Je, huyu ni rafiki mwema kwangu?

Grau

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
4,224
3,845
Habari wana MMU?

Nilikuwa na rafiki yangu tulisoma pamoja chuo, wakati tupo chuo kiukweli hali yake ya maisha hata kipindi tupo chuo ilikuwa ni ngumu sana na mimi ilikuwa niyakawaida tu japo wote tulikuwa na maisha magumu ili nilijitahidi sana kusaidiana nae.

Kutokana na maisha tuliyokuwa nayo mimi nilikuwa natumiwa pesa kutoka kwa ndugu zangu ila yeye ilikuwa ni mara chache sana kupatiwa pesa hivyo ilinigharim kutoa kidogo nilicho nacho ili kumsaidia.

Ilifikia kipindi fulani tukaenda field aisee alikuwa hana kitu na mimi nilitumiwa kiasi fulani nikamchangia, na hivyo ndivyo tulivyo ishi hata kama alikuwa akiugua naenda kumnunulia dawa. Kiukweli nilimhurumia sana.

Tuliishi kwa magumashi mpaka tukamamaliza chuo, hatukuchukua mda tuka tukaajiriwa kwa pamoja serikalini bahati nzur mimi nilipelekwa Halmashauri karibu na kwao na yeye alipelekwa halimashauri karibu na kwetu. Siku moja niliwatembelea wazazi wake ila yeye aligoma kwenda kwetu maana tulikuwa tukiwasiliana kila mara.

Tumeishi kama mwaka na kitu tukiwasiliana inamaana urafiki wetu ulikuwa ni wamawasiliano tu, jamaa ukikwama ukamwambia akukope hela utamrudishia hata kama anayo hakupi.

Kunasiku nilipata msiba mwezi wa 5 mwaka huu ambapo nilifiwa na baba yang mzazi, aisee kipindi hicho nilikuwa sina pesa nilimuomba jamaa anikope pesa niende msibani alininyima aisee na wakati huo alikuwa akiniambia mishe zake kuwa anapesa kadhaa kwenye akaunt yake, na nilivyo enda msibani hakuwa hata akinijulia hali wala kunipa pole, kiukweli niliumia sana kwa mtu kama yule.

Hatimaye nilirudi kazini et ndio kuanza kunipigia akiniambia niambie jembe na mimi kakajisemea moyoni wewe nakutema.

Saiz yupo kwenye blacklist
 
Habari wana MMU?
Nilikuwa na rafiki yangu tulisoma pamoja chuo, wakati tupo chuo kiukweli hali yake ya maisha hata kipindi tupo chuo ilikuwa ni ngum sana na mimi ilikuwa niyakawaida tu japo wote tulikuwa na maisha magum ili nilijitahidi sana kusaidiana nae.
Achana naye.

Usifosi marafiki. Watu wema kwenye maisha huja bila kutumia nguvu.
 
Binadamu bwana, kiuhalisia ilitakiwa aje kwenye msiba na suala la hela hata kabla ya kumwambia alipaswa akutoe ila kama haitoshi ndo umkope.

Now days kumsaidia mtu for my side ni big no.!
 
Hio hali iko kila mahali na ukijaribu kumwelezea mtu hali hio hawezi kukuelewa mpaka aipitie ndio ataelewa ulikua unamaanisha nini, Cha msingi umeshapata fundisho hivyo huwezi kugawa tena msaada wako mahali ambapo hakuna shukrani ni vizuri ikiwa ulipata fundisho, siku atakayokua anahitaji msaada ndio atarudi kwako akijua bado wewe ni yule ambaye ulikua hujajifunza.
 
Tenda wema nenda zako. Pamoja na Yesu kufundisha tutendeane mema, kuponya wagonjwa na mengi mazuri lakini aliishia kuteswa na kisulubiwa msalabani hadi kummaliza uhai wake.

Moja ya changamoto kubwa sana katika maisha yetu hapa duniani ni kuishi kwa upendo wa kweli
 
Binadam ndivyo tulivo mkuu wengine kula vya watu haiwachomi lakini kuliwa vya kwao inakua ni kesi kubwa sana cha msingi mtu kama huyo ukishamsoma Nyimbo zake unatakiwa uishi nae vile yeye anavoishi na wewe ili kama ni msumeno ukate kote kote
 
Mkuu tumia akili hujasoma post yang? Ninacho maanisha sio favor ni msiba ulio nipata halafu bdo hakujali hvyo tu. Ingekuwa ni hvyo basi ningemfungulia uzi mapemaa.
Nasema tena wewe ni kiazi, una msaidia mtu kwa 'kuwekeza' ukipata shida asipokusaidia unalialia, huo ni utopolo

Stori ya yako ina pande mbili, 1. ulimsaidia kwanza 2. ukategemea akusaidie baadae
 
Huyo ungeendelea tu kuwasiliana nae ili siku nae akiwa na shida unampotezea baada ya siku kadhaa unamjulia hali kama yeye alivyokufanyia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom