Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!

Hata smartphone sio sawa na kiswaswandu, lakini kwa kutumia Smartphone mtu hawezi kufanyia uhalifu??!!--- pick up your senses, DP world ametapakaa sehemu nyingi duniani katika shughuli za bandari lakini yeye ndiye anayeongoza kuwa na kesi nyingi kuhusiana ni migogoro ya mikataba.
Una ushahidi gani kama hizo habari za kesi ni za kweli?. Huko whatsapp wamejaa kila aina ya watu kuanzia matapeli mpaka watakatifu.
 
Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" kuhusu jambo lolote lenye maslahi makubwa kwa taifa letu liwe ni la kisiasa, kiuchumi au kijamii.

Mada ya leo ni kuhusu Bunge letu tukufu, limeridhia makubaliano ya IGA kati ya Serikali ya UAE na Tanzania, kampuni ya DP World ya Mwarabu wa Dubai, kutuendeshea Bandari zetu.

Angalizo la Uzalendo
Unapohoji baadhi ya mambo makubwa kama haya, na kufuatia kuna baadhi ya watu wameupinga mpango huu, hivyo unawekwa kwenye kundi la wapinzani, mimi sio mpinzani wa mpango huu, na bandiko hili limetanguliwa na mabandiko yangu matatu kuusuport mpango huu
1- Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe!. Je DPW Tunapigwa?.

2- Wabunge Wetu, Macho ya Watanzania Wote Leo ni Kwenu!. Maslahi ya Taifa Mbele!. Tuwaogope Kama Ukoma Muflis Hawa!, Kama Huwezi, ni Lazima Usaidiwe Tuu!

3- Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie? hivyo nawaomba sana wasomaji wangu, msiwe na wasiwasi kabisa kuhusu uzalendo wangu kwa nchi yangu!.

Kuna watu wana support hatua hiyo kwa hoja za msingi, kuwa DP World ni kampuni kubwa na ina uwezo mkubwa, inaendesha Bandari nyingi duniani, hivyo itatusaidia sana kuboresha uendeshaji wa Bandari yetu ya Dar es Salaam. Na kuna wanaopinga wakiwaita DP World ni matapeli, kufuatia kesi na migogoro mingi mahali pengi ambapo DP World wana operates, hivyo kitendo cha Bunge letu kuridhia hiyo IGA ya DP World bila kuifanyia a due diligence report, kumewafanya wachoke na kudhani, it's over, it's the end of the road kwa suala hili,. naomba kuwapa faraja na kuwatia moyo kuwa it's not the end!, it's not over yet until it's over!.

Hiyo HGA ni makubaliano tuu na sio mkataba, yaani ni an agreement na sio contract. Kila mkataba ni agreement, lakini sio kila agreement ni mkataba, mfano mzuri ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuunda Tanzania, ni makubaliano tuu na sio mkataba, mkifika mahali mkashindwa kuelewana, mnagawana tuu fito, kila mtu anasepa kivyake Je, Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?!.

Hivyo kile Bunge letu lilichoridhia, ni agreement tuu, tukiithibitishia serikali yetu, hawa DP World, pamoja na uzuri wao wote, pamoja na uwezo wao mkubwa wa kuendesha Bandari kibao, lakini ni matapeli na wana matatizo lukuki, hivyo serikali yetu iwe makini sana kabla ya kusaini HGA, na utepeli wao, ukiwekwa wazi hadharani peupe, kila mwenye macho aone, tutaisaidia sana serikali yetu, tutamsaidia sana Rais wetu Samia na kulisaidia taifa letu Tanzania tusiingizwe tena mkenge na Mwarabu wa Dubai kama alivyofanywa Chief Mangungo, hivyo serikali yetu, viongozi wetu na Bunge letu kuridhia fasta fasta kwasababu tuu, Mwarabu wa Dubai ni mtu Rahim, mkarimu, amemkirimu Mama yetu kuipaisha bure Tanzania kwenye Expo Dubai, akawakirimu waserikali wetu, kwa trips za Dubai, akawakirimu waheshimiwa wabunge wetu kwa trips za Dubai, na kuwakirimu waandishi wetu wa habari na media zetu kwa trips za Dubai.

