Je kuna Ukweli Wadada/Wanawake wakiwa period ni wakali kwa waume /BF Wao?

Ngo

JF-Expert Member
May 25, 2010
284
51
Wana jamii kuna ukweli wowote kuwa wanawake wakiwa katika siku zao wanakuwa wakali zaidi kuliko siku zingine wakiwa kawaida. Nimeliona hili kwa mwenzi wangu, akiwa siku zake ni kitu kidogo tu anakuwa mkali ile mbaya, na hapo ndo anahitaji penzi lionyeshwe kwelikweli kuwa unampnda. Nimeongea na marafiki zangu wawili wenye wake wote wamekubali kuwa kuna mabadiliko ya tabia kipindi wenzi wao wakiwa katika siku zao. Je hii ni kweli ? Kama ni kweli, hii inakuwa imechangiwa na biological factors au ni tabia tu. Wadada/wamama na wakaka mnakaribishwa katika huu mjadala.
 
:confused2::confused2:

mmh sina uhakika ila kuna fununu nilizisikia kama sio hapa hapa JF kuwa wanakuwa na hamu sana wakati huo..........asa cjui ukali huwa ni matokeo kuwa hawawezi saidiwa ile huduma ama vipi?

Lakini wapo hapa hebu watujuvye
 
Ni vema ukavuta subira tuende kwenye field walau kwa miezi 3, then tuje na majibu......!
 
:confused2::confused2:

mmh sina uhakika ila kuna fununu nilizisikia kama sio hapa hapa JF kuwa wanakuwa na hamu sana wakati huo..........asa cjui ukali huwa ni matokeo kuwa hawawezi saidiwa ile huduma ama vipi?

Lakini wapo hapa hebu watujuvye

una uwongo wewe....sasa ukiwa na hamu ndio unafanyaje na hayo maporomoko....na wengine huwa wanaumwa sana tumbo n.k...nikusaidie kujua siku za hamu?
 
una uwongo wewe....sasa ukiwa na hamu ndio unafanyaje na hayo maporomoko....na wengine huwa wanaumwa sana tumbo n.k...nikusaidie kujua siku za hamu?

Huo ni muda wa kuwa karibu na wake/wapenzi wetu,kuwakumbatia,kuwasaidia kazi,kuwa wapole kwao,kuwachekesha.
 
We acha tu muda huo unaweza ukauliza swali hilo jibu utakalopewa ukiwa sio mvumilivu unaweza kujikuta unamlamba kibao maana hali wanayokuwa nayo wanaijua wao wenyewe.
 
una uwongo wewe....sasa ukiwa na hamu ndio unafanyaje na hayo maporomoko....na wengine huwa wanaumwa sana tumbo n.k...nikusaidie kujua siku za hamu?

Preta bwana wengine mnakuwa kama vile mmenyweshwa maji ya betri something small mnakuwa na attitude moja ya ajabu
 
Kwa nini...................kwa sie waume/bf zenu ndio tumesababisha?:confused2:

Siyo suala la wanaume kusababisha au la. Hii inatokana na mabadiliko ya hormones. Wengine ghubu linaanza karibia na period hadi baada ya kipindi hicho. Kwa hiyo ni suala la kawaida ila wakati mwingine wanapiliza na kuwa wakali kama nyuki! Ndo maana wanaume wengi wanaishi na wanawake ila hawawafahamu walau kwa 50%!
 
Ni ukweli kabisa kaka yangu, mimi ni mwanamke na hiyo hali huwa inanitokea lakini si kila mwezi na kuna miezi mingine hasira inakuwepo lakini si sana ila kuna miezi mingine lol hata mimi mwenyewe huwa najistukia sijui kwa wenzangu. Mfano mzuri toka jana nadhani ndio nakaribia basi nina hasira hapa usipime mpaka mwenyewe najishangaa kabisa yaani safari hii ni too much ningekuwa na mume ndani naona angehama nyumba kwa muda kwani nina hasira zisizo kipimo ila ninajitahid tu kuzishusha. Kwa hiyo nadhani ni hali ya kawaida kwa wanawake ingawa hata sisi wenyewe hatuipendi ila hatuna jinsi labda kama kuna mtaalamu atusaidie tunaweza kuepuka vipi hii hali
 
Ni kweli. Mtupende zaidi basi na kutusaidia kipindi hicho.

Wengine ukisema ujitahidi kuvumilia mwenzako ndio anakuwa kama vile amenyweshwa acid sasa kama mtu yuko period and she doesnt even want to see you unafikiri hapo utafanya effort gani, ila infidelity ndio maana zinaanzia sehemu nyingi sana
 
:confused2::confused2:

mmh sina uhakika ila kuna fununu nilizisikia kama sio hapa hapa JF kuwa wanakuwa na hamu sana wakati huo..........asa cjui ukali huwa ni matokeo kuwa hawawezi saidiwa ile huduma ama vipi?

Lakini wapo hapa hebu watujuvye

Maskini_Jeuri nafikiri hii period na yenyewe ni chanzo cha infidelity
 
Hii ni kweli kabisa na hasa inatokana na mabadiliko ya kihormone katika miili yao. Huo ukali sio kwa B/friend au mme tu hata mtu mwingine ukiingia katika anga zake vibaya utaipata fresh.
PIA INASEMEKANA WAKIWA NA UJAUZITO WANAKUWA WAKALI PIA.
 
Wengine ukisema ujitahidi kuvumilia mwenzako ndio anakuwa kama vile amenyweshwa acid sasa kama mtu yuko period and she doesnt even want to see you unafikiri hapo utafanya effort gani, ila infidelity ndio maana zinaanzia sehemu nyingi sana

Hili suala kama nilivyosema linatokana na mabadiliko ya hormones. Moving from estrogen at ovulation to progesterone peak before menses siyo kitu kidogo. Ni muhimu kuelewa na kuwasaidia. Binafsi nilikuwa nakwazika sana ila baada ya kuwa mtu mzima na kuelewa vizuri hizo dynamics naona ni kawaida tu. Hakuna justification kukimbilia nje kwani hata hao wa nje wana hormone cycles kama za wake zetu. Tofauti ni kuwa, kule nyumba ndogo watu hawaendi kipindi hicho vinginevyo wangeyaona hayo matatizo ya mood.
 
Back
Top Bottom