Je kuna umuhimu wowote kumuandalia Chakula mumeo wakati housegirl yupo?

MFUMO DUME huo. Mwanamke haolewi ili atumikishwe kazi. Kunatakiwa kusaidiana ama sivyo atakuwa kama Punda.

Aaaah kwa kazi gani nazo zitazomchokesha? Mwanamke sharti achakarike mwanaume ni kama mtoto anataka kuenziwa na kutunzwa kwa kila hali

Sent from my BlackBerry 9100 using JamiiForums
 
Asante. Hapa nimejikuta napiga makofi. Nimekupenda bureeee.

Wewe ni kama mume wangu...mi najua kupika sana tu, ila mume wangu nimeshajua hapendi kila nikitoka kazini nishinde jikoni maana anajua kitakachofuata ni kwenda kulala wakati yeye anakoroma. Lol.

Ananijali na hataki nichoke ili tufurahishane bila excuses. Ndio maana tuka ajiri house girl. Lol. Division of labor.

Na house girl wangu namlea kibinadamu si kipunda. Kufua mashine...kupika kuna kila nyezo za kurahisisha kazi kama rice cooker, jiko la gesi ashindwe yeye.

Kazi anazofanya ni kazi ambazo hata mimi kama ningekuwa sina kazi ningeweza fanya bila msaidizi...ziko simplified. Na mshahara nampa wa maana. Na upendo juu kwa kutusaidia kutunza familia.


Mi nimeoa na watoto ninao na house girl yupo, na anafanya kazi nyingi tu za kawaida za Nyumbani. Hata kuniandalia chakula pia anafanya. Binafsi Mimi sioni uhusiano uliopo Kati ya house girl kufanya kazi za Nyumbani na kukupasia na kukuandalia chakula na wewe baba Mwenye nyumba kumtamani. Ni tamaa tu wanaume wanatafuta njia za kuhalalisha tamaa walizonazo. Sasa Kama mke wangu anasaidiwa kila kitu na house girl na hatimaye mke anapata muda mzuri Wa kujiweka swaafi na kunipa burudani kuna ubaya gani? Cha msingi Ni kufuata haki za binaadam house girl asifanyishwe kazi Kama punda.
 
Back
Top Bottom