Japo Rais wetu, Mama Samia, ana nia njema ya kweli na ya dhati kulisaidia taifa letu, lakini anapokutana na matapeli wa kimataifa wakamuingiza mkenge, sisi watu wa Mhimili wa Nne, the media, tuna wajibu wa kulisaidia taifa letu kwa kuonyesha utepeli huo uko wapi, kisha serikali yetu ikiamua kuendelea na HGA ya Mwarabu wa Dubai, sisi watu wa media, tutakuwa na a clear conscious kuwa angalau tumetimiza wajibu wetu, tumeieleza serikali yetu inavyotaka kuingizwa mkenge na kutapeliwa, hivyo vipengele vya mkataba wa HGA viboreshwe na kazi, iendelee!.

Kwa vile mimi licha ya kuwa ni mwandishi tuu wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, mimi pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, kwa kujitolea kutetea bure haki kwa wasio na uwezo, hivyo nitawaletea makubaliano hayo na kuwachambulia kuwaonyesha jinsi tunavyotaka kutapeliwa mchana kweupe.

  1. Utapeli wa kwanza mkubwa, ni hakuna mtu yoyote kati yetu aliyefanya a due diligence report ya DP World, tunaelezwa ni Governmental Organisation, wakati sii kweli, it's a private company!. Kabla ya kuingia mkataba wowote, lazima kwanza kufanyike kitu kinachoitwa a due diligence process na kutolewa a due diligence report. Hili halikufanyika hivyo serikali yetu kujikuta inaingia mkataba wa kimataifa na parties to contract which has no capacity to contract hivyo ku vitiate makubaliano kugeuka void hivyo makubaliano hayo yanakuwa null and void ab initio!.
  2. Mkataba wa IGA na HGA inaingiwa kati ya serikali na serikali, hivyo ukisoma documents za makubaliano utaona ni kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya UAE, lakini signatories kwa serikali ya Tanzania ni serikali kweli, lakini kwa serikali ya UAE, signatories ni Mwarabu wa Dubai wa DP World na sio serikali ya UAE, kwenye mkataba wameandika serikali ya Dubai, Dubai hivyo hapa tunatapeliwa!, serikali yetu inaingizwa mkenge kuingia mkataba na a private company disguised as a government of UAE kumbe ni kampuni binafsi!.View attachment 2653406
  3. Mkataba Kati ya serikali ya Tanzania na Dubai ni batili kwenye sheria za kimataifa. Maana Dubai sio nchi, a sovereign state kama ilivyo Tanzania, Dubai hapa inajitambulisha kama a State Party, Dubai is not a state hivyo haiwezi kuwa a state party, it has no the capacity to transact as an international IGA, haiwezi kuingia mikataba ya kimataifa na nchi, inaweza kuingia mkataba wa kimataifa na mamlaka ya Bandari, taasisi kwa taasisi, kama ilivyofanya hapa View attachment 2653409ambapo DP World iliingia mkataba na Mamlaka ya Bandari TPA, mkataba ambao Rais Samia aliushuhudia ukisainiwa kule Dubai during Expo Dubai.
  4. Sasa kampuni hii ya DP World iliyoingia mkataba na mamlaka ya Bandari, sasa inajigeuza nchi, sovereign state of Dubai, imeingia mkataba wa kimataifa na serikali yetu!, huku ni kututapeli!. Dubai is not a state, it's not a nation na nchi isiyo na sovereignty!. DP World is not a state, it's a private company, hapa imejigeuza ni nchi!. Huu ni utapeli!. View attachment 2653458
  5. Mikataba ya kimataifa inaingiwa kati ya nchi na nchi, na Falme ya Kiarabu inayotambulika kwenye sheria za kimataifa na sio Dubai ambayo ni sehemu ya UAE, hivyo hapa kuna utapeli!. Due diligence ingefanyika, hili lingeonekana.
  6. Status ya Dubai kwe UAE ni sawa na status ya Zanzibar ndani ya JMT, Zanzibar has no capacity to transact an international treaty kwasababu Zanzibar sio sovereign. Dubai pia sio sovereign, hivyo mikataba yote ya kimataifa ya Zanzibar, inaingiwa na JMT kwaniaba ya Zanzibar, IGA na HGA inapaswa kuingiwa kati ya Tanzania na UAE na sio Tanzania na Dubai!.
  7. DPW ni kampuni kama inavyoonyesha hapaView attachment 2653462
  8. Wanasheria wanapoamua kufanya magumashi ya kisheria, wanakuzuga kwa maneno ya kweli kwenye mkataba, mfano hapa Dubai inatambulishwa kama nchi,View attachment 2653466lakini mkataba wetu hii iliyoandikwa kama nchi, sio nchi kweli bali ni kampuni ya DPW!.
  9. Kwa vile kwa upande wetu ni serikali yetu, ili kuonyesha IGA ni kati ya serikali mbili, hapa wameitaja kampuni ya kiserikali ili kuiserikalisha kampuni binafsi ya DPW kuwa ni serikali View attachment 2653471
  10. Hivyo mikataba ya HGA utaokuja kuingiwa na serikali yetu, sio mkataba wa kimataifa wa kiserikali kati ya serikali yetu na serikali ya UAE, lakini hakuna chochote cha UAE bali kampuni binafsi ya DPW iliyoserikalishwa na kujifanya ni serikali!.View attachment 2653477View attachment 2653481
  11. Kwa vile mikataba ya kimataifa inahusisha state parties, HGA inayokwenda kuingiwa ni HGA kati ya nchi ya Tanzania ambayo ni state na kuingia na DPW iliyo ji stetisha kama a state ambapo huu pia ni utapeli!.View attachment 2653488
  12. Kwa Tanzania mamlaka yote ya nchi, mtu yoyote ili asaini mkataba wa kimataifa wa kuiingiza nchi, anapaswa apewe the Power of Attorney na Rais wa JMT. Hii hapa chini ni POA ya Rais Samia kumpa mamlaka Prof. Mbarawa kuingia huo mkataba kwa niaba ya Tanzania, View attachment 2653454POA hii kisheria ni defective, kwasababu japo imesainiwa na Rais Samia, lakini haina muhuri wa rais, au muhuri wa serikali, hizi documents za kisheria ikisemwa POA must be signed and stamped by the official seal, lazima iwe hivyo, not otherwise!, kama walivyofanya hawa counter parts hapa chini.View attachment 2653455
  13. Ili serikali yetu iingie kwenye mkataba wa kihalali wa kimataifa na taasisi ambayo sio nchi, kulitakiwa kuwepo POA toka UAE kuipa mamlaka Dubai kuingia mkataba wa kimataifa kwa niaba ya UAE, then ndipo Emirate wa Dubai angeweza kuwapa POA DPW kujigeuza ni nchi.
  14. Hapa Prof. Mbarawa almanusura angekosea kusaini View attachment 2653452
  15. Hakuna ubaya wowote kwa kampuni yoyote kuingia mkataba na serikali under PPP, lakini hili la kampuni binafsi iliyo serikalishwa kuingia an International treaty na serikali yetu, halikakaa vizuri.
  16. Jambo jingine, kuna kipengele cha kuizuia nchi isiendeleze Bandari nyingine, hivyo kuiweka mashakani Bandari ya Bagamoyo, hili halikubaliki hata kidogo!.
Hitimisho
Kwa vile Rais Samia ana nia njema ya dhati kuisaidia nchi yetu, wasaidizi wa rais na sisi Watanzania wengine wote tuna wajibu wa kumsaidia rais wetu na kulisaidia taifa letu na huu ndio uzalendo wa kweli.

Paskali.
Tukiachana na ujinga, umaskini na maradhi adui mwingine mpya kwa watanzania ni vyombo vya habari vyenye jukumu la kuripoti matukio tu.
 
Nasubiri ufafanuzi wako wa Ibara zenye utata, ikizingatiwa kuwa IGA ndio utakuwa Mkataba mama (referal agreement) wakati wa kuandaa HGAs.

