Je, kifo ni uzembe,bahati mbaya au mapenzi ya Mungu?

Emmanuel_mtui

Member
Apr 10, 2012
56
13
Samahani wana jamvi kama nitakuwa nimeingiza thread hii mahala ambapo siyo mahala pake, ila leo nilikuwa nimepanda daladala kukatokea mabishano yaliyo nishawisha mimi kwashirikisha ninyi tupate maoni.

Kuna mtu alisema kuna binadamu wanakufa kwa kujitakia, au kupenda wao, akitumia mfano m2 unajua kuna magonjwa na unafanya ngono zembe.

Mwingine akaulioza kwani wote walioathirika wanakufa kabla au baada ya kujua wameathirika,? Mwingine akasema mbona wanakufa kwa ajali na tunasema freemason.

Kwamuda huo nikawa nimefika kituo changu cha kushuka nikaacha mjadala unanaendelea, wadau nini maoni yenu mkizingatia kuwa, kama ni ajali wapo waliopata ajali za kutisha na bado wapo hai, wapo waliougua na kuteseka sana bado wapo, na tulio wafahamu wazima au wenye uwezo walmekufa.

Nawakilisha

Wana JF,

Jana nilikutana na mchungaji mmoja nikamuuliza swali kuwa ajali yoyote duniani inatokea kwa mapenzi ya Mungu au ni laana , hakunipa jibu zuri ila ilionekana naye hajui vizuri kwa kuwa alinijibu ni mapenzi ya Mungu, ni kamuuliza kama ni mapenzi ya Mungu iweje watu wapangiwe kifo cha pamoja, iweje mtoto mdogo ambaye ana hata zambi moja afe?

Mbona sasa waliosababisha wanatiwa nguvuni na kufungwa? Hata vifo vya Albino watu wanatafutia utajiri , kweli albino amepangiwa hivyo?

Tukafika mbali kuwa mbona nchi nyingi tajiri duniani kama Norway, Sweden Uswis watu hawafi kiasi hiki hao Mungu hawapendi? kwa kweli mjadala ulivunjika bila kupata majibu.

Nakaribisha maoni , ya kuridhisha na majibu yenye ukweli. Ila tuzingatie kuwa katika biblia Adam alipewa onyo asile tunda la katikati ya bustanini lenye mvuto sana kwani akila atakufa.
 
Kama ulivyo anza tumekusamehe, tambua sasa kuwa,

KIFO NDIO ZAWADI KUBWA KULIKO ZOTE MUNGU AMEPATA KUMPA KIUMBE HAI YOYOTE.
 
kufa ni sifa ya kiumbe hai chochote . as long as ni kiumbe hai basi ni lazima kife . KAMA NI MAPENZI YA MUNGU KIUM BE GANI AMBACHO MUNGU HAKUPENDA KIFE NA KIKO HAI HADI LEO????
 
Bahati mbaya ni uzembe
Mapenzi ya mungu ni kama wale wanaoenda kulala wakiwa wameagana na jamaa wakiwa wazima, hawakuonesha dalili yoyote ya kuumwa na asubuhi jamaa zake wanamsubiri aamke lakini kimya. Wanagonga mlango kimya, wakiingia ndani jamaa amenyooka kama mtu wa jana au juzi. Chukulia, Mandela kwa umri alionao akiondoka ni mapenzi ya Mungu.(Mandela anapatiwa matibabu lakini kuna siku viungo vitakataa dawa)

Lakin hawa katika hii link https://www.jamiiforums.com/matanga...t322-ddp-kisa-mlevi-kutoka-kilombero-dar.html wangekubali dereva aliyelewa aendeshe na basi kupata ajali na vikatokea vifo basi huo ni uzembe au ndio bahati mbaya yenyewe.....bahati mbaya maana yake uzembe. Au ajali ni uzembe. Ukichunguza ajali yoyote utagundua kuna uzembe ulifanyika.
 
Kama ni kweli kwanini anampangia kifo mtoto mdogo ambae hata hajaanza kutenda dhambi na kuacha wenye dhambi.
 
1. Hapana, hapangi kifo wala siye aliyesababisha watu waanze kufa - ndiyo sababu anaahidi kuwapatia watu uzima wa nnmilele.
2. Watu wakifa hawaendi mahali popote panapoitwa peponi bali wanaenda kaburini - ndiyo maana kuna siku ya kuwafufua watu toka makaburini
3. Shetani ndiye aliyesababisha watu waanze kufa na kuvuruga makusudi ya Mungu (kwa muda tu) - ndiyo maana Mungu anaahidi kumfutilia mbali shetani na wote wanaomfuata hivi karibuni
4. Kifo cha binadamu si mapenzi ya Mungu - kazi ya Mungu haina makosa, yenye makosa si kazi yake.
Swali jingine.
 
point no.2 kwamba watu wakifa wanaenda kaburini...je hiyo roho inakwenda wapi??? kwani hiyo roho ikitoka kwenye mwili ndo tunasema mtu kafa na hana budu kuzikwa..je hyo roho inazikwa nayo???huwa najiuliza pia bila majibu ya uhakika.

