Jamani wenzangu mnaishije na 'house girl' nyumbani?

flowerss

JF-Expert Member
Nov 25, 2017
640
590
Salamu nyoooote!

Ni matumaini yangu kwamba nyote my wazima wa afya njema.

Tuende moja kwa moja na mada husika.

Kwanza kabisa naomba nikili wazinya kuwa Hawa Wadada wa kazi wanaotusaidia kazi majumbani mwetu na kulea watoto Ni muhimu Sana Sana pengine kuliko wengi wetu tunavyodhani Na ukitaka kujua kuwa na Mtoto mdogo then unatakiwa kazini halafu huna Beki tatu Basi utajua hujui.

Lakini pamoja na umuhimu wao mkubwa Sana Kwetu na kutokana na experience toka kwa watu wengine pengine na Mimi binafsi huwa nachoka Sana kwa vituko vyao.

Mimi binafsi nimewahi au naishi na house gal kutokana na kazinnqkuwa na watoto jamani Kuna baadhi ukiwapata Ni waelewa kiasi lkn wengine Ni pasua kichwa.

Mfano Kuna mmoja niliwahi kumpata ndani ya siku mbili keshakuwa mwenyeji atafatisha mziki unaoimbwa toka kwenye tv kwa sauti kubwa hata Kama Kuna wageni.Ukimkanya Basi Ni kesho tu atarudia.Vituko juu ya vituko atachukua simu yako chumbani na kwenda kujiSelfie bila hata kuomba.Ukitoka kidogo atakunywa maziwa ya mtoto na vyakula vya mtoto wkt anapika mwenyewe vya watu wazima.

Mara atalala Sebuleni mapaja wazi wkt chumbani kwao kupo mpaka baba wa Nyumba amfukuzie chumbani jamaniiii.. Mwingine Sasa hivi wanasimu zao Ni kuchat muda wote mpaka anaunguza mboga na Gesi haikai.
Mara atakwambia nimetoka mkoani tunalima kweli haya saidia weekend bustani.Nikakuta kang'oa mboga zote mchicha majani ya kunde na maboga eti alidhani magugu huyu ndo katoka shamba.Mwingine ukimuambia hii nyumba usifanye vitu visivyotakiwa kumefungwa Camera Basi kesho yake atasema naomba nirudi Kwetu nyumba ya Camera haiwezi.

Mara Nyumbani mama baba wanaumwa tuma pesa ya matibabu kumbuka pesa yake unampa Sasa usipompa ya kutibia wazazi wazazi watapiga simu Basi mtoto arudi aje kusaidia kazi. Yaani mwingine unamuambia kitambaa Cha kufutia vyombo Kama unaosha tumia kibeseni tu Cha vyombo Mana so kinatumika kwenye vyombo.Kesho anafulia soksi kwenye beseni akisema mbona Jana tulifulia Taulo la vyombo kwenye kibeseni Yaani hata kureason hakuna na hapo eti amemaliza form 4.Vituko Ni vingi hata Kuna majirani zangu wameamua kuachana na habari za Housegirl maana Ni vituko kwa kwenda mbele Ni mengi na yanachosha na wanasahau Sana hata Kama unamsaidia kazi ukitoka kazini utakuta anashinda kuangalia Tamthilia hata wkt mwingine mtoto hata kