Je kama CCM hawamwelewi mwenyekiti wao, Je Watanzania tutamwelewa?

Quinty

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
462
74
Ndugu wanajamvi wenzangu...yafuatayo ni maneno ya wajumbe wa CCM wakimuongelea mwenyekiti wao ambaye wengi tunamjua kama Raisi wa Tanzania
“Si rahisi kuwa na maamuzi mazito; tatizo la bwana mkubwa haeleweki. Tunashindwa kumsaidia. Tazama kama suala la Dowans, utadhani hakuna serikali, Waziri mzima (Ngeleja) anaitisha press conference anasema walipwe, Mwanasheria Mkuu wa Serikali naye anasema walipwe, Rais kakaa kimya, Kamati Kuu nayo inakaa inasema ni suala la kisheria, halikwepeki, walipwe, badala ya kufanya siasa nao wanashabikia Dowans kulipwa, sasa unajiuliza bwana mkubwa kasimamia wapi katika suala hili, huwezi kujua"
 
Akina nani,lini na wapi? Au fumbo mkuu? Anyway hata mimi simuelewi uyu m/kiti.
 
Rais Kikwete ameamua kuachia demokrasia ichukue mkondo wake. kwa hiyo hayo ndo madhara yake. Well done JK. waache wasemeeeee mpaka wachoke.
 
Ndugu wanajamvi wenzangu...yafuatayo ni maneno ya wajumbe wa CCM wakimuongelea mwenyekiti wao ambaye wengi tunamjua kama Raisi wa Tanzania
"Si rahisi kuwa na maamuzi mazito; tatizo la bwana mkubwa haeleweki. Tunashindwa kumsaidia. Tazama kama suala la Dowans, utadhani hakuna serikali, Waziri mzima (Ngeleja) anaitisha press conference anasema walipwe, Mwanasheria Mkuu wa Serikali naye anasema walipwe, Rais kakaa kimya, Kamati Kuu nayo inakaa inasema ni suala la kisheria, halikwepeki, walipwe, badala ya kufanya siasa nao wanashabikia Dowans kulipwa, sasa unajiuliza bwana mkubwa kasimamia wapi katika suala hili, huwezi kujua"

Sio hao wanaccm wenzie ndio hawamuelewi, inaelekea hata mawaziri wake pia hawayaelewi maagizo yake! Nitatoa mfano mmoja tu kuthibitisha ; Jakaya ameagiza ripoti ya mkaguzi mkuu ipelekwe haraka bungeni na ifanyiwe kazi ikiwa na maana kwamba maagizo ya CAG yatekelezwe haraka kama ilivyopendekezwa, kwa mshangao mkubwa CAG anashauri kwa nia njema ili kuleta ufanisi katika utendaji wa mashirika kuwa wabunge wasiwe kwenye mabodi ya mashirika ya umma lakini kesho yake mawaziri wanafanya kinyume chake!! Hii inaonesha kuwa hawa mawaziri sio tu hawamuelewi boss wao bali wanamdharau!!
 
Back
Top Bottom