1. Hapana, hapangi kifo wala siye aliyesababisha watu waanze kufa - ndiyo sababu anaahidi kuwapatia watu uzima wa nnmilele.
2. Watu wakifa hawaendi mahali popote panapoitwa peponi bali wanaenda kaburini - ndiyo maana kuna siku ya kuwafufua watu toka makaburini
3. Shetani ndiye aliyesababisha watu waanze kufa na kuvuruga makusudi ya Mungu (kwa muda tu) - ndiyo maana Mungu anaahidi kumfutilia mbali shetani na wote wanaomfuata hivi karibuni
4. Kifo cha binadamu si mapenzi ya Mungu - kazi ya Mungu haina makosa, yenye makosa si kazi yake.
Swali jingine.
 
Mwenyenzimungu hakika yeye ni mwingi wa Hekma,Mwenye nguvu,
basi na atusamehe sisi wakosefu tunaohoji uwezo na mipango yake muumba wetu.
Hakika amesema kamwe mwanadamu hatojua
1.hatojua lini atakufa
2.wapi itafia
3.nini itachuma kesho.
 
wewe umekufa kwa ngoma Mungu kapanga kivipi?? Mungu tunamsingizia tuu mambo mengine!!
 
tunachanganya nadhalia mbili hapa kifo, na sababu ya kifo, swala la kufa halina mjadala tareh ikifika mtu hufa, iwe kwa ukimwi malaria kagongwa na gar nk
 
kwanini ukiwa mzee meno yanapukutika wakati ulikuwa na meno kama magurudumu ya trekta???
 
Kama ni kweli kwanini anampangia kifo mtoto mdogo ambae hata hajaanza kutenda dhambi na kuacha wenye dhambi.

Allah says: "He it is who created death and life so He may try you as to which of you is best in deeds." [Sûrah al-Mulk: 2]
 
Kama ni kweli kwanini anampangia kifo mtoto mdogo ambae hata hajaanza kutenda dhambi na kuacha wenye dhambi.

2.jpg
1.jpg
 
Mungu hajawahi kufanya lolote bali binadamu. Hajawahi umba wala kupanga bali binadamu. Kifo kipo kabla ya chochote hakijaandikwa. Walioandika walifanya hivyo kwa kuona hali halisi. Vipi tembo na wanyama wengine walifanya kosa gani hadi nao wafe? TEMBO akiwa na malisho mazuri huishi hadi maika 70 ndio anakufa na kama si meno kuisha na kushindwa kula angeishi zaidi. Sisi tunakufa kwa sababu tumejipangia hivyo. Kama unabisha kula kwa utaratibu mwili utakavyo kama hujaishi miaka mingi pia na kupumzika.
 
1. Hapana, hapangi kifo wala siye aliyesababisha watu waanze kufa - ndiyo sababu anaahidi kuwapatia watu uzima wa nnmilele.
2. Watu wakifa hawaendi mahali popote panapoitwa peponi bali wanaenda kaburini - ndiyo maana kuna siku ya kuwafufua watu toka makaburini
3. Shetani ndiye aliyesababisha watu waanze kufa na kuvuruga makusudi ya Mungu (kwa muda tu) - ndiyo maana Mungu anaahidi kumfutilia mbali shetani na wote wanaomfuata hivi karibuni
4. Kifo cha binadamu si mapenzi ya Mungu - kazi ya Mungu haina makosa, yenye makosa si kazi yake.
Swali jingine.

Nakubaliana nawe hapo namba 1,lakini no. 2. hakika mtu akifa kinachoenda kaburini ni mwili lakini roho huchukuliwa na kuwekwa sehemu ya mangojeo,yaani paradiso (peponi) kwa watakatifu na jehanumu ya mangojeo kwa wenye dhambi.

Yesu akamwambia,Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi. (sio makaburini) Luka 23:43
Zaidi angalia Ufunuo 20:4.

Hapo no. 3 nakubaliana na wewe.

Ni sahihi si mapenzi ya Mungu watu wafe,lakini kwa kadri dhambi zilivyozidi na miaka ya mwanadamu ilipungua hata kufikia 70.(Vinginevyo shetani anahusika kwa vifo visivyotarajiwa).

Asante mkuu
 
Kama ni kweli kwanini anampangia kifo mtoto mdogo ambae hata hajaanza kutenda dhambi na kuacha wenye dhambi.

Ni kweli tunapozeeka lazima tufe(natural death),lakini vijana na watoto wanaweza kufa.(Ni shetani anayesababisha vifo visivyotarajiwa,sio Mungu,ingawa anaweza ruhusu.
 
Kama ni kweli kwanini anampangia kifo mtoto mdogo ambae hata hajaanza kutenda dhambi na kuacha wenye dhambi.

huduma mbovu tu za afya ndiyo zinasababisha watoto kufa, wala sio Mungu...

angalia nchi zilizoendelea, hakuna vifo vya ajabu ajabu, sasa huko tuseme Mungu anawapendelea ama vipi?

Waafrika tuko rough katika field nyingi sana za maisha, ndiyo maana hatuishiwi shida!

Kufa nako kunatengenezwa wakati mwingine.

mtoto anakufa kwa malaria, twasingizia Mungu badala ya kutafuta chanzo na suluhu ya tatizo..
 
Back
Top Bottom