Jaribio la kijeshi kumuondoa Rais wa Burundi madarakani

Niliwaza hili tangu juzi kuwa akija Tanzania hakuna figisu figisu zitatokea??!! Japo najua maraisi wengi Africa huchagua wakuu wa majeshi vibaraka wao!!!

Lakini pia huenda hii ni janja ya Nkurunziza kuondoka madarakani baada ya kupata aibu huku wapinzani washindwe kutwaa dola kwa njia ya kura huku jeshi likiwa na watu wake!!

Bado mapema kulijua hili. Muda ndio jibu.
 
Jambo la kujiuliza atarudi kwao au atakuwa mkimbizi ktk nchi ya tz??

Ninashauri apelekwe kule nyarugusu kwenye kambi ya wakimbizi akajionee,

Pia inaonekana hakuwa na mahusiano mazur na jeshi maana jamaa ameweza ku co-ordinate kirahic sana..

African continent has lots of wonderful,
 
Jeshi limechukua nchi
 

Attachments

  • 1431524678917.jpg
    1431524678917.jpg
    16.5 KB · Views: 351
Kama ni kweli kuwa Rais Nkurunzinza amepinduliwa huko Burundi, ni dhahiri shahiri kuwa sasa ngoma imegeuka na imemkalia yeye. Mara ya kwanza alipoitwa na marais wenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kulijadili hilo swala, yeye ndiye aliyekuwa akibembelezwa kuwa abadili msimamo wake ili nchi iwe na amani. Hata kabla ya kubembelezwa, maafisa wa serikali yake walishatoa matamko kuwa EAC haiwezi kuingilia maswala ya ndani ya wanachama wake. Lakini sasa vipi? Ngoma imeshageuka. Yeye sasa ndiye atakayewabembeleza wenzake wa EAC ili wamsaidie kutuliza upepo ili angalau arejee madarakani amalizie kamwezi kamoja kalikosalia. Mwanzoni alikuwa mbembelezwa, sasa yeye ndiye mbembeleza! Mkataa pema, pabaya panamngoja!
 
kama ivo safi sana haiwezekani mtu mmoja kusababisha watu maelfu kuhangaika na kufa ang'oke tu na tunaomba iwe hivyo hivyo
 
Mpya kutoka bujumbura

habari zaidi kutoka burundi zinasema waliopindua nao wamepinduliwa na wanajeshi watiifu kwa nkurunzinza

na jengo la ikulu,na lile la shirika la utangazaji vimezingirwa na wanajeshi watiifu kwa rais!

Jenerali aliyetangaza mapinduzi inasemekana amekimbia kwa helkopta kuelekea maeneo ya mpakani mwa kongo na burundi!
 
Viongozi wa Afrika wamezidi kupenda madaraka, wananchi wa Burundi walijua fika wakisubiri sanduku la kura Nkurunzinza atapita tu kwa hila! Nawapongeza wanajeshi wa Burundi ilimradi nao wasiwe kama waliyempindua.
 
Mpya kutoka bujumbura

habari zaidi kutoka burundi zinasema waliopindua nao wamepinduliwa na wanajeshi watiifu kwa nkurunzinza

na jengo la ikulu,na lile la shirika la utangazaji vimezingirwa na wanajeshi watiifu kwa rais!

Jenerali aliyetangaza mapinduzi inasemekana amekimbia kwa helkopta kuelekea maeneo ya mpakani mwa kongo na burundi!
 
Sisi watu weusi tunatia aibu sana, ulafi, uchoyo na ubonafsi. Haya majamaa pia nimajinga na mashenzi.

1. Yowel Kaguta Museven - Uganda

2. Paul Kagame - Rwanda

3. Joseph Kabila - DRC Kongo

4. Ally Bashil- Sudan

5. Robert Mugabe - Zimbabwe


What does this have anything to do with Burundi? Unajua Lee Kuan Yew wa Singapore alikaa madarakani kwa miaka mingapi? Fidel Castro? Putin? Hao ni watu weusi???
 
Tanzania should send this dude back to Burundi akaface music ya kudharau democracy
 
Back
Top Bottom