Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,482
- 40,001
Anasema miaka 10 iliyopita serikali iliamua TANESCO ibinafsishwe; anatoa historia ya mgao; walipokuja NETGROUP solutions kuendesha TANESCO, walitumia maji mengi kuzalisha umeme.Hawakuwekeza kwenye chochote hasa miundombinu hivyo tatizo likaanza ukichanganya na uhaba wa mvua.
Walitumia jitihada kubwa kukusanya madeni kwa vile mkataba uliweka kipengere cha bonus .So walikazana sana kukusanya madeni kwa sababu ya motisha wa bonus. Mwaka 2006 SERIKALI IKARUDISHA TANESCO serikalini. Matatizo y aumeme kwa kiasi yanatokana na mambo mengi. Haijakuwepo big investment katika uzalishaji hata ugavi.
Pia anasema kuwa umeme mwingi unapotea njiani kutokana na uchakavu wa miundo mbinumore than 20% ya 1100MW inayozalishwa. Anasema umeme unapotea mathalani, ni mwingi kuliko ule unaozalishwa na Songas!
Anaelezea matatizo ya umeme:
a. Kiwanda cha MBolea kufungwa mara tatu
b. Vodacom wanatumia fedha nyingi
c. Viwanda vidogo
Anasema wananchi wanalalamika na kuwauliza kama "wana akili" kwamba watu wanawashangaa iweje iwepo mitambo ipo imezimwa. Anasema yapo mapendekezo 30 la kuwasha mitambo ya Dowans ni moja tu.
Ameulizwa swali "kwanini miaka mitano ya kwanza Serikali haikuwekeza kwenye uzalishaji wa umeme?" Jibu lake: "Swali unaloniuliza ndilo na mimi nauwaliza serikali" (akimaanisha barua yake kwa Ngeleja).
Anaelezea suala la Stielger's Gorge anasema tatizo limekuwa ni suala la mazingira ndio limechelewesha sana. Anasema lakini sasa hivi jambo hilo linazungumzika na kuwa wapo taasisi binafsi ambazo wako tayari kuwekeza (akigusia suala la RUBADA na Brazili). Kwa hiyo anasema ni suala la kulinda maslahi ya "mazingira" na yale ya wananchi.
Ameuliza kuhusu suala la Dowans na anakiri kuwa Mtambo haujawashwa na anakiri ni kwa sababu ya "unafuu uliopo sasa kwa sababu ya mvua" lakini anasema kuwa "ni unafuu wa muda". Anasema kwa sababu mabwawa yaliyojaa maji sasa hivi ni yale yanayotegemea maporomoko ya maji (water falls) lakini siyo yale mabwawa ya hifadhi (water reservoir) kama Mtera.
Anaunga mkono kubadilisha sheria ya manunuzi ya umma ambayo itaruhusu manunuzi ya vitu vilivyotumika. Anasema kwa mfano nchi kama za kwetu na mazingira yetu na ya kibiashara dunia ni vizuri kuruhusu manunuzi hayo. Anasema sheria lazima iwe "flexible". Anasema nchi kama za kwetu haziwezi kupata vitu vipya kila wakati na anatolea mfano wa ndege.
Ameulizwa "kuna emergency ya kununua ndege"? anasema hata barabara siyo emergency - wanacheka tu - kwani anaambiwa kuwa mambo mengine ni ya mipango ya muda mrefu. Anasema "udharura" mwingine ni wa kujitakia. Anadai kuwa ( naamini kwa makosa) kuwa huwezi kwenda kununua mtambo wa kuzalisha umeme MW100 ni lazima usubiri miaka miwili.
Anasema kuwa serikali inataka kukodisha mitambo ya Tanesco ya 260 na amewatumia ujumbe Tanesco kuwa ahadi yao isipotimizwa basi "watakamatana" na "kuulizana vizuri" huko Dodoma.
Ametoa wito kwa watu ambao wameathirika na uchakachuaji wa mafuta wafike ofisi za Bunge jijini Dar leo ambao wanakusanya maoni ya nini cha kufanya.