Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 19,708
- 59,872
UTANGULIZI
Kwa sasa dunia inabadilika sana, kila nchi inaweka mipango ya kuibadili miji mikokwe na kuwa miji ya kisasa. Kwa upande wa Dar es salaam, mji huu umekuwa ni wa zamani zana lakini miundombinu iliyo mingi bado ni ya kizamani kama mji ulivyo.
Tukianza na mfumo wa maji taka, tangu mji ujengwe hakuna jitihada zozote za kubadilisha miundo mbinu ya maji taka. Ndio maana mvua kidogo tu ikinyesha kunakuwa na mafuriko kila kona.
Upangiliaji wa Nyumba na majengo. Jiji na Dar es salaam ni kati ya miji iliyopangiliwa ovyo ovyo hapa duniani. Ujenzi wa nyumba ni holela hakuna hata plan yoyote. Kwahiyo mji umekuwa na makazi yasiyo na maana. Yakitokea majanga kama moto, kupata barabara ya kukufikisha moto ulipotokea inakuwa ni shida.
MPANGO WA KUJENGA NEW DAR ES SALAAM CITY
Kuweza kubadika bandika mipango ndani ya Dar es salaam, haitasaidia chochote. Maana tayari watu zaidi ya 7m wanaishi ndani ya Dar es salaam. Lazima kuwepo na juhudi za maana kuanzisha CIty Mpya ili kuwahamisha watu wote walipo Posta na Kariakoo kwenda kwenye mji huo mpya.
Tunaweza kabisa tukaanzisha Dar es salaam New city kule Kiembeni Forest iliyopo Bagamoyo.
GHARAMA ZA KUJENGA MJI MPYA WA DAR ES SALAAM
NImefanya utafiti kwa kuangalia miji mbalimbali mipya inayojengwa duniani na gharama zake.
1. King Abdullah Economic City
Huu mji upo Saudia Arabia. Mji huu mpya upo na ukubwa wa 173 km² yaani ni zaidi ya ukubwa wa Dar es salaam.
Gharama za kujenga mji huo mpya inakadiliwa kuwa $55 billion. Na unategemewa kuwa na wakazi 1.8 million.
Tayari First Stage ilikamilika mwaka 2010.
2. Dholera city - India
Huu nao ni mji unaojenga India na upo katika hatua za mwisho kabisa. Gharama zake ni $30 billion.
KWANINI TUJENGE MJI WA DAR ES SALAAM MPYA
Kwa sasa mji wa Dar es salaam ni vigumu sana kurekebisha maana uharibifu uliofanyika ni mkubwa sana. Cha msingi ni kuwahamisha watu na kubomoa majengo kisha kuujenga upya. Lakini hiyo hatua ya kubomoa majengo lazima tujenge Mji mwingine mzuri wa kuwavutia watu waende huko.
Ile posta inatakiwa kuvunjwa vunjwa na kujenga upya.
Kuweka budget ya $55 billion kwa mpango wa mika 20 siyo mbaya.
Je, inawezekana kwetu?