalia mr kila inapowezekana, cwezi kuwa home then house boy ndio mtayarishie chakula na mambo mengine kumuhusu mr wangu, kama kupac nitapac na mengineyo!kama cpo sawa.

Hehehe eti Nyamayao tuambie siri ya wewe kuwa na houseboy badala ya housegirl nasikia wengi wenu mmejeruhiwa kwi kwi kwi.
 
MFUMO DUME huo. Mwanamke haolewi ili atumikishwe kazi. Kunatakiwa kusaidiana ama sivyo atakuwa kama Punda.

Naku support kabisa! Kwani imeandikwa wapi kazi za mke ni hizo?:confused: Ninaona tu na utasikia kwenye vicheni party, 'umpokee mumeo akitoka kazini, umwekee maji...............' najiuliza wanajuaje mke atakuwa asharudi kazini? Vijijini ndo usiombe ni zaidi ya punda,mke akalime,akatafutte kuni ,atafute mboga,arudi apike,awatunze watoto na aamtunze mtoto mkubwa! PUU :(
 
Dada lazima ahusike,unless huja ajiriwa au hujajiajiri,cha muhimu
ni kumuelekeza jinsi ya kupika vizuri,vinginevyo uache kazi,na kama unampango wa kusoma au kujiendeleza kielimu usahau.
 
Wakuu ebu nisaidieni kuna umuhimu wowote kumwandalia chakule mumeo wakati housegirl/houseboy yupo na analipwa kwa ajili ya kuhakikisha kila kitu kuanzia usafi hadi chakula kinaenda vizuri?

Je, mm nilimuoa Housegirl au....? Ndio maana mnaachika kwa kutojua majukumu yenu...Kwa hiyo chakula kikiwa kitamu nimsifie nani? Housegirl au ww (mke wangu)?
 
kumruhusu housegirl kumwandalia chakule mumeo si nzuri sana, labda itokee mara chache wakati we uko busy na mambo mengine otherwise utakuwa unatengeneza bomb, mpende mmeo. unaona kazi kumwandalia chaluka mmeo ? yes sometimes unaweza ukawa umechoka so jitahidi ushirikiane na house girl
 
Kuna watu wako kigender equality zaidi. Wanawake wenye hekima na akili, pamoja na vyeo vyao wanahakikisha chakula cha familia kinaandaliwa na yeye akiwepo. Hata asipokuwepo atahakikisha anaacha maagizo nini cha kuandaa. Na ndoa sio zote zina kanuni moja, anachoongea mwenzako sicho na we ukiige.
 
Kila nyumba ina utaratibu wake..

Kila mume na ghubu lake (Haroooo).

Mi naitaga ghubu... ile mi sili mpaka apike wife...mi sili mpaka aniandalie wife...mi nguo zangu house girl agusi ni maghubu tu hayo. Ila kama mumeo analo utafanyaje sasa...muandalie tu bishosti usije twangwa talaka. Lol.
 
mimi mpaka maji ya kunawa nioshwe na wife
hilo ni gubu kuumbee?
 
Sitashangaa hata ID 'The Boss' sidhani kama uliichagua by mistake. Lol.

Napenda wanaume simple nyie ma ghubu a.k.a complicated ntawaweza wapi mie.

Lakini kama ulikua ukimuona baba ana act U Boss na wewe si ndo unajua kuwa mwanaume ni kuoa mke wa kukuhudumia kama mtoto.

Mume wangu alinisaidia kufua nilipoenda kusalimia kwao kwa mara ya kwanza...mbele ya mama yake na bibi yake...nilikazana kumkonyeza aache akasema hamna noma wala nini. Na wazazi wake wala hawakujali...hivyo malezi na makuzi yana matter.

Makuzi yes
wapo wanawake wanapenda hivyo
na wa kwangu anapenda hivi ninavyompeleka
fuuny baba yangu alikuwa so simple
hakuwahi kuwa na hata kuandaliwa chakula chake

mimi kila kitu ni custom made lol
 
Okay...basi ni makuzi upande wa wife. Lol.

Makuzi yes
wapo wanawake wanapenda hivyo
na wa kwangu anapenda hivi ninavyompeleka
fuuny baba yangu alikuwa so simple
hakuwahi kuwa na hata kuandaliwa chakula chake

mimi kila kitu ni custom made lol
 
Mi nimeoa na watoto ninao na house girl yupo, na anafanya kazi nyingi tu za kawaida za Nyumbani. Hata kuniandalia chakula pia anafanya. Binafsi Mimi sioni uhusiano uliopo Kati ya house girl kufanya kazi za Nyumbani na kukupasia na kukuandalia chakula na wewe baba Mwenye nyumba kumtamani. Ni tamaa tu wanaume wanatafuta njia za kuhalalisha tamaa walizonazo. Sasa Kama mke wangu anasaidiwa kila kitu na house girl na hatimaye mke anapata muda mzuri Wa kujiweka swaafi na kunipa burudani kuna ubaya gani? Cha msingi Ni kufuata haki za binaadam house girl asifanyishwe kazi Kama punda.
 
Back
Top Bottom