Elections 2010 James Mbatia apata shida kupiga kura Kawe

Kazi ipo huu mwaka. Kama wamechakachua hadi jina la Yakobo (James) Mbatia halionekani, basi kuna shida kubwa sana mahali.
 
kama mtu akithibitisha habari kwamba mbatia hakupiga kura nanua bia kusherekea kupotea kwa kura moja ya JK, wow!
 
Nafikiri hizi ndo zile namba ambazo zilikuwa zinaonekana kwenye daftari la wapiga kura na kwenye vituo. Nafikiri leo ndo zinafanya kazi yake. Wakamatwe hao wote
 
sasa Mbatia atashtaki Tume au ataendelea na kesi yake na CHADEMA? Na tumwulize alivyokuwa analalama kuwa CHADEMA wamemkiuka bila kumwachia jimbo, sasa kumbe hata hajajiandikisha na sii mpiga kura halali! aisee, jamaa ka-expire mno!
 
sasa Mbatia atashtaki Tume au ataendelea na kesi yake na CHADEMA? Na tumwulize alivyokuwa analalama kuwa CHADEMA wamemkiuka bila kumwachia jimbo, sasa kumbe hata hajajiandikisha na sii mpiga kura halali! aisee, jamaa ka-expire mno!
Hatimaye amefanikiwa kupiga kura baada ya kuwasiliana na NEC kwa kutumia jeuri ya kuwa mgombea, vinginevyo asingepiga kura kabisa!
 
Kuna kazi Kwa mbatia, atafanyaje! Ajiunge tu na CHADEMA kama akikubaliwa maana, hana chama tena.
 
hali hii inanihuzunisha sana na mimi ni mmoja wapo:sad:.Ila MUNGU yupo pamoja nasi tunategemea mema tu.
 
katika hali ya kushangaza, jina la mgombea ubunge jimbo la kawe kupitia nccr mageuzi, mh. James Mbatia hatapiga kura mpaka sasa kwa sababu jina lake halijaonekana kwenye orodha.

Kwa kweli NEC wamechemsha sana kwenye maandalizi ya uchaguzi. Pia mh. Mbatia amewaonesha waandishi wa habari kadi feki ya kupigia kura iliyo amatwa yenye jina bila picha ya mwenye kitambulisho.
Hiyo haitishi,enzi hizi za maendeleo ya uchapichaji kitu kama hicho ni rahisi kufanywa na watu wa kawaida,na wala NEC wasihusike
Bora kueleza yeye kaipataje?.Isije ikawa walalamishi wanatumia jina lake kutaka......

 
Kama Mbatia amezuiwa...hali inakuwaje hapa? Mtu mwingine si ndo itakula kwake!!
 
Nyota njema huonekana asb, huyo bwana si mtu makini. Kuongea kwa kufumba macho akionesha ukali kumbe naye ni maji kama yule mwenye mdahalo aliyekuwa na majibu lakini anajikanyaga kanyaga.

Mshikaji hata yeye hakujipigia!!!!!!! MAKUBWA!
 
tatizo linaloonekana hapa ni tume tuliyonayo! mbatia sio mlengwa. jina waweza liona siku mbili kabla lakini utashangazwa siku unakuja kupiga kura na wala mantiki haionekani mambo yangalikuwa kama ilivyopangwa awali daftari kutolewa mwezi mmoja kabla nafikiri tatizo lingepunguwa kama sio kuwepo kabisa!
 
Hatimae ameweza kupiga kura baada ya kuletewa makaratasi yake kutoka ofisi za Tume ya Uchaguzi.

Mbatia anasema ametumia nafasi yake kisiasa kuweza kuwasiliana na NEC moja kwa moja.

Bahati mbaya ni kwamba wengine hawana nafasi hiyo, utaratibu tunaoambiwa vituoni ni kwamba kama jina lako halionekani unatakiwa utume ujumbe wa simu NEC halafu usubiri kujibiwa kama unaweza kupiga kura.

Mbatia ametumia njia za mkato tunazojaribu kuzikataa katika jamii, influence peddling. Kiongozi gani huyu?
 
Usually Majina Yapo. Watu wanashindwa tu kufuatilia kwa Uzuri.

Kituo nilichopigia kura mimi wale makarani waongozaji bure kabisa, wamenilekeza milango zaidi ya minne na huko kote hakukuwa na jina langu. Nikawaambia, acheni ubabaishaji, nitajihudumia mwenyewe. nikapitia milango yote 15; pale kituoni nikisoma kila jina kwa kutrack kialphabet, baada ya milango tisa nikaona jina Mama mdogo, moyo ukatulia, nikapiga kura kuchagua rais, mbunge na diwani wangu! Ajabu yule msimamizi hata hakuniuliza kamna najua kusoma na kuandika, wala kunielekeza tick niweke chumba gani. Niliamua kukaa pale kuwasaidia wazee na wasiofahamu kusoma na kuandika wapatao kumi na watano, I repeat 15, kutambuwa wamepangwa kuingia chumba gani. Nimechukia sana kufanya kazi za hawa makarani waongozaji wakati wao wamekaa tu wanatumbua macho na kunywa soda! Ila nimefurahi nimetimiza wajibu wangu wa kiraia, na niliowasaidia, nilishia kuwaonyesha milango husika, sijaifluence kura zao. Rai yangu, tume ya uchaguzi naona hawajifunzi kutokana na makosa, kwani errors za 1995, 200 na 2005 zinajirudia leo 2010, hawakuwa wamejitayarisha kikamilifu, na sishangai Mbatia kuchakachuliwa, natumaini somo limemwingia kichwani kuwa ni muhimu kukagua kabla!
 
Mbatia hafai hata kidogo,niwazi kuwa hana umakini,kwani hata jina lake hukulihakiki,kweli wapinzani wanatafuta lakusema wakti Kikwete akitangazwa ushindi,mmh
 
Back
Top Bottom