January Makamba: Najua kinachoendelea BUMBULI hata kama nikiwa New York

Mbona unaleta habari za uswazi?jadili hoja sio kudandia mambo ya kipuuzi!

Habari za Uswazi zikoje?

Huyu jamaa anasema mengi kuhusu uongozi wakati kuna habari yeye na familia yake wameomba mamilioni ya dola za Kimarekani kwa ajili ya uchaguzi, kutoka kwa wafadhili wa nje ya nchi wasio Watanzania, huku wakiwaambia wafadhili hao "we are talking about a future energy minister" . Kimsingi shutuma za umalaya wa kisiasa.

Sasa kama kuna allegations hizo, kuna email imeletwa hapa, hatujasikia kukanushwa, sisi tutakuwa vipi kama tutaendelea kuwaamini tu hawa watu kwamba wanafaa?

Utasemaje mie kuuliza response - hata sijasema kwamba habari hii ni ya kweli au la- ni "habari za Uswazi"?
 
ndio maana nikasema labda macho yangu hayaoni vizuri..ahsante kwa kunionyesha huo mstari...kwa hiyo anajifagilia kuwa yuko juu katika kufatilia mabo kuliko wenzie..haya makamba mdogo.
Sidhani kama anajifagilia lakini kijana kaonesha njia kwenye siasa za kisasa na sisi tufuate. Thanks kwa kuelewa
 
Sidhani kama anajifagilia lakini kijana kaonesha njia kwenye siasa za kisasa na sisi tufuate. Thanks kwa kuelewa

Mtu anayeonyesha njia "kwenye siasa za kisasa" anatakiwa atuonyeshe anavyothamini mawasiliano na wananchi. Na njia moja ya kuthamini mawasiliano na wananchi, ukishutumiwa unafafanua nini kimetokea. Kama allegations ni upuuzi usio kweli unasema hilo.

Ukikaa kimya unaendeleza siasa za kizamani zile zile. Wengine tunaamini kwamba huja respond kwa sababu shutuma ni kweli.
 
Nafkiri viongozi wetu wangeacha fikra potofu kua tunachohitaji ni wao kujua matatizo yetu ili wakayazungumzie kwenye vikao vyao. Bahati mbaya hata wananchi wanaridhika sana wanaposikia mbunge wao anawapigania bungeni au anayajua matatizo yao. Nafkiri kipimo kizuri cha utendaji wao kingekua wamefanya nini majimboni mwao.

It's ok ume design njia nzuri ya kujua matatizo ya wananchi wako,so what? Namfurahia kiongozi ambaye siku anamaliza mda wake, anasema "kwa kushirikiana na wananchi, eg tumejenga shule,barabara,madaraja, uzalishaji wa mazao umepanda kwa kiasi hiki, ufaulu wa wanafunzi umeongezeka kwa kua tumekua na shule bora zenye vifaa, wananchi wangu wamekua na makazi bora, yaliyo pangwa vyema baada ya ku-mobilize ujenzi wa nyumba bora na upangwaji wa makazi" lakini huwa tuna sikia porojo tu.......mtu yuko bungeni vipindi 3 but ktk kampeni anazungumzia matatizo yaleyale aliyozungumzia wakati anaomba kura ktk 1st term
 
Watu wengi tuna ugonjwa wa kukurupuka bila kuangalia content vizuri, hii ni hatari n ndio maana mafisadi wanatupiga mabao kila siku. We need to read between them goddem lines!! Huyu jamaa January yuko creative. Angalia anajiaanda kupeleka muswada wa wapangaji bungeni. Kwa miaka 50 CCM imekuwa na wabunge machachari ila walishindwa kutunga sheria za ku-mprotect mpangaji, yeye kaliona
 
Mheshimiwa ni wazo zuri, nakuongezea ushauri kidogo.

Wacha kutumia kiingereza kwani unataka ujumbe uwafikie Watanzania wenzako zaidi, na wengi wao Kiingereza ni haba kwao.

Wacha kutumia Kiingereza kwani hujui kukiandika vizuri, kama hicho kilichoandikwa hapo juu ni Kiingereza ulichoandika wewe mwenyewe, nakushauri usiandike tena na ukifanyie mazoezi, hakina hadhi ya Mbunge, unakuwa kama Sugu!

kama siyo nyie wenyewe mlo sababisha wananch wasikijue kiingereza ni nan mwingne?.We shall blame ön you forever and ever,hamfai.
 
Hata mimi ningefanya hivyo given the opportunity kua dada yangu yupo ktk shirika hilo la cmu....it makes a lot of things easier.
Ni sawa na kusema kama baba yake angekua anamiliki mabasi ya shambalai ( lushoto-Dar) then wale wote wa jimboni kwake wangemtumia barua zao za maoni, nk kupitia hilo basi la shambalai
 
- Siasa za majitaka sana, they never did ask anybody for anything I spoke to Januari for three hours looking him in his eyes nothing majitaka tupu!, kila biandam ana mapungufu lakini sio ya kubambikiana ni upuuuzi na inatuharibia Viongozi wetu wazuri for nothing, Januari is our Nation's future leader he is young and articulate if not smart!

Es!

Really? ama kweli njaa zinaliangamiza taifa
 
Ujumbe umenilenga mimi na mimi ni "mtu wake" na huyo ni mtunga sheria ambazo hazitumiwi na wana Bumbuli pekee na humhusu kila Mtanzania.

Wazo lake ni zuri sana, linafaa kuigwa lakini lugha aliyotumia haifai kwa kuwa Watanzania wengi Kiingereza chao ni haba, na aliyeandika hakielewi kukiandika vizuri. Kwa mbunge si vyema. Kama ana kasoro za kuandika kiingereza angetumia wajuao waka edit halafu aka post. Tunaongelea Mbunge hapa hatuogelea

Umetaja Uingereza, ngoja nikufunde kuhusu Uingereza, Hutamkuta Mbunge wa Uingereza aki communicate na wananchi wake kwa lugha nyingine yoyote zaidi ya Kiingereza, ingawa, shule zao kuanzia "primary" ni compulsory kujifunza na lugha ya pili. Wanakienzi Kiingereza chao na ndio lugha nyepesi ya kuwasiliana huko kwao.

Jee, sisi lugha nyepesi ya kuwasiliana, iwe ujumbe umeletwa kwangu au kwa wana Bumbuli pekee, ni Kiingereza? Fikiri.

Mkuu Ribosome,

Ulitaka January aandikeje Kiingereza chake ndio utambue kwamba ameandika Kiingereza kizuri? Sioni ubaya kabisa wa lugha katika hiyo article yake. Ameandika kama vile anaongea, anahutubia au anajadiliana na hao anaowasimulia.

Kwa taarifa tu UK ina lugha zaidi ya Kiingereza na Wabunge wanazitumia kuwasiliana na wapiga kura wao. kwa mfano Wales kuna Cymraeg ambayo ni official na inatumika hata mashuleni. Pia Scotland kuna Gaelic nk. Hata maeneo mengine ya London wana Cockney slang, akikuambia anaomba bottle utafikiri anaomba chupa kumbe kitu kingine kabisa mkuu.

Muhimu kwenye lugha ni kuhakikisha wasikilizaji wako au wasomaji wako wataelewa unataka kuongea nini. Kama ni suala la umahiri wa lugha basi kuna watu waliosomea lugha na sio vinginevyo. Tony Blair alishindwa kuandika neno tomorrow mbele ya waandishi wa habari. Hata walipomwambia arudie bado akakosea na wala haikuwa issue kubwa kabisa. Ingelikuwa TZ, hapo blogs na magazeti yote yangeliandika.

Asilimia kubwa ya Watanzania tena wasomi, hatuwezi kuandika mistari kumi kwa kiswahili bila makosa lakini tunatumia muda mwingi kusahihisha Kiingereza.

January ni creative na aendelee hivyo hivyo, itamsaidia. Hata kwenye masuala ya umeme unamkuta anakuja na ideas nyingi sana. Kwa TZ ambayo ina opportunities nyingi tunataka watu ambao ni creative ili angalau baadhi ya hizo fursa tuweze kuzibadilisha na ziwe na faida kwa wananchi.
 
Mheshimiwa ni wazo zuri, nakuongezea ushauri kidogo.

Wacha kutumia kiingereza kwani unataka ujumbe uwafikie Watanzania wenzako zaidi, na wengi wao Kiingereza ni haba kwao.

Wacha kutumia Kiingereza kwani hujui kukiandika vizuri, kama hicho kilichoandikwa hapo juu ni Kiingereza ulichoandika wewe mwenyewe, nakushauri usiandike tena na ukifanyie mazoezi, hakina hadhi ya Mbunge, unakuwa kama Sugu!

mbona humcheki mtu asiyejua kikwenu...i mean kisambaa! Umeshakuwa brainwashed na wazungu!
kiingereza my"S"!
 
January sisi ni vijana na mimi pia baba yangu katokea huko Lushoto. Tatizo kubwa kule ni maji, umeme na barabara. Barabara imeishia Lushoto mjini lakini kule milimani hatuna maji kwasababu huwezi kuchimba kwenye milima ya Lushoto. Umeme vilevile ni tatizo. Kwa mawazo yangu hayo ndiyo matatizo makubwa ambayo ungeweza kufikiria na si kwa bumbuli tu bali Lushoto. Mimi ningeomba wahusika wote mkutane pamoja na mtatue tatizo la maji, umeme na barabara
 
Mbona unaleta habari za uswazi?jadili hoja sio kudandia mambo ya kipuuzi!

