GHOST RYDER
JF-Expert Member
- Jun 10, 2011
- 1,025
- 475
Japan Bado wanahaha na Mionzi sisi Mambo Saafii
Serikali ya Japan inafanya uchunguzi wa kina kwa vifaa vya kisasa (ambavyo sisi wala hatuna na tunashabikia kuwa samaki wako salama na hawana mionzi ya Nyuklia) ili waweze kubaini kama mchele, Nyama, samaki, mazao ya Bahari na matunda yanayopatikana katika miji ya Miyagi na Fukushima vimeathiriwa kwa kiasi gani na Mionzi ilivovuja kutoka kinu cha Nyuklia cha fukushima.
Inashangaza kuona Tanzania suala hili limechukuliwa kisiasa zaidi huku shehena ya Samaki waliokamatwa na TFDA wanatokea katika Mji wa Miyagi na sehemu kutoka fukushima, hapakuwa na haja ya kuharakisha majibu mepesi wakati vifaa vya kuchunguza mionzi hii nina mashaka kama tunavyom katika kiwango hicho ambacho Japan wanahangaika.
Katika kutekeleza mkakati huo serikali ya Japan hivi majuzi izuia shehena ya Nyama iliyokuwa ikisafirishwa kwenda nje ya Nchi hiyo kutokana na kubainika kuwa na viwango vya mionzi juu ya kiwango hatarishi kwa afya ya Binaadam.
Uchunguzi mkali unaendelea katika miji ya Niigata na Fukushima ambayo hivi karibuni imekumbwa na Mvua nyingi ambazo zinaweza kuchangia kusambaa kwa kasi kwa mionzi hii ambayo inahofiwa kumea katika mashamba ya mpunga na mazo mengine ya Kilimo na Mifugo.
Inahofiwa zaidi ya zaidi ya asilimia 40 ya mpunga unaozalishwa japan utakuwa umeathiriwa na mionzi, tafiti zinazoendelea ni kubaini ni kwa kiwango gani mpunga huo utakuwa umeathiriwa na mionzi.
Kwa mintarafu hiyo hakuna ushawishi wowote ambao serikali ya Tanzania inaweza kuuthibitishia Umma kuwa Samaki hao kutoka Nchini Japan wapo salama, sina shaka ubalozi wa Japan ulitumia kauli ya Kidiplomasia zaidi kuepusha kadhia hiyo ambayo ingezua mtafaruku mkubwa katika siasa za kimataifa, na kwa kupenda kuabudia weupe tukaikUbali bila shaka yoyote.
Kuna kichwa kazi bado ipo .
Source: www.scientificamerican.com/article.cfm?id=japanese-rice-to-be...
www.sciencenewsdaily.org/energy-news/cluster108394560/
ADIOS