Je, kifo ni uzembe,bahati mbaya au mapenzi ya Mungu?

1. Hapana, hapangi kifo wala siye aliyesababisha watu waanze kufa - ndiyo sababu anaahidi kuwapatia watu uzima wa nnmilele.
2. Watu wakifa hawaendi mahali popote panapoitwa peponi bali wanaenda kaburini - ndiyo maana kuna siku ya kuwafufua watu toka makaburini
3. Shetani ndiye aliyesababisha watu waanze kufa na kuvuruga makusudi ya Mungu (kwa muda tu) - ndiyo maana Mungu anaahidi kumfutilia mbali shetani na wote wanaomfuata hivi karibuni
4. Kifo cha binadamu si mapenzi ya Mungu - kazi ya Mungu haina makosa, yenye makosa si kazi yake.
Swali jingine.

Em' acha ujinga wewe..! sasa wanaokufa maporini kwenye vita na hawazikwi nao wanafufuliwa tokea wapi..??!
 
point no.2 kwamba watu wakifa wanaenda kaburini...je hiyo roho inakwenda wapi??? kwani hiyo roho ikitoka kwenye mwili ndo tunasema mtu kafa na hana budu kuzikwa..je hyo roho inazikwa nayo???huwa najiuliza pia bila majibu ya uhakika.
Em acha ujinga wewe..! hakuna kitu kama roho..!
 
Nakubaliana nawe hapo namba 1,lakini no. 2. hakika mtu akifa kinachoenda kaburini ni mwili lakini roho huchukuliwa na kuwekwa sehemu ya mangojeo,yaani paradiso (peponi) kwa watakatifu na jehanumu ya mangojeo kwa wenye dhambi.

Yesu akamwambia,Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi. (sio makaburini) Luka 23:43
Zaidi angalia Ufunuo 20:4.

Hapo no. 3 nakubaliana na wewe.

Ni sahihi si mapenzi ya Mungu watu wafe,lakini kwa kadri dhambi zilivyozidi na miaka ya mwanadamu ilipungua hata kufikia 70.(Vinginevyo shetani anahusika kwa vifo visivyotarajiwa).

Asante mkuu
Hiyo roho imtokayo binadamu unaijua, au umekaririshwa unayoyaandika hapa?.
Hebu tuone hapa katika mafungu yafuatayo kwamba hiyo roho ni kitu gani.
Katika kitabu cha Ayubu 27:3 tunasoma (Kwa kuwa uhai wangu ukali mzima ndani yangu, Na roho ya Mungu i katika pua yangu;).
Pia umesema roho huwekwa sehemu ya paradiso, hebu fuatana nami katika aya ifuatayo.
Mhubiri 3:21 tunasoma hivi Ni nani ajuaye kama roho ya binadamu huenda juu, na kama roho ya mnyama huenda chini? ama wewe watumia Biblia ipi?.
Pia katika hilo fungu linalohusu Yesu na mwizi msalabani, hebu pitia biblia vizuri kwa kufuata nukta, mkato n.k uione kama inasema ulichoandika.
 
Em' acha ujinga wewe..! sasa wanaokufa maporini kwenye vita na hawazikwi nao wanafufuliwa tokea wapi..??!
Ujinga unao wewe au yeye, hebu kwa mfano soma aya hii ndiyo ujue ni nani mjinga.
Ufunuo 20:13 tunasoma Bahari​ ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake....
 
1. Hapana, hapangi kifo wala siye aliyesababisha watu waanze kufa - ndiyo sababu anaahidi kuwapatia watu uzima wa Mnnmilele.
2. Watu wakifa hawaendi mahali popote panapoitwa peponi bali wanaendi - ndiyo maana kuna siku ya kuwafufua watu toka makaburini
3. Shetani ndiye aliyesababisha watu waanze kufa

AYO NI MASWALI YA KIWAKI.
 
wewe umekufa kwa ngoma Mungu kapanga kivipi?? Mungu tunamsingizia tuu mambo mengine!!

