Japan Bado wanahaha na Mionzi sisi Mambo Saafii

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475
Japan Bado wanahaha na Mionzi sisi Mambo Saafii


Serikali ya Japan inafanya uchunguzi wa kina kwa vifaa vya kisasa (ambavyo sisi wala hatuna na tunashabikia kuwa samaki wako salama na hawana mionzi ya Nyuklia) ili waweze kubaini kama mchele, Nyama, samaki, mazao ya Bahari na matunda yanayopatikana katika miji ya Miyagi na Fukushima vimeathiriwa kwa kiasi gani na Mionzi ilivovuja kutoka kinu cha Nyuklia cha fukushima.

Inashangaza kuona Tanzania suala hili limechukuliwa kisiasa zaidi huku shehena ya Samaki waliokamatwa na TFDA wanatokea katika Mji wa Miyagi na sehemu kutoka fukushima, hapakuwa na haja ya kuharakisha majibu mepesi wakati vifaa vya kuchunguza mionzi hii nina mashaka kama tunavyom katika kiwango hicho ambacho Japan wanahangaika.

Katika kutekeleza mkakati huo serikali ya Japan hivi majuzi izuia shehena ya Nyama iliyokuwa ikisafirishwa kwenda nje ya Nchi hiyo kutokana na kubainika kuwa na viwango vya mionzi juu ya kiwango hatarishi kwa afya ya Binaadam.

Uchunguzi mkali unaendelea katika miji ya Niigata na Fukushima ambayo hivi karibuni imekumbwa na Mvua nyingi ambazo zinaweza kuchangia kusambaa kwa kasi kwa mionzi hii ambayo inahofiwa kumea katika mashamba ya mpunga na mazo mengine ya Kilimo na Mifugo.

Inahofiwa zaidi ya zaidi ya asilimia 40 ya mpunga unaozalishwa japan utakuwa umeathiriwa na mionzi, tafiti zinazoendelea ni kubaini ni kwa kiwango gani mpunga huo utakuwa umeathiriwa na mionzi.

Kwa mintarafu hiyo hakuna ushawishi wowote ambao serikali ya Tanzania inaweza kuuthibitishia Umma kuwa Samaki hao kutoka Nchini Japan wapo salama, sina shaka ubalozi wa Japan ulitumia kauli ya Kidiplomasia zaidi kuepusha kadhia hiyo ambayo ingezua mtafaruku mkubwa katika siasa za kimataifa, na kwa kupenda kuabudia weupe tukaikUbali bila shaka yoyote.

Kuna kichwa kazi bado ipo….

Source: www.scientificamerican.com/article.cfm?id=japanese-rice-to-be...
www.sciencenewsdaily.org/energy-news/cluster108394560/


ADIOS
 
Ukweli ni kuwa hao samaki hawangeweza kuingizwa nchi yoyote ile isipokuwa Tanzania na hao wafanya biashara walijua hilo fika. Sio samaki tu kuna bidhaa nyingi tu kutoka Japan ambazo soko pekee duniani linapatikana hapa Tanzania tu. Tanzania kufa kufaana.
 
Serikali imewachoka wananchi wake,wenzetu wanakesha kuwaokoa wananchi sisitunaficha udhaifu wa serikali kwa kuangamiza wananchi.shame on us.
 
Mimi pia nina mashaka sana na magari lukuki yanayoendelea kuingizwa toka Japan. Jee kuna anayeyapima dhidi ya mionzi ya nuclear? Bila kujua watanzania wengi mno tunaweza kuathirika - tukawa tunazaa vilema baadaye na kupata kansa za ajabu ajabu!
 
Tanzania kuna soko gani la samaki linalowafanya wavue Japan na wawasafirishe mpaka Tanzania kwa gharama na kuuza kwa Purchases power gani hiyo tuliyonayo?
 
Mionzi hii ni hatari sana kiasi kwamba hata mtu anayetoka huko lazima tuwe na wasiasi naye kama katrap hiyo mionza
 
Tanzania kuna soko gani la samaki linalowafanya wavue Japan na wawasafirishe mpaka Tanzania kwa gharama na kuuza kwa Purchases power gani hiyo tuliyonayo?

Oooh God, Prof huna habari hata vifua vya sangara kutoka Mwanza kwa ndugu zangu wasukuma ni ghafi muhimu katika soko la Hoteli za Kitalii kuliko hata Minofu.

Kiwanda cha Nile Perch Kilichopo eneo la Nyakato huko Mwanza kinavuna asilimia 90 ya mapato yake kwa kuuza vifua vya sangara na fish maws *mabondo* kama sijakosea katika soko la hoteli za Kitalii za dar na viwanda china kwa fish maws.

Hapa kwetu consumerism culture imeathiri trend ya min market nyingi sana product za bahari kutoka nje zina soko zaidi kuliko hata wale samaki fresh pale ferry.

Tafiti hili leo kama una muda kwa muda mfupi utajiridhisha katika hili
 
Last edited by a moderator:
Serikali imewachoka wananchi wake,wenzetu wanakesha kuwaokoa wananchi sisitunaficha udhaifu wa serikali kwa kuangamiza wananchi.shame on us.

Hapa ndipo aliulizwa Ndugai katika mjadala wa STAR TV jumamosi iliyopita, itakapofika wabunge hawayavumilii haya kama walivyo wananchi mnawafanyaje hata kama wataropoka hovyo bila kuzingatia kanuni japo si ustaarabu na msingi ya uendeshaji wa shughuli za Bunge je mnafanyaje hapo. Domo likamjaa mate na vicheko vya kinafiki viiiingi. Kweli inakera sana kwa siasa chafu hizi za kushabikia ujinga na kujifanya tuna majibu ya haraka huku watanzania wenzetu wanateketea
 
shje twala samaki twala. Kitumbo(mchele huu cjui walimwa wapi) twala magari from japan twaendesha hata kama yatatoka niigata

Na kwa bei ya mchele ilivyopanda kwa sasa mchele huo kutoka Japan ushapenya siku nyingi na unauzwa mini market tsh. 1200 / 1300 huku mchele wa kibongo ukiendelea kubaki shilingi 1500 maeneo mengi ya Dar katika mfungo huu mtukufu wa Ramadhan
 
UPDATES:

France 24

Program FOCUS

18 AUG 2011 - 10:00

JAPAN inafanya usafishaji na uchunguzi wa vimelea ya miozi huko fukushima. Zoezi hilo linalojulikana kama JAPAN DECONTAMINATION PROCESS linahusisha magari....vyakula....mpaka Binaadam

VIPI WADAU
 
Back
Top Bottom