January kwenye Power Breakfast: Aelezea tatizo la Mgao wa Umeme

attachment.php


Ndio maana aliforce William Ngeleja aingie kwenye baraza la mawaziri kama waziri wa nishati na madini kwa nguvu zote maana ni kijana wake na amemuweka kwa maslahi yake zaidi na si ya nchi JK inabidi aonyeshe uungwana kumfukuza kazi huyu dogo hatufai kabisa

Ngeleja hana shida yoyote so far ni mtendaji mzuri. Angalia mengi aliyoyafanya tangu aingie hapo! usiangalie kuwa kabla ya hapo alikuwa wapi. Kila kijana aliyeko kwanye siasa kuna sehemu ameanzia. Tuangalie Ngeleja je kuna maamuzi ameyafanya ya kumpa favour RA? Kwangu mimi hakuna! Lakini kama ni maoni yangu jamaa anachapa kazi sema nchi yenyewe ndiyo hii ambaye hata mwenye nchi mwenyewe anaiangalia tu jinsi alivyoicomplicate mwenyewe!!!
 
Hii nchi itaendelea pale tutakapoacha kuongea ongea tuuu na kuanza kutekeleza majukumu kwa vitendo na si kwa maneno. WaTz sasa washachoka kusikiliza maneno tu na ahadi nyingi, tunachotaka sasa ni vitendo. Kila mtu anakuwa muongeaji tu, kuanzia mkuu wa nchi, waziri mkubwa mpaka hawa wakina January wote wanapiga porojo tu. Imefika wakati hata unaposikia mkuu wa nchi anaongea unabadili station coz una uhakika hakuna la maana litakaloongelewa, na hii ni hali ya hatari sana.

Zamani unapopata taarifa kuwa Rais au Waziri mkuu (Sokoine) anahutubia nchi lazima uhakikishe unatafuta radio umsikilize hata kama utatembea mpaka kwa jirani ili tu usikilize hiyo hotuba. Siku hizi hakuna kitu, imekuwa ni nchi ya bla bla tu. Watz ogopeni sana hii aina ya viongozi wanaopenda kujionyesha kwenye vyombo vya habari, hawa ni hatari kama ukoma.
 
kaka sio bahati mbaya ni makusudi, wanajua wanacho maanisha Watanzania wengi wana amini hili, Mimi na kuomba kama mzee wa Kijijini embuwaletee humu bei na aina ya mitambo, pia uwezo wake na UPATIKANAJI wake ili WATANZANIA wajue kuwa huu ni uongo!

Unaweza kupitia ripoti ya Mwakyembe au hata kuwacheki GE, Yamaha na wengine watengenezaji.
 
hivi kwanini uyu bwana mdogo na genge lake la waliomtuma wanatudharau sana watz???
ivi suala la umeme ni la kulipigia porojo km hivi?
ivi wanatuona wote ni wajinga mbumbumbu na hatuna wataalam wenye kutoa suluhisho?
ivi kwanini wanaleta utani na siasa za k.i.s.e.n.g.. namna hii?
mgao upo palepale na makali yapo palepale hata silioni la uyu dogo kwenda apo kwa mafisadi wezie na kuuza sura na kuleta mizaha,how I wish atokee kichaa mmoja ivi achape watu risasi!!
ila ipo siku walahi watajibu ili kwa wanainchi,saddam,hosni,gadhaf,mussolin,adolph et al wako wapi now!!

wamezidi kunichefua zaidi


Sent from my TECNO KD6 using JamiiForums mobile app
 
Msikilize tu, mwishoni lazima atapigia kampeni serikali kununua mitambo CHAKAVU ya Dowans!
Yuko kikazi fulani zaidi huyu dogo!
Du!!! Hivi hii mitambo chakavu ya DOWANS bado ipo? Hakika mgao wa umeme ni wa kutengeneza kwa asilimia 100 ni suala la muda tu mtaelewa.
 
Anasema miaka 10 iliyopita serikali iliamua TANESCO ibinafsishwe; anatoa historia ya mgao; walipokuja NETGROUP solutions kuendesha TANESCO, walitumia maji mengi kuzalisha umeme.Hawakuwekeza kwenye chochote hasa miundombinu hivyo tatizo likaanza ukichanganya na uhaba wa mvua.

Walitumia jitihada kubwa kukusanya madeni kwa vile mkataba uliweka kipengere cha bonus .So walikazana sana kukusanya madeni kwa sababu ya motisha wa bonus. Mwaka 2006 SERIKALI IKARUDISHA TANESCO serikalini. Matatizo y aumeme kwa kiasi yanatokana na mambo mengi. Haijakuwepo big investment katika uzalishaji hata ugavi.

Pia anasema kuwa umeme mwingi unapotea njiani kutokana na uchakavu wa miundo mbinumore than 20% ya 1100MW inayozalishwa. Anasema umeme unapotea mathalani, ni mwingi kuliko ule unaozalishwa na Songas!

Anaelezea matatizo ya umeme:

a. Kiwanda cha MBolea kufungwa mara tatu
b. Vodacom wanatumia fedha nyingi
c. Viwanda vidogo


Anasema wananchi wanalalamika na kuwauliza kama "wana akili" kwamba watu wanawashangaa iweje iwepo mitambo ipo imezimwa. Anasema yapo mapendekezo 30 la kuwasha mitambo ya Dowans ni moja tu.

Ameulizwa swali "kwanini miaka mitano ya kwanza Serikali haikuwekeza kwenye uzalishaji wa umeme?" Jibu lake: "Swali unaloniuliza ndilo na mimi nauwaliza serikali" (akimaanisha barua yake kwa Ngeleja).

Anaelezea suala la Stielger's Gorge anasema tatizo limekuwa ni suala la mazingira ndio limechelewesha sana. Anasema lakini sasa hivi jambo hilo linazungumzika na kuwa wapo taasisi binafsi ambazo wako tayari kuwekeza (akigusia suala la RUBADA na Brazili). Kwa hiyo anasema ni suala la kulinda maslahi ya "mazingira" na yale ya wananchi.

Ameuliza kuhusu suala la Dowans na anakiri kuwa Mtambo haujawashwa na anakiri ni kwa sababu ya "unafuu uliopo sasa kwa sababu ya mvua" lakini anasema kuwa "ni unafuu wa muda". Anasema kwa sababu mabwawa yaliyojaa maji sasa hivi ni yale yanayotegemea maporomoko ya maji (water falls) lakini siyo yale mabwawa ya hifadhi (water reservoir) kama Mtera.

Anaunga mkono kubadilisha sheria ya manunuzi ya umma ambayo itaruhusu manunuzi ya vitu vilivyotumika. Anasema kwa mfano nchi kama za kwetu na mazingira yetu na ya kibiashara dunia ni vizuri kuruhusu manunuzi hayo. Anasema sheria lazima iwe "flexible". Anasema nchi kama za kwetu haziwezi kupata vitu vipya kila wakati na anatolea mfano wa ndege.

Ameulizwa "kuna emergency ya kununua ndege"? anasema hata barabara siyo emergency - wanacheka tu - kwani anaambiwa kuwa mambo mengine ni ya mipango ya muda mrefu. Anasema "udharura" mwingine ni wa kujitakia. Anadai kuwa ( naamini kwa makosa) kuwa huwezi kwenda kununua mtambo wa kuzalisha umeme MW100 ni lazima usubiri miaka miwili.

Anasema kuwa serikali inataka kukodisha mitambo ya Tanesco ya 260 na amewatumia ujumbe Tanesco kuwa ahadi yao isipotimizwa basi "watakamatana" na "kuulizana vizuri" huko Dodoma.


Ametoa wito kwa watu ambao wameathirika na uchakachuaji wa mafuta wafike ofisi za Bunge jijini Dar leo ambao wanakusanya maoni ya nini cha kufanya.
Miaka kumi baadaye
 
Back
Top Bottom