Je, wewe umefanikiwa kuona na kusoma MoU kati ya TPA na DP World, kwa maana "boss" wa TPA ameitetea sana DPW?
Nmetoka kumsikiliza lipumba akisoma vipengele muda si mrefu jambo tv, nimesikitika sana kwa kweli. Kuna sehemu unasema ukishaanza kutekelezwa hata ikifika kipindi cha renew serikali haina uwezo wa kukataa renew bila kibali cha UAE. Yani hiyo MoU ni ome sided inaomgelea majukumu ya TZ kwa DP world haiongelei majukumu ya DP world kwa TZ. Mkuu ukipata muda kaisikilize maana anao anasa vipmegele tatanishi. Pascal Mayalla
 
Mkuu leo nimeelewa na kusoma topic yako kwa umakini mkubwa sana

Swali langu najiuliza je Professor Palamagamba Kabudi si tuliambiwa kazi yake ni kumshauri mama yetu Samia kwenye kitengo cha mikataba ya kimataifa hakuyaona madhaifu haya au mkataba uliingia nchini ukiwa tayari una signature?

Au yupo ikulu tuu kusukuma Siku ziende ilhali uliyoyaongea naona kama yana Fact kwenye ubongo wangu!

Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Africa
 
Na cha kushangaza zaidi, mama Samia wakati anamtoa kwenye uwaziri, Prof. Kabudi alisema atakuwa ndio baba wa mikataba,sasa Jana kwenye hoja hii hakusikika kusema chochote na kama alihusika,angalau angetetea lakini hakusema chochote,labda hakushirikishwa.
Wabunge wetu wao wanadhani watanzania wanapinga uwekezaji,No, kinacholalamikiwa ni vipengele vya mkataba vyenye utata na viko wazi, lakini wawakilishi wetu hawavioni,wanaishia kutoa matamko ya kutishia wanaokosoa mkataba.
 
Hapa kwa ufupi niseme kwamba, bunge limetumika kuhalalisha uhuni uliofanywa na serikali, nalo kwa kutokujitambua, likabariki uhuni huo, hivyo hapo ni kama serikali inafurahi imempata mjinga mwingine wa kufa nae, huku Spika Tulia akiwa ndie kiongozi wa hao wajinga.

Nachotaka hayo makubaliano/mkataba yavunjwe, naona kabisa kuna vitu vingi ambavyo havina haki kwetu ajabu tumeweka saini kwenye yale makubaliano, na inapoonekana Mbarawa mzanzibari, na Samia mzanzibari wote wamehusika, ndio inaumiza moyo zaidi, hawa wawili wana nia mbaya na wabara, ukweli usemwe tu.
Hilo Bunge la Magufuli ni hasara na mzigo kwa Taifa.

Ndio maana tunahitaji Katiba Mpya Leo kuliko juzi na jana.

Kukomesha ufisadi na kuondokana na huu utamaduni wa kifasadi ulioota mizizi zaidi ya miaka 40 sasa nchini, we need to RESET.
Mkataba unafanana na mingine, mfano wa Loliondo na Ile ya madini. Ni Lazima sasa tutoke hapa tulipokwama na kukwamishwa.
 
  1. Ili serikali yetu iingie kwenye mkataba wa kihalali wa kimataifa na taasisi ambayo sio nchi, kulitakiwa kuwepo POA toka UAE kuipa mamlaka Dubai kuingia mkataba wa kimataifa kwa niaba ya UAE, then ndipo Emirate wa Dubai angeweza kuwapa POA DPW kujigeuza ni nchi.
  2. Hapa Prof. Mbarawa almanusura
Conclusively ni kwamba tumepigwa na Wabunge wa CCM
 
Na cha kushangaza zaidi, mama Samia wakati anamtoa kwenye uwaziri, Prof. Kabudi alisema atakuwa ndio baba wa mikataba,sasa Jana kwenye hoja hii hakusikika kusema chochote na kama alihusika,angalau angetetea lakini hakusema chochote,labda hakushirikishwa.
Wabunge wetu wao wanadhani watanzania wanapinga uwekezaji,No, kinacholalamikiwa ni vipengele vya mkataba vyenye utata na viko wazi, lakini wawakilishi wetu hawavioni,wanaishia kutoa matamko ya kutishia wanaokosoa mkataba.
Mimi sio mwanasiasa na kwanza siasa siipendi nilichokiona ilikuwa ni mipasho law wapinzani rejea mchango wa mbunge waitara,na press ya kibajaji
Nilidhani wangekuja na vipengele vp vitatuumiza na vipi tuvitoe wao wanaongea kama wapo najukwaani nilijikuta nawashangaa sana maana watakuja kuulizwa hata wao siku moja mkataba ulikuwa unasema nn utashangaa na wao hawajui
 
Conclusively ni kwamba tumepigwa na Wabunge wa CCM
Uliwahi kutegemea wafanye tofauti?

Wamefanya "walichoteuliwa" kukifanya na hayati Magufuli, na pia wamekamilisha kazi "waliyotumwa" na CCM. Wako pale kwa maslahi na malengo ya hao waliowaweka hapo.

Iko hivyo na itabaki hivyo Hadi pale tutakapobadilisha hilo - Katiba Mpya!
 
Mimi nilidhani pamoja na kuwa nchi Ina mfumo na vyombo vya kusaidia ulinzi maendeleo na kulinda maslahi yake, idara ya Usalama wa Taifa ingekuwa ndio chombo makini na nyeti kwa yote.

Hili jambo la bandari, idara inahusikaje hapo? Haina taarifa za kujibu mashaka? Haina stadi za kuchambua, kupima na kuainisha faida na madhara kwa miaka mingi ijayo?

Mbona hata waziri mwenye dhamana inaonekana kama kastukizwa kwa baadhi ya hoja?

Haipendezi jambo kubwa kama hili kupitishwa kwasababu mkuu kaona ni jema. Lipitishwe kwa sababu hoja zote za msingi kiusalama, kibiashara, kiuchumi na maslahi vyote vipo sawa.

Kama idara ya Usalama huwa inaingizwa kazini baada ya wakubwa kusaini, nahisi siyo salama. Au kama hiyo idara haikuwa na ijuacho kuhusu huyo mwekezaji kiasi cha kushindwa kupenyeza taarifa kwa wakuu, mantiki inaniongoza kuamini Kuna tatizo.

Hili ni funzo, Kuna rekebishika. Leo tumeanza na bandari. Mambo ya ufanisi kwetu ni kitendawili. Huenda mbele tutahitaji pia wawekezaji kwa kila kitu.

Mungu ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
 
Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" kuhusu jambo lolote lenye maslahi makubwa kwa taifa letu liwe ni la kisiasa, kiuchumi au kijamii.

Mada ya leo ni kuhusu Bunge letu tukufu, limeridhia makubaliano ya IGA kati ya Serikali ya UAE na Tanzania, kampuni ya DP World ya Mwarabu wa Dubai, kutuendeshea Bandari zetu.

Angalizo la Uzalendo
Unapohoji baadhi ya mambo makubwa kama haya, na kufuatia kuna baadhi ya watu wameupinga mpango huu, hivyo unawekwa kwenye kundi la wapinzani, mimi sio mpinzani wa mpango huu, na bandiko hili limetanguliwa na mabandiko yangu matatu kuusuport mpango huu
1- Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe!. Je DPW Tunapigwa?.

2- Wabunge Wetu, Macho ya Watanzania Wote Leo ni Kwenu!. Maslahi ya Taifa Mbele!. Tuwaogope Kama Ukoma Muflis Hawa!, Kama Huwezi, ni Lazima Usaidiwe Tuu!

3- Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie? hivyo nawaomba sana wasomaji wangu, msiwe na wasiwasi kabisa kuhusu uzalendo wangu kwa nchi yangu!.

Kuna watu wana support hatua hiyo kwa hoja za msingi, kuwa DP World ni kampuni kubwa na ina uwezo mkubwa, inaendesha Bandari nyingi duniani, hivyo itatusaidia sana kuboresha uendeshaji wa Bandari yetu ya Dar es Salaam. Na kuna wanaopinga wakiwaita DP World ni matapeli, kufuatia kesi na migogoro mingi mahali pengi ambapo DP World wana operates, hivyo kitendo cha Bunge letu kuridhia hiyo IGA ya DP World bila kuifanyia a due diligence report, kumewafanya wachoke na kudhani, it's over, it's the end of the road kwa suala hili,. naomba kuwapa faraja na kuwatia moyo kuwa it's not the end!, it's not over yet until it's over!.

Hiyo HGA ni makubaliano tuu na sio mkataba, yaani ni an agreement na sio contract. Kila mkataba ni agreement, lakini sio kila agreement ni mkataba, mfano mzuri ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuunda Tanzania, ni makubaliano tuu na sio mkataba, mkifika mahali mkashindwa kuelewana, mnagawana tuu fito, kila mtu anasepa kivyake Je, Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?!.

Hivyo kile Bunge letu lilichoridhia, ni agreement tuu, tukiithibitishia serikali yetu, hawa DP World, pamoja na uzuri wao wote, pamoja na uwezo wao mkubwa wa kuendesha Bandari kibao, lakini ni matapeli na wana matatizo lukuki, hivyo serikali yetu iwe makini sana kabla ya kusaini HGA, na utepeli wao, ukiwekwa wazi hadharani peupe, kila mwenye macho aone, tutaisaidia sana serikali yetu, tutamsaidia sana Rais wetu Samia na kulisaidia taifa letu Tanzania tusiingizwe tena mkenge na Mwarabu wa Dubai kama alivyofanywa Chief Mangungo, hivyo serikali yetu, viongozi wetu na Bunge letu kuridhia fasta fasta kwasababu tuu, Mwarabu wa Dubai ni mtu Rahim, mkarimu, amemkirimu Mama yetu kuipaisha bure Tanzania kwenye Expo Dubai, akawakirimu waserikali wetu, kwa trips za Dubai, akawakirimu waheshimiwa wabunge wetu kwa trips za Dubai, na kuwakirimu waandishi wetu wa habari na media zetu kwa trips za Dubai.

Japo Rais wetu, Mama Samia, ana nia njema ya kweli na ya dhati kulisaidia taifa letu, lakini anapokutana na matapeli wa kimataifa wakamuingiza mkenge, sisi watu wa Mhimili wa Nne, the media, tuna wajibu wa kulisaidia taifa letu kwa kuonyesha utepeli huo uko wapi, kisha serikali yetu ikiamua kuendelea na HGA ya Mwarabu wa Dubai, sisi watu wa media, tutakuwa na a clear conscious kuwa angalau tumetimiza wajibu wetu, tumeieleza serikali yetu inavyotaka kuingizwa mkenge na kutapeliwa, hivyo vipengele vya mkataba wa HGA viboreshwe na kazi, iendelee!.

Kwa vile mimi licha ya kuwa ni mwandishi tuu wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, mimi pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, kwa kujitolea kutetea bure haki kwa wasio na uwezo, hivyo nitawaletea makubaliano hayo na kuwachambulia kuwaonyesha jinsi tunavyotaka kutapeliwa mchana kweupe.