Kweli majina (mfno Ground Zero) huathiri tabia ya mtu na upeo wake,mfano Shida,majuto,Matonya nk. Na pia kwa watu wanaowaza kwa mapana na marefu wewe ndio mpuuzi na pengine mshenzi wa makusudi kwa kukashifu mwenzio pasipokuhoji.
Makamba ni pandikizi la mafisadi na makaburu,mtake msitake lakini huu ndio ukweli na anajaribu kuji-moddel ili awe public figure then atapewa cheo cha presidential material ili aonekane anaweza (hili litathibitika katika baraza jipya la mawaziri)!!

kwa kuwa sina mda wa kuandika sana kwa sasa basi tujiulize/jiulizen maswali machache tu yafuatayo!!
1) Ajira yake pale magogoni aliipata kwa kutumia vigezo gani?? Ilitangazwa??

2) masomo yake kule ughaibuni kwa mda wote yaligharamiwa na nani?? Kwa mfumo upi uliorasmi/si rasmi??
3) hivi mnazani ni bahati mbaya tu Makamba huyu alimridhi Shelukindo kuanzia ubunge wa Bumbuli hadi vyeo alivyonanavyo kule bungeni?? Fanyeni tathimini katika wabunge wapya na pia jaribuni kujifikirisha watu washenzi wangapi wapo na maslahi yao na watu wao kwenye ile wizara alipo karibu na pia kundi gani yupo huyu jamaa!!

3) tuachane na hotel ya baba yake pale Morogoro mlimani na nyumba yake, je ile mansion aliyojenga dada yake ana uwezo kwa mshahara wake kujenga kwa kununua jumba kama lile??

4) tuhuma za ukuadi wa rushwa wa dada yake kwa niaba yake(puuzia kujitoa kwa unyumba kwake kwa wazungu wa Barrick), hakumtoi sifa ya kuwa kiongozi wa umma???

Tuendeleeni kuitikia vibwagizo vyao tu watwana wao halafu tuje tusage meno!!!
 
- He has a vision and very articulate, open mind and smart!

Es!

Nothing new.

Coffee farmers in Mbinga know the prices at New York on the same day and decide or not to sell their coffee at TCB auction in Moshi.
MVIWATA has created the same mechanism: Its members all over Tanzanians can easily access marketing information in Kariakoo, even before deciding to hire FUSO to carry their crops...
 
Kweli majina (mfno Ground Zero) huathiri tabia ya mtu na upeo wake,mfano Shida,majuto,Matonya nk. Na pia kwa watu wanaowaza kwa mapana na marefu wewe ndio mpuuzi na pengine mshenzi wa makusudi kwa kukashifu mwenzio pasipokuhoji.
Makamba ni pandikizi la mafisadi na makaburu,mtake msitake lakini huu ndio ukweli na anajaribu kuji-moddel ili awe public figure then atapewa cheo cha presidential material ili aonekane anaweza (hili litathibitika katika baraza jipya la mawaziri)!!

kwa kuwa sina mda wa kuandika sana kwa sasa basi tujiulize/jiulizen maswali machache tu yafuatayo!!
1) Ajira yake pale magogoni aliipata kwa kutumia vigezo gani?? Ilitangazwa??

2) masomo yake kule ughaibuni kwa mda wote yaligharamiwa na nani?? Kwa mfumo upi uliorasmi/si rasmi??
3) hivi mnazani ni bahati mbaya tu Makamba huyu alimridhi Shelukindo kuanzia ubunge wa Bumbuli hadi vyeo alivyonanavyo kule bungeni?? Fanyeni tathimini katika wabunge wapya na pia jaribuni kujifikirisha watu washenzi wangapi wapo na maslahi yao na watu wao kwenye ile wizara alipo karibu na pia kundi gani yupo huyu jamaa!!

3) tuachane na hotel ya baba yake pale Morogoro mlimani na nyumba yake, je ile mansion aliyojenga dada yake ana uwezo kwa mshahara wake kujenga kwa kununua jumba kama lile??

4) tuhuma za ukuadi wa rushwa wa dada yake kwa niaba yake(puuzia kujitoa kwa unyumba kwake kwa wazungu wa Barrick), hakumtoi sifa ya kuwa kiongozi wa umma???

Tuendeleeni kuitikia vibwagizo vyao tu watwana wao halafu tuje tusage meno!!!

Unajua saa nyingine hizi cheap popularity zina cost sana.
Imagine wewe unayempigia debe, sifa unazompa (cheap popularity) na hizi tuhuma zinalingana?
Bro, think twice kabla ya kujaribu kumpigia mtu kifua, unaweza kummaliza kabisa.
watu wa JF sio sawa na wale wa Bumbuli.
waombe ma mods watoe hii thread unamumbua dogo bure.
 
Mhe. January tumia lugha ya kiswahili, huu ni ushauri. Kisha nenda kaangalie eneo la KWEMILUNGU mpaka MPALALU utajionea makandarasi wa barabara mauzauza waliyofanya!! Vijana wengi jimboni mwako wapo mtaani Je una mkakati ngani mpaka sasa? Nakushauri tembelea jimbo kijana. Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom