Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 316
- 523
Baraza la Sanaa la Taifa BASATA badala ya kuwapa elimu sahihi Wasanii kama Sheria inavyo wataka, wao wanawadanganya na kuwapoteza eti NEMC inazima Muziki.
NEMC haizimi Muziki, imeweka viwango ambavyo havitaleta kero kwa jirani asiyetaka Kelele.
Mfano mtu anaweka baa katikati ya makazi ya watu halafu anataka apige muziki usiku kucha tena kwa sauti ya juu
Maana yake watoto waliozunguka eneo hilo hawawezi kujisomea, wazee, wajawazito na wagonjwa hawawezi kupumzika matokeo yake pressure zinaongezeka, vifo, kuzaa watoto njiti, viziwi wanaongezeka
Lakini watu wanakosa amani na utulivu wa falagha wawapo majumbani mwao.
NEMC hauzii muziki ndo maana baa zilizofuata masharti zimefunguliwa na zinaendelea.
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
Katika kudhibiti changamoto ya kelele na mitetemo, BASATA imetakiwa na Sheria kufanya yafuatayo;
1. Kusimamia vibali vya matukio ya sanaa na burudani vinatumika kulingana na masharti ya vibali husika.
2. Kutoa elimu juu ya athari zitokanazo na kelele na mitetemo.
3. Kushiriki katika vikao vya kufanya tathmini na kutoa maamuzi juu ya uthibiti wa kelele na mitetemo katika jamii.
Lakini leo BASATA hiyo hiyo inaungana na watu wasio na uelewa kuhusu udhibiti wa kelele na kuruhusu nyimbo zinazowaondolea Weledi katika utendaji wao wa kazi.
Watu wenye vyanzo vya kelele hawawezi kuachwa tu wafanye watakavyo kinyume na Sheria iliyopo.
Kelele ni sauti zilizozidi viwango zinazosababisha madhara kwa afya ya binadamu, wanyama na mazingira.
Uchafuzi huu unatokana na kelele zisizo dhibitiwa pale zinapozalishwa na kusababisha athari za kiafya kwa jamii.
Changamoto ya kelele inachangiwa zaidi na kukua kwa shughuli za kiuchumi na kijamii ikiwemo matumizi mabaya ya teknolojia.
Kwa siku za hivi karibuni, kelele zimeongezeka kwenye maeneo ya makazi na hivyo kusababisha matatizo ya kiafya kwa jamii ikiwemo kupoteza uwezo wa kusikia, matatizo ya uzazi, kupunguza umakini katika mafunzo, ajali na uwezo wa kawaida wa kusikilizana.
Vyanzo vikuu vya kero ya kelele ni pamoja na kumbi za starehe ikiwemo biashara za vileo (baa), vyombo vya usafiri na usafirishaji (magari, ndege, treni nk.), matumizi ya teknolojia zilizopitwa na wakati kwenye viwanda vikubwa na vidogo (Karakana za kuchomelea, ufyatuaji matofali, mashine za kusaga na kukoboa nafaka), majenereta, matangazo ya biashara kwenye makazi, shughuli za ujenzi, nyumba za ibada n.k.
Hivyo katika kukabiliana na changamoto ya kelele ni muhimu kuimarisha jitihada za pamoja na ushirikiano miongoni mwa Taasisi za Serikali na wadau ili kusimamia viwango vya kelele na mitetemo vilivyowekwa kwa mujibu wa Sheria.
Kila Mtanzania ana wajibu wa kuhakikisha kelele zinapungua mtaani ili watu wasikilizane na Walale kwa amani, sio swala na NEMC peke yake
Ukiachilia mbali BASATA na NEMC, taasisi nyingine zinazotakiwa ziwe mstali wa mbele kudhibiti kelele ni pamoja na TBS, Ofisi ya Makamu wa Rais, OR-TAMISEMI, Mamlaka ya Afya na Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA) nk.