  1. Utapeli wa kwanza mkubwa, ni hakuna mtu yoyote kati yetu aliyefanya a due diligence report ya DP World, tunaelezwa ni Governmental Organisation, wakati sii kweli, it's a private company!. Kabla ya kuingia mkataba wowote, lazima kwanza kufanyike kitu kinachoitwa a due diligence process na kutolewa a due diligence report. Hili halikufanyika hivyo serikali yetu kujikuta inaingia mkataba wa kimataifa na parties to contract which has no capacity to contract hivyo ku vitiate makubaliano kugeuka void hivyo makubaliano hayo yanakuwa null and void ab initio!.
  2. Mkataba wa IGA na HGA inaingiwa kati ya serikali na serikali, hivyo ukisoma documents za makubaliano utaona ni kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya UAE, lakini signatories kwa serikali ya Tanzania ni serikali kweli, lakini kwa serikali ya UAE, signatories ni Mwarabu wa Dubai wa DP World na sio serikali ya UAE, kwenye mkataba wameandika serikali ya Dubai, Dubai hivyo hapa tunatapeliwa!, serikali yetu inaingizwa mkenge kuingia mkataba na a private company disguised as a government of UAE kumbe ni kampuni binafsi!.View attachment 2653406
  3. Mkataba Kati ya serikali ya Tanzania na Dubai ni batili kwenye sheria za kimataifa. Maana Dubai sio nchi, a sovereign state kama ilivyo Tanzania, Dubai hapa inajitambulisha kama a State Party, Dubai is not a state hivyo haiwezi kuwa a state party, it has no the capacity to transact as an international IGA, haiwezi kuingia mikataba ya kimataifa na nchi, inaweza kuingia mkataba wa kimataifa na mamlaka ya Bandari, taasisi kwa taasisi, kama ilivyofanya hapa View attachment 2653409ambapo DP World iliingia mkataba na Mamlaka ya Bandari TPA, mkataba ambao Rais Samia aliushuhudia ukisainiwa kule Dubai during Expo Dubai.
  4. Sasa kampuni hii ya DP World iliyoingia mkataba na mamlaka ya Bandari, sasa inajigeuza nchi, sovereign state of Dubai, imeingia mkataba wa kimataifa na serikali yetu!, huku ni kututapeli!. Dubai is not a state, it's not a nation na nchi isiyo na sovereignty!. DP World is not a state, it's a private company, hapa imejigeuza ni nchi!. Huu ni utapeli!. View attachment 2653458
  5. Mikataba ya kimataifa inaingiwa kati ya nchi na nchi, na Falme ya Kiarabu inayotambulika kwenye sheria za kimataifa na sio Dubai ambayo ni sehemu ya UAE, hivyo hapa kuna utapeli!. Due diligence ingefanyika, hili lingeonekana.
  6. Status ya Dubai kwe UAE ni sawa na status ya Zanzibar ndani ya JMT, Zanzibar has no capacity to transact an international treaty kwasababu Zanzibar sio sovereign. Dubai pia sio sovereign, hivyo mikataba yote ya kimataifa ya Zanzibar, inaingiwa na JMT kwaniaba ya Zanzibar, IGA na HGA inapaswa kuingiwa kati ya Tanzania na UAE na sio Tanzania na Dubai!.
  7. DPW ni kampuni kama inavyoonyesha hapaView attachment 2653462
  8. Wanasheria wanapoamua kufanya magumashi ya kisheria, wanakuzuga kwa maneno ya kweli kwenye mkataba, mfano hapa Dubai inatambulishwa kama nchi,View attachment 2653466lakini mkataba wetu hii iliyoandikwa kama nchi, sio nchi kweli bali ni kampuni ya DPW!.
  9. Kwa vile kwa upande wetu ni serikali yetu, ili kuonyesha IGA ni kati ya serikali mbili, hapa wameitaja kampuni ya kiserikali ili kuiserikalisha kampuni binafsi ya DPW kuwa ni serikali View attachment 2653471
  10. Hivyo mikataba ya HGA utaokuja kuingiwa na serikali yetu, sio mkataba wa kimataifa wa kiserikali kati ya serikali yetu na serikali ya UAE, lakini hakuna chochote cha UAE bali kampuni binafsi ya DPW iliyoserikalishwa na kujifanya ni serikali!.View attachment 2653477View attachment 2653481
  11. Kwa vile mikataba ya kimataifa inahusisha state parties, HGA inayokwenda kuingiwa ni HGA kati ya nchi ya Tanzania ambayo ni state na kuingia na DPW iliyo ji stetisha kama a state ambapo huu pia ni utapeli!.View attachment 2653488
  12. Kwa Tanzania mamlaka yote ya nchi, mtu yoyote ili asaini mkataba wa kimataifa wa kuiingiza nchi, anapaswa apewe the Power of Attorney na Rais wa JMT. Hii hapa chini ni POA ya Rais Samia kumpa mamlaka Prof. Mbarawa kuingia huo mkataba kwa niaba ya Tanzania, View attachment 2653454POA hii kisheria ni defective, kwasababu japo imesainiwa na Rais Samia, lakini haina muhuri wa rais, au muhuri wa serikali, hizi documents za kisheria ikisemwa POA must be signed and stamped by the official seal, lazima iwe hivyo, not otherwise!, kama walivyofanya hawa counter parts hapa chini.View attachment 2653455
  13. Ili serikali yetu iingie kwenye mkataba wa kihalali wa kimataifa na taasisi ambayo sio nchi, kulitakiwa kuwepo POA toka UAE kuipa mamlaka Dubai kuingia mkataba wa kimataifa kwa niaba ya UAE, then ndipo Emirate wa Dubai angeweza kuwapa POA DPW kujigeuza ni nchi.
  14. Hapa Prof. Mbarawa almanusura angekosea kusaini View attachment 2653452
  15. Hakuna ubaya wowote kwa kampuni yoyote kuingia mkataba na serikali under PPP, lakini hili la kampuni binafsi iliyo serikalishwa kuingia an International treaty na serikali yetu, halikakaa vizuri.
  16. Jambo jingine, kuna kipengele cha kuizuia nchi isiendeleze Bandari nyingine, hivyo kuiweka mashakani Bandari ya Bagamoyo, hili halikubaliki hata kidogo!.
Hitimisho
Kwa vile Rais Samia ana nia njema ya dhati kuisaidia nchi yetu, wasaidizi wa rais na sisi Watanzania wengine wote tuna wajibu wa kumsaidia rais wetu na kulisaidia taifa letu na huu ndio uzalendo wa kweli.

Paskali.
Una akili kubwa sana sema huwa inazongwa zongwa na uoga Mixer unafiki. Ndio maana unazunguka sana ili kutuambia Namba Moja ni Aidha hajielewi(Hana akili) kabisa au Ametishwa na anawaogopa sana Bwana Mananasi na Mchele wa Igunga. Na zaidi andiko lako hili ni kama unasema Hao watu wasipokuwepo Chini ya hili Jua letu, basi Tz inaweza kuwa nchi konki kinyama. Huyu bwana ni wakutandika Shabazz hadharani
 
Mimi nilidhani pamoja na kuwa nchi Ina mfumo na vyombo vya kusaidia ulinzi maendeleo na kulinda maslahi yake, idara ya Usalama wa Taifa ingekuwa ndio chombo makini na nyeti kwa yote.

Hili jambo la bandari, idara inahusikaje hapo? Haina taarifa za kujibu mashaka? Haina stadi za kuchambua, kupima na kuainisha faida na madhara kwa miaka mingi ijayo?

Mbona hata waziri mwenye dhamana inaonekana kama kastukizwa kwa baadhi ya hoja?

Haipendezi jambo kubwa kama hili kupitishwa kwasababu mkuu kaona ni jema. Lipitishwe kwa sababu hoja zote za msingi kiusalama, kibiashara, kiuchumi na maslahi vyote vipo sawa.

Kama idara ya Usalama huwa inaingizwa kazini baada ya wakubwa kusaini, nahisi siyo salama. Au kama hiyo idara haikuwa na ijuacho kuhusu huyo mwekezaji kiasi cha kushindwa kupenyeza taarifa kwa wakuu, mantiki inaniongoza kuamini Kuna tatizo.

Hili ni funzo, Kuna rekebishika. Leo tumeanza na bandari. Mambo ya ufanisi kwetu ni kitendawili. Huenda mbele tutahitaji pia wawekezaji kwa kila kitu.

Mungu ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
idala yetu pia inaweza kuwa manipulated tuu mkuu ni watu wale Kama wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa waandishi wa magazeti wameahidiwa fedha iwapo watapigia Debe mkataba wa kuuza nchi!
These mercenaries are now busy spinning to facilitate the sale of our country kama Mangungo wa Mvomelo alivyouza kwa shanga enzi hizo za utumwa!
Nchi unaiuzaje kwa mfano?. Tulikuwa na TICTS, mbona nchi yetu bado tunayo?

Pale Airport kuna Swiss port na NAS, hawa DP World hawatakuwa wa kwanza kufanya biashara hapa nchini.

Uoga unatusumbua miaka yote.
 
Back
Top Bottom