Hakuna uwezo wala nguvu juu yake yeye. Mungu asipotaka jambo litokee halitokei. Yeye ndiye mwenye mamlaka. Angetaka tusife tusingekufa. Kila nafsi itaonja umauti.....hili ni neno lake. Na neno la Mungu halianguki hata siku moja.
Ni mpango tu wa maisha aliouweka kwamba kukutana nae tutakufa kisha kwa uweza wake atatufufua.
Mungu ndiye mwenye mamlaka yote duniani na mbinguni na sayari zote. Asipotaka jambo halifanyiki.
 
mawazo ya mtu sio ujinga kaka kama hayajakuingia ni bora useme hujakubabliana na yeye tu basi lakini sio kumwambia aache ujinga.
Em' acha ujinga wewe..! sasa wanaokufa maporini kwenye vita na hawazikwi nao wanafufuliwa tokea wapi..??!
 
@Molembe Mungu wala hampangii mtu yeyote kifo, kifo nimatokeo ya dhambi aliyoifanya Adamu na Hawa wazazi wetu na hivyotukarithishwa,tunajuaje ikiwa si kifo si mapenzi ya Mungu kaa ujiulize maswaliyafuatayo:
1.kwa nini aksidenti zikitokea watu tunzahuzunika nakulia ilhali ni mapenzi ya Mungu yaani Mungu kapanga watu hao wafe kwaaksidenti?je tunalia kwa maana ya kwamba hatukupenda mapenzi ya Munguyatendeke?

2.mbona mtu akijifungua tunampa hongera na mtu akifiwatunampa pole?je hatukupaswa kupa hongera mtu aliyefiwa pia kwa kuwa mapenzi yaMungu yamentendeka kwake?

3.mbona tukiugua tukiwa kwenye hali mbaya tunazoona zikojuu ya uwezo wetu na zinaweza kutusababishia kifo tunamwomba Mungu ambaye ndiyeanapanga vifo?inawezekana ukamwomba msaada mtu ambaye anapanga mabaya yakupate?utawombajeMungu akuponyehe ili uepuke kifo ilhali yeye amepanga kifo,nadhani kama yeyendiye mpangaji basi hatuna haja ya kumwomba msaada wake.

4.biblia inasema Mungu ni upendo,je inawezekana kuwakweli ana upendo kwetu kama anapanga kifo?inawezekana mtu mwenye upendoakafurahia kuona watu anaowapenda wakiteseka?tuapofiwa tunateseka au tunafurahia?upendowa Mungu uko wapi ikiwa yeye ndiye anapanga kifo kiwapate wanadamu?kifo aduimkubwa wa wanadamu?
 
God planning is an absract idea which cause soo much confrontations among religious scholars!

what i wanna to tell you is that God planing have its scope and limitations!

Is not justice to say every thing happens is God planning!

Hiyo ni General over view!

Kifo ni mpango wa Mungu kwa contest ya kila chenye uhai kitakufa! But how and when huo sio mpango wake ingawa anauwezo wa kufanya hivyo!

God is knower! Perfect knower! He knows past, present and future events!

You ought to distinguish between 'know' and 'plan'
...
I think nimeeleweka hapo na kama kuna swali ulizeni!
Cc: Eiyer, kahtaan!
 
Last edited by a moderator:
Hiyo roho imtokayo binadamu unaijua, au umekaririshwa unayoyaandika hapa?.
Hebu tuone hapa katika mafungu yafuatayo kwamba hiyo roho ni kitu gani.
Katika kitabu cha Ayubu 27:3 tunasoma (Kwa kuwa uhai wangu ukali mzima ndani yangu, Na roho ya Mungu i katika pua yangu;).
Pia umesema roho huwekwa sehemu ya paradiso, hebu fuatana nami katika aya ifuatayo.
Mhubiri 3:21 tunasoma hivi Ni nani ajuaye kama roho ya binadamu huenda juu, na kama roho ya mnyama huenda chini? ama wewe watumia Biblia ipi?.
Pia katika hilo fungu linalohusu Yesu na mwizi msalabani, hebu pitia biblia vizuri kwa kufuata nukta, mkato n.k uione kama inasema ulichoandika.

