kichakaa man
JF-Expert Member
- Oct 20, 2011
- 5,479
- 5,070
Kwanza nianze kwa kusema mungu awabariki waanzilishi wa huu mtandao kwa kweli mmesadia watu wengi na wachangiaji wake wote kuna solidarity moja humu ya kipekee sana
Nimeamua Leo kutoa Ushuhuda kuhusu jinsi mtandao huu umenisadia sana kufanya mapinduzi ya kimaisha (hata kama sio makubwa sana)
Nakumbuka baada ya kuhitimu chuo kikuu 2014 nilipata kigugumiz fulani hasa nitaishi vipi hapa mjini kwa kuangalia sikuwa kazi na upatikanaji wa kazi kama mnavyojua hali ilivyo sasa na pia sikuwa na mtaji wala nini na hapa Dar sina cha ndugu wala nini, nikiwa mwenye mawazo mazito hasa baada ya kusumbuliwa sana kodi ya chumba na mwenye nyumba huku nikiwa sina hata 5 mbovu , siku hiyo nikaamua kulog in jf angalau nijiliwaze tu maana nilikuwa sio active sana kwa sababu ya masomo kunitinga muda mwingi japo nimejiunga JamiiForums tokea 2011.
Nakumbuka nilikutana uzi fulani kuhusu mambo ya ujasiriamali vile UNAWEZA mbinu za mawazo kutoka kuwa wazo hadi kuwa pesa, nilijifunza vingi siku na nakumbuka nilipitia kuhusu mambo ya matatizo ya mapenz na mahusiano .
Kiutani utani nikaanzisha mada fulani nakumbuka ilikuwa ni facebook nikasema acha leo nitumie ujuz wangu wa jandoni kutoa elimu ya mahusiano na kuboresha ndoa za watu. Nikaweka ada ya 2000 tu huwezi amini nilipata watu kama 80 hivi kwa siku ile mungu wa ajabu sana nikafundisha kama wiki wastani nilikuwa sikosi watu 50 kwa siku, nakumbuka nililipa kodi ya chumba na mengine kibao na kupata ka mtaji ka kufanyia mambo yangu japo baadaye nilihamishia mada zangu Instagram.
Kwanini nimeamua kusema hivi hapa jf ni kisima cha maarifa na mbinu zote ni vile ukiwa serious kuchukua mawazo ya watu hasa yale yenye kujenga na ukawa na akili ya kujiongeza kidogo utafanikiwa tu hapa kuna kila aina ya ujuzi upo hata ukitaka kuwa mchawi wakubwa zangu wakina mshana jf na mzizimkavu wapo.
Wale wenzangu na mimi mnaokuwa na changamoto mbali mbali hebu msisite kutumia JamiiForums kama mkombozi wenu mtafanikiwa tu.
Asante