January Makamba: Najua kinachoendelea BUMBULI hata kama nikiwa New York

Tatizo kubwa sana lililopo kati ya wabunge wetu na wapiga kura wao ni ukosefu wa mawasiliano. Hili halina mjadala. Ni vigumu sana kwa mwananchi na mpiga kura wa kawaida kuwasialiana moja kwa moja na mbunge wake. Kwa mfano hapa hapa JF kuna watu wengi tuu wamekuwa wakumuulizia mbunge wa jimbo la Rombo. Wanadai kuwa haonekani jimboni na hata hapatikani kwa simu. Wengine hata wakafikia kuazisha thread ya kuomba aliye na namba yake. Sasa kama mbunge haonekani jimboni kwake na hapatikani kwa simu, hapo sijui atatatuaje atajuaje matatizo ya wapiga kura wake.

Kutokana na tatizo la mawasiliano, inakuwa vigumu kwa mbunge kuyajua matatizo ya wananchi na kuyafikisha sehemu husika. Mbunge anaweza kuwa na priorities ambazo zinatofautiana na zile za wapiga kura wake kutokana na uhaba wa mawasiliano. Kwa maana nyingine, hataweza kufuatilia matatizo ya wapiga kura wake kama hana mawasiliano nao.

Mawasiliano na mbunge yanaweza kufanywa kwa njia mbalimbali. Lakini njia anayotumia January Makamba ni mpya kwetu. Whether or not inafanya kazi, wananchi wa Bumbuli ndio wanajua. Kuna mwananchi wa mmoja wa Bumbuli hapo juu amejaribu kuelezea vizuri kuwa inafanya kazi. Lakini huo ni mfano mmoja tuu na hatuwezi ku-rely on it kusema kuwa system ya Makamba inafanya. Tutahitaji more case studies kutoka Bumbuli.

Having said, that bado nadhani system yake ni nzuri. Anachofanya ni kurahisisha mawasiliano na wapiga kura wake kwa kutumia teknologia ya kisasa zaidi. Labda tujiulize ni wangapi hapa tunaweza kuwasiliana na wabunge wetu moja kwa moja? I am sure tutakuwa wachache sana. Lakini hili la kuwasiliana na wapiga kura wake kwa SMS lisimfanye asiwatembelee wapiga kura wake personally na kusikiliza matatizo yao na kuyafikisha sehemu husika.

Lakini suala la mawasiliano ni tofauti na ufuatiliaji. Kunaweza kuwa na mawasiliano mazuri lakini kama hakuna ufuatiliaji, then mawasiano yanakuwa useless. At the end of the day atapimwa sio tuu kwa kurahisisha mawasiliano na wapiga kura wake bali pia kwa kufuatilia na kuyatafutia ufumbuzi matatizo ya wapiga kura wake.

So, kwa suala la kurahisisha mawasiliano na wapiga kura wake kupitia teknologia ya sasa nampa plus. Whether the system actually works in the sense that matatizo ya Wanabumbuli sasa yanafuatiliwa na kutafutiwa ufumbuzi kupitia SMS wanazotuma, ni Wanabumbuli pekee ndio wanaoweza kujibu hili swali.
 
Kwanza aondoe hiyo fikra ya kukanyaga New York kwa sasa; Mpaka atatue matatizo na CIA/FBI

Mdogo wake kiume akiliekuwa Atlanta kuoa Mmarekani Mweupe bado haijasaidia
 
Mimi nampongeza Makamba kwa idea hiyo nzuri, ila ningependa kujua zile ahadi zilizowahi kuandikwa kwenye magazeti mbali kama ameshatekeleza?

Ebu tujikumbushe gazeti la economist lilisema nini kuhusu huyu Mheshimiwa:

"But now he must prove himself on the ground. He showed his steel by ousting a long-serving CCM parliamentarian. It helps that he comes from the main town, Lushoto, and lived there as a boy. Up in the village he promises fertilisers, medicine, more teachers. Electricity? No, too costly.Bumbuli is among Tanzania's most densely populated constituencies. Most of its people farm tiny plots too small to be subdivided further. But Mr Makamba has a plan. He wants to borrow $10m from Wall Street philanthropists, to be repaid in ten years. The sum, he says, will be invested in east African treasury bonds and stocks, in the hope of dividends producing $700,000 a year to invest in Bumbuli. Some of the cash would help farmers package their fruits and vegetables. Mr Makamba dreams of refrigerated lorries owned by the community leaving daily at dawn for Dar es Salaam and Nairobi with "Fresh from Lushoto" produce. Another project aims to parcel a scenic bit of the constituency and sell it to a university to set up a campus for 5,000-odd students. Turkish investors, he claims, are interested."

Source: Tanzania's election: Promises, promises | The Economist
 
Back
Top Bottom