Janga la Obesity limepiga hodi Tanzania .

Spear

JF-Expert Member
Jun 21, 2008
507
28
Jamani!!! hii hali ya Obesity hapa Tanzania serekali yetu wanaliona na wanaelewa athari zake na harama zake?huhitaji

Rocket Science kuliona hilo.humjuwi nani mja mzito kati ya wananchi si wanaume si wanawake na wala sio watoto hali inatishia.
 
Hali ya obesity kwa watoto kwa kweli ni mbaya, hasa watoto wa mijini. Lakini pia kama taifa hatulioni hilo kama ni tatizo ili kuweza kuchukua initiatives. But siku si nyingi tunaweza kujikuta tupo busy kutibu magonjwa na madhara yatokanayo na obesity. So far in my strugle to write about obesity sijaona studies zozote zinazohusu obesity zilizofanyika Tanzania.
 
Unajua kuna ka-ushamba fulani ambako watu wengi tena wa kada zote yani wasomi na wasio wasomi wanakaamini kuwa kitambi au unene au kufuga minyama uzembe ni sign ya kuonyesha kuwa mambo yako ni safi,kinachoniudhi mimi zaidi ni mtu anapolisha mtoto(overfeed) ili iwe ni kiashirio kuwa mzazi mambo yake yamenyooka wakati anasahau kuwa anamsababishia madhara makubwa baadaye.
 
Hali ya obesity kwa watoto kwa kweli ni mbaya, hasa watoto wa mijini. Lakini pia kama taifa hatulioni hilo kama ni tatizo ili kuweza kuchukua initiatives. But siku si nyingi tunaweza kujikuta tupo busy kutibu magonjwa na madhara yatokanayo na obesity. So far in my strugle to write about obesity sijaona studies zozote zinazohusu obesity zilizofanyika Tanzania.
usivumishe! taifa lina njaa kama nini!!~
 
watoto wa mijini bwana, huko vijijini ni kweli underweight ni serious problem kuliko overweight but kwa mijini, overweight ndo tatizo kubwa.
mjini wapi? manzese? kijitonyama?, magomeni?, kunduchi mtongani?, kariakoo?, nenda MNH makuti kaone ule utapia mlo alafu utowe taarifa
 
Unajua watu bado wana zile perspective za zamani kuwa Wembamba kuassociate na ngoma!
No wonder case za BP kibao!
 
Mnaionea tu Serikali. Wewe mtu kuwa mnene kupita kiasi au kuwa na mitambi hujui madhara yake. Tena cha kushangaza hata madaktari wengine wana matatizo hayo
Unajuwa, madaktari ni watu wazuri sana, sema tatizo lao kubwa ni wamefundishwa 'kukariri' na si kuuliza 'kwanini'?. Kweli kama unaenda hospitalini halafu unamkuta anayetaka kukutibu naye anaumwa, haileti picha nzuri.

Kwa sasa watu wengi hawajuwi kuwa unene au uzito kupita kiasi ni magonjwa pia!!!, mbaya zaidi namna watu wanavyoelekezwa jinsi za kudhibiti hali hii haiendani na ukweli wa kisayansi.

Lakini nini hasa husababisha uzito na unene kupita kiasi?, bonyeza link hii ukajifunze namna rahisi za kudhibiti hali hiyo bila gharama yeyote: uzito na unene kupita kiasi | maajabu ya maji
 
Mkuu asante kwa hiyo link tena umehusika kuitengeneza. Mkuu nasema hivyo kwa sababu kuna madaktari nawajua ni wanene kupita kiasi na vitambi aisee mpaka mimi nisiye jua maana ya afya nawaonea huruma sana.
 
mmenipa moyo mi ninayeitwa mfupa na ngozi kisa sio mnene

diabetes melitus is common among the poor in rich countries and common among the rich in poor countries. OBESITY being the common risk factor. Hii ni kwa sababu kwenye nchi tajiri maskini ndio wanakula hovyo hovyo na vyakula vyao haviko balanced kwani kupata vyakula bora ni ghali. Huku kwetu matajiri ndio wanakula misosi ya hovyo wakijua ndio inayotakiwa kuliwa na wenye hela kumbe haiko balanced na maskini wanakula vyakula vya kawaida ambavyo kumsababishia unene ni ngumu.
 
mjini wapi? manzese? kijitonyama?, magomeni?, kunduchi mtongani?, kariakoo?, nenda MNH makuti kaone ule utapia mlo alafu utowe taarifa
Anachokisema Lukolo chaweza kuwa na kaukweli kidogo; kuna article nimeiona kuhusu obesity kwa watoto Tanzania ni kama inaonyesha kwamba mjini hali si nzuri sana. Labda jaribu kusoma hapa: Prevalence of Overweight and Obesity Among Primary School Children in Tanzania: Experiences from Kinondoni and Njombe Districts by Ayoub Kafyulilo, Fidelis Mafumiko :: SSRN
 
Ukiwa mnene Tanzania unaonekana mambo safi miaka nenda rudi. Angalieni viongozi wetu mitambi ilivyokuwa mikubwa? Alafu wakidondoka na kufa ghafla wanaanza kutafuta mchawi nani.

Muhimu ni serikali kuelimisha taifa kwa ujumla si watoto wala wazee. Njia nzuri yaku kuelimisha ni kupitia matangazo ya kwenye radioni, tv, na magazeti mara kwa mara. Unawaambia wananchi madhara yake na nini cha kufanya hili wasiwe wanene kupita kiasi na kupata magonjwa kama kisukari, na magonjwa ya moyo.

Kwa upande wa watoto sasa hivi kuwa wanene sana ukitoa kula vyakula vyenye mafuta mengi au mlo usio kua na mpangilio ni kutokana kutumia mda mwingi kwenye kucheza video game au internet. Zamani tulikua tuna piga mpira kila siku, kila mtaa tuna timu ya mpira, lakini siku hizi watoto,vijana wote wanakimbilia internet. Mda wa kufanya mazoezi hamna matokeo watu wananenepeana tu.

Muhimu kwa wazazi kujaribu kuwahimiza watoto wacheze michezo ya nje sio kukaa ndani tu na video game au internet .

Kwa watu wazima pia, tufanye mazoezi na tuangalie mda wa kula, aina ya chakula na kiwango cha chakula. Tabia ya kula mapocho pocho kibao alafu unaenda kuchapa usingizi hapo hapo sio vizuri. Vitambi vinatoka na kula chakula kingi sana wakati wa usiku na baada hapo mtu anaenda kulala. Matokeo yake wakati huu. Chakula kinasagwa kwa kasi ndogo sana na kingi kinaifadhiwa kama mafuta kwenye maeneo ya tumbo.

Tule milo midogo midogo kwa siku yenye mboga za majani, matunda, maji mengi, kuku, samaki, karanga. Wali na ugali tule kiwango kidogo pia na muhimu zaidi tufanye mazoezi japo nusu saa kwa siku, mara tano kwa wiki. Kutembea pia ni zoezi tosha kabisa.

Kila la kheri ndugu zangu.
 
Anachokisema Lukolo chaweza kuwa na kaukweli kidogo; kuna article nimeiona kuhusu obesity kwa watoto Tanzania ni kama inaonyesha kwamba mjini hali si nzuri sana. Labda jaribu kusoma hapa: Prevalence of Overweight and Obesity Among Primary School Children in Tanzania: Experiences from Kinondoni and Njombe Districts by Ayoub Kafyulilo, Fidelis Mafumiko :: SSRN
data alizoweka katika article hiyo sioni tofauti na magaezeti ya ulaya. na asilimia ALIYOWEKA PIA NI KUBWA. ila sawa kama kaona ni kweli. kuandika data lazima siku zote pia tuangalie population. kama anaongelea dar sawa, kama ni mikoa yote mijini data na za uongo.
 
Hili ni tatizo kubwa kwelikweli, wengi wetu tunaamini kuwa mtu akiwa na mwili mkubwa ndio ishara ya afya bora, wazazi wengi wanawalisha watoto wao vyakula vya mafuta na protini kwa wingi sana na kupotezea vyakula vya vitamini ambavyo ndio msaada mkubwa kwa mwili wa binadamu.......
 
Tatizo ni Ufisadi na income gap,ukifatilia hilo tatizo mnalosema la obesity lipo tanzania A,sie huku asubuh chai na mihogo miwil ya kukaanga,mchana wali kama ngumi na vimaharage na vinyama viwili,usiku dinner wali beans sina tunda,juice,maziwa hiyo obesity ntaitoa wapi? Hao wanaotuibia ndio wanapata vya kusaza,naamin mungu ameanza kutulipia kwa njia ya kuwapiga mikansa,mipresha,visukari n.k
 
another article by Dr Marina Njelekela....2004...obesity and other cardovascular risk factors....

Anachokisema Lukolo chaweza kuwa na kaukweli kidogo; kuna article nimeiona kuhusu obesity kwa watoto Tanzania ni kama inaonyesha kwamba mjini hali si nzuri sana. Labda jaribu kusoma hapa: Prevalence of Overweight and Obesity Among Primary School Children in Tanzania: Experiences from Kinondoni and Njombe Districts by Ayoub Kafyulilo, Fidelis Mafumiko :: SSRN
 
Wabongo wengi hawafikishi milo mitatu kwa siku...Obesity tena!?hainiingii akilini
 
Back
Top Bottom