JamiiForums yapongezwa Bungeni kwenye Bajeti Kuu ya Serikali. Maxence Melo apongezwa kwa Uzalendo wa Ushauri Kodi Biashara ya Mtandao

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,116
Mchango wa JamiiForums watambulika bungeni, Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba asema anaipongeza JamiiForums kwa kuweza kufanya uratibu wa mchakato wa mazungumzo yahusuyo mambo ya digitali.

Aidha amempongeza Maxence Melo Mkurugenzi wa JamiiForums kwa kuwakusanya Wadau wa kiditali ili waweze kujadili na Serikali kuhusu masuala mbalimbali ya kidigitali.


 
Mwigulu Nchemba, Dr! Ubarikiwe sana. Sasa ni wakati wetu wa kutembea vifua mbere kama kuku walio nyonyolewa.

Nitakutafuta PM ili nije kukutembelea hapo bungeni. Tafadhali sana unipokee! Na ikiwezekana unikabidhi kwa Mjeshimiwa yoyote yule wa Viti maalum, ili kunionesha mazingira ya hapo mjengoni! Najua wewe utakuwana majukumu mengi ya kazi.
 
Big Big Big Up Maxence Mello!

Ukisikia uzalendo wa kweli kwa nchi yako, ni hiki kitendo alichokifanya Maxence Mello kushauri kuhusu kodi kwenye biashara ya mtandao, Jamii Forums imepongezwa Bungeni.

This is a big big thing!.

Maxence Mello ametajwa kwa jina na kupongezwa in person ni jambo kubwa Sana.

Nashauri sisi wana jf, kwa umoja wetu, tufanye maandamano ya mtandaoni kumpongeza Max.

What does pongezi hizi means Kwa Jamiiforums?.
Hii ya leo ndio the biggest recognition JF imewahi kupata, kupongezwa Bungeni, kwa something positive.

Sasa baada ya pongezi hizi, tutegemee sasa tutawaona wana jf hawa waliipotea, wakirejea na wakichangia tena kwenye mijadala mbalimbali humu jamvini
hawa ni baadhi yao
  1. Mwigulu Nchemba
  2. Anna Tibaijuka
  3. Nape Nnauye
  4. Zitto Kabwe
  5. Paul Makonda
  6. Kagasheki
  7. Freeman A. Mbowe
  8. John Mnyika
  9. Bernard Membe ,
  10. Tundu Lissu,
  11. Anthony Mtaka
Big up sana Max
Big up Jf
Paskali
 
Katika hotuba yake ya bajeti, leo hii 14/06/2022, Waziri wa Milango na Fedha, ndg Mwigulu Nchemba leo amempongeza kwa jina , Maxence Mello kwa kazi nzuri ya kuwaunbanisha wana mitandao na kukubaliana kiutaratibu na serikali.

Huku ni kutambuliwa kwa m tandao wetu pendwa wa Jamiiforums.

Hongera sana Max kwa kazi yako ya kujitolea kwa ajili ya free speech kwa muda mrefu na hatimaye serikali kuikubali mitandao na kuipongeza.
 
Back
Top Bottom