Je hili ni sahihi?

kanyampaog

Member
Apr 25, 2011
11
2
Naomba kuuliza wajameni, mtoto wa kike ukiwa na mahusiano na mtu unampenda kwa moyo wako wote, ukamficha baadhi ya mali zako ni sahihi kuwa unampenda au unajidanganya tu na nafsi yako? Mali hizo ni kama vile kuwa na kiwanja then unaficha wakati ye kakuweka wazi vyakwake. Na je kumuweka wazi kabla ya ndoa na mkaamua hata kujenga kwa pamoja ni inashauriwa?
 
kwakweli suala kama hilo huwezi kumsemea mtu sababu kila binadamu ana tabia yake,mie binafsi kwanza ntamuangalia kwa mda kama mkweli na tumeowana kwanini nisimwambie,lakini mchumba siwezi mwambia mali zangu,kwani sina uhakika na yeye.mume afadhali unaweza ukampa nafasi kidogo yakumuamini.
 
Kila siku viongozi wadini wanakemea ufusika uliobatizwa kwa majina ya boyfriend@buzi na girlfriend@wakupozea, inakuwaje tena miss kelly unakuja na hoja za wewe kufichwa mali na boyfriend wako?kwani mali ya mwisho ulisikiliza mahubiri lini?Amini kama unafichwa mali na huyo buzi lako jua ni dalili kuwa Mungu bado anakupenda.Murudie Muumba wako atakupa mume atakayekupenda na kukuweka wazi kwa kila jambo hata uhai wake.
 
Unauliza na huku tena majibu unayo..umeshasema unampenda kwa moyo wako wote then unamficha! mimi nafikiri wapenzi hukaa na kushauriana kwa kila kitu! may b kama hauna future nae
 
jamaa mwenyewe kama unamtilia shaka malengo yake......................................hakuna shida kujihami kabla ya tufani kukuangukia....................kumbuka penzi ni suala la wakati......................
 
Inategemea na uhusiano ulipofikia! Je ninyi wachumba ( i mean mnatambulika kwa pande zote 2) au mnatunguana tu kiaina na hamna malengo mahsusi na muelekeo wenu . Kama ni wachumba si vibaya kushirikishana kila kitu...ila isiwe mwanzoni sana kwani hiki pekee kinaweza kuwa kichocheo pekee cha huyo mwenzi wako kukupenda na ni hatari upendo ukijengwa kwenye mali.
 
Shida siku hizi wanawake tunaingia kwenye ndoa kwa ajili ya kujaribisha, na sio kama ndio tumeolewa (for life). Ndio maaana inakuja swala la kuficha mali na hata KUKATAA KUBADILISHA MAJINA YA WAZAZI WETU!

Shoga ukiwa hivyo,. litakusumbua sana. Ukiamua kuolewa na sio kwenda kujaribisha, kuwa muwazi!
 
Back
Top Bottom