Sawa mkuu nakushukuru
Lakini fahamu kuwa sikukaririshwa bali ndivyo ilivyo,maneno uliyo nukuru katika Ayubu 27:3 ni mithali (fumbo) ukiangalia mstari wa 1,kwahiyo tunahitaji neema ya roho mt kuelewa hiyo roho (pumzi) ya Mungu puani ni nini.

Ni kweli kwa mujibu wa Mhu 3:21 hakuna ajuaye kama roho ya mtu huenda ama juu ama chini baada ya kufa. Isipokuwa kwa njia ya Yesu pekee TUNAJUA. Kama tunamwamini,tuna hakika kuwa,tujapokufa (ktk tumaini) tu hai pamoja naye. 2Timotheo 2:11.
 
MUNGU kuna miaka kakuwekea ukifa ndani ya hyo miaka ni yeye ila ukifa mtoto sio MUNGU bali ni mungu
 
point no.2 kwamba watu wakifa wanaenda kaburini...je hiyo roho inakwenda wapi??? kwani hiyo roho ikitoka kwenye mwili ndo tunasema mtu kafa na hana budu kuzikwa..je hyo roho inazikwa nayo???huwa najiuliza pia bila majibu ya uhakika.

Mtu anapokufa mwili huzikwa kaburini ambapo kama katika uumbaji mwili uliumbwa kwa mavumbi na mavumbini utarejeshwa. Bali Roho ni pumzi ya uhai iliyotoka kwa Mwenyezi Mungu na Roho hiyo humrudia aliyeitoa...
 
Kufa ni adhabu tuliyopewa baada ya kuasi kwa wazazi wetu pale Edeni ila Yesu akaja kufa kwa ajili yetu na kutuokoa kufa milele, tukifa katika Kristo Yesu ipo siku tutaamka na kwenda kumlaki Mawinguni
 
point no.2 kwamba watu wakifa wanaenda kaburini...je hiyo roho inakwenda wapi??? kwani hiyo roho ikitoka kwenye mwili ndo tunasema mtu kafa na hana budu kuzikwa..je hyo roho inazikwa nayo???huwa najiuliza pia bila majibu ya uhakika.
1. Ni muhimu sana kuelewa roho nini - ukielewa roho ni nini kila kitu kinakuwa wazi
2. Roho ni nini? Ni nguvu ya uhai inayotolewa na Mungu peke yake. Roho ndiyo nguvu inayofanya mtu awe hai.
3. Mtu akifa nguvu ya uhai inamrudia aliyeiweka
4. Fikiria mfano rahisi wa kigari cha kuchezea mtoto kinachotumia betri. Ukitoa betri kigari hakiwaki (kinakufa)
5. Kwa hiyo betri sio mbadala wa kigari au kiwakilishi cha kigari, hapana. Kazi ya betri ni kuhuisha kigari
6. Mwili wa mtu ulitengenezwa tokana na udongo, na ili uwe nafsi hai ilibidi upuliziwe roho (yaani nguvu ya uhai)
7. Kigari bila betri kimekufa, na mwili bila nguvu ya uhai(roho) umekufa
7. Kwa mantiki hiyo huwezi kuitesa nguvu ya uhai, haiwezekani. Bali unaweza kuitesa nafsi hai.
 
Ni kweli tunapozeeka lazima tufe(natural death),lakini vijana na watoto wanaweza kufa.(Ni shetani anayesababisha vifo visivyotarajiwa,sio Mungu,ingawa anaweza ruhusu.

Mkuu hapo kwenye red huoni kuwa unamfanya shetani kuwa na uwezo kuliko Mungu? Kama Mungu ana uwezo kuliko shetani kwa nini aruhusu shetani asababishe vifo?
 
Kama ni kweli kwanini anampangia kifo mtoto mdogo ambae hata hajaanza kutenda dhambi na kuacha wenye dhambi.

Kwenye Bible kuna mstari unasema, "muogopeni yeye anaeweza kuua mwili na roho". Shetani hana mamlaka juu ya roho zetu. The point is, mungu haui wala hampangii mtu kifo, bali mungu ndie alieweka kifo kwa muujibu wa kitabu cha mwanzo, na yeye kuwa ndie aliyeweka kifo haimaanishi kuwa yeye ndie anaeuwa bali ni mwenye mamlaka juu ya kifo.

Ameweka kifo, Haui, Lakini yeye ndie mwenye mamlaka ya kuruhusu roho ya mtu itoke ndio maana tunajifunza kwa Ayubu kuwa mungu alimruhusu shetani amfanye ayubu vile atakavyo lakini roho yake asiiguse, hii inadhihirisha kuwa hakuna mwenye mamlaka juu ya roho za watu(kuzitenganisha na mwili).

Kifo kinakujae? Baada ya mungu kuruhusu kifo ameweka na mechanism inayoweza kupelekea kifo. kwahiyo fact ni hii, Ukipigwa panga na jambazi ukafa, sio mungu amekuua bali ni jambazi ila kifo chako kimefanikiwa kwasababu mungu alisharuhusu watu wafe, na akaweka mechanism zinazoweza kupelekea kifo, ikiwemo na ya kupoteza damu nyingi.
mtoto mchanga akizaliwa, usipomlaza kwenye net ataumwa malaria na atakufa tu, kwa ajili ni kitu ambacho mungu alisha panga.

Mwenyenzimungu hakika yeye ni mwingi wa Hekma,Mwenye nguvu,
basi na atusamehe sisi wakosefu tunaohoji uwezo na mipango yake muumba wetu.
Hakika amesema kamwe mwanadamu hatojua
1.hatojua lini atakufa
2.wapi itafia
3.nini itachuma kesho.

Wewe umekosea.. mbona ata ndepe,kompyuta,na simu vinakufa bila kujulikan lini vitakufa..miti je?
 
1. Hapana, hapangi kifo wala siye aliyesababisha watu waanze kufa - ndiyo sababu anaahidi kuwapatia watu uzima wa nnmilele.
2. Watu wakifa hawaendi mahali popote panapoitwa peponi bali wanaenda kaburini - ndiyo maana kuna siku ya kuwafufua watu toka makaburini
3. Shetani ndiye aliyesababisha watu waanze kufa na kuvuruga makusudi ya Mungu (kwa muda tu) - ndiyo maana Mungu anaahidi kumfutilia mbali shetani na wote wanaomfuata hivi karibuni
4. Kifo cha binadamu si mapenzi ya Mungu - kazi ya Mungu haina makosa, yenye makosa si kazi yake.
Swali jingine.

Point namba 2. Kuna wengine hawazikwi hivyo hawana makaburi. Kuna wanaochomwa na majibu kutupwa baharini, kuna wanaofia majini na kupotea humo, kuna wanaofia nchi kavu mfano porini na kutozikwa. Hivyo si kila anayekufa anazikwa au anakaburi!

Point namba 3. Shetani ni nani? Ananguvu kuliko Mungu? Na kwanini hamfutiii mbali kwa muda wote ambao amekuwapo huku akisababisha vifo kama unavyosema?

Point namba 4. Kama kifo si mapenzi ya Mungu, kwanini aache watu (na wanyama pia) waendelee kufa? Amezidiwa na shetani?
 
Tusifosi maelezo ambayo hayana Logic, shetani haui wala hakuna ushahidi wowote kwamba shetani alisha wahi kutoa roho ya mtu. lakini tunafoundation moja ya kifo kwenye kitabu cha mwanzo baada ya adamu na hawa kufanya dhambi. kwa foundation hiyo mungu ndiye aliyeweka kifo.

Mungu kuweka kifo haimaanishi kuwa yeye ndie anaeua (Muuaji) hapana, lakini yeye ameufanya mwili uwe na uwezo wa kuchakaa mpaka kufa.
 
Back
Top Bottom