Je, hali ya maisha ya Tanzania kwa sasa haitoi nafasi kwa mtu kuanzia chini hadi kuwa billionea?

Quartz360

Senior Member
Mar 27, 2023
124
302
Habarini wanajukwaa.

Kwa namna hali ilivyo katika nchi yetu imekua ni changamoto Sana kwa mtu kuanza "from Zero to Hero" Jambo linalofanya watu wengi wanao hustle kuamini kuwa mazingira si rafiki kwa wao kufanikiwa yaani kuwa self-made Billionaires ukiwatoa wale talented people ambao kwao imekua sio changamoto kubwa kutokana na uwepo wa vipaji vyao"

Mtazamo wangu.
 
Hivi kipindi kile cha phase 01 na phase 02 (wakuu wa kaya) kipindi hakuna teknolojia, wataalam walikuwa ni wa kuhesabu, elimu haba, usafiri mtihani na mambo kibao yalikuwa magumu na bado hovyo mbona wapo walio-rise na mpaka sasa wana legacy kubwa tu ingawa wao baadhi hawapo hai tena?! Mfano Marehemu Mzee Mengi, kina mzee Khimji n.k

ACHA KULAUMU!, FANYA KAZI KWA BIDII! ZIFUATE FURSA ZILIPO!, GUNDUA FURSA MPYA MAHALI ULIPO!, NIDHAMU YA KIDOGO ULICHONACHO HATA KIKUBWA!, ENDELEA KUJIFUNZA SIKU ZOTE!

Pia kumbuka msemo ule wa "Choosen from god!"

Vijana wa sasa kazi ni kulaumu sirikali tu 😔
 
Vijana wa sasa kazi ni kulaumu sirikali tu
Umenena vyema mkuu,,, Lakini kwenye suala la Elimu,,, Kipindi kile Elimu ilikua haba, Lakini kuna watu waliweza kutoboa, nashanga nowadays Elimu imekuwa accessible kwa urahisi, Lakini hali ndo inazidi kuwa mbaya,,, Pengine labda na mfumo wetu wa Elimu hauwaandai vyema vijana wa taifa hili.
 
Kuanzia chini ya level ipi mkuu? Au kwamba mtu akiwa na mtaji wa kiasi gani cha pesa ndyo anaweza kuwa billionea?
 
Kuanzia chini ya level ipi mkuu? Au kwamba mtu akiwa na mtaji wa kiasi gani cha pesa ndyo anaweza kuwa billionea?
Nilimaanisha kuwa mtu anaanza from the Scratch,, kwa mfano kutoka kwenye hali duni kabisa ya maisha.
 
NI NGUMU kwa sasa...mambo mengi yamebadilika pia,changamoto lukuki na by now gharama za maisha zimepanda!!kwa ufupi ni kama tu hamna mtu anaeweza kuanza zero to hero unless kwa wale wenzetu wanaotengenezewa mazngira
 
Umenena vyema mkuu,,, Lakini kwenye suala la Elimu,,, Kipindi kile Elimu ilikua haba, Lakini kuna watu waliweza kutoboa, nashanga nowadays Elimu imekuwa accessible kwa urahisi, Lakini hali ndo inazidi kuwa mbaya,,, Pengine labda na mfumo wetu wa Elimu hauwaandai vyema vijana wa taifa hili.
Na matoto yetu yenyewe hayataki kusoma. Yanataka kwenda kushinda kariakoo kuuza simu... wenyewe wanaita mazoezi 😅

Mtu akipata divisheni ziro saiv anasifiwa na kuambiwa atakuja kuwa mfanya biashara mkubwa na kuajiri wenye divisheni wani ambao wataenda mpaka vyuo na kuwa majobless waje warudi kitaa wasote wakute wenzao washanyookewa. Ni hadithi nzuri, tamu na rahisi yenye kufikirika na kukuhadaa kiurahisi ukaamini maneno hayo ila tathmini hawa watoto wanakwenda wapi!

Kipindi kile elimu ilikuwa haba sawa ila wapo waliozembea kwa kigezo hicho. Wenzao wakakomaa leo hii wanakula keki ya taifa.
 
Kufikia hizo level ni ngumu kwa kuplay fair, waliofika huko hawawezi kukwambia hilo.

“Kwenye kitabu cha mafanikio kuna page huwa hazisomwi”

Rough ni nyingi, “michezo” ya mjini haikwepeki, lazima ujue kula na wajanja.
 
Back
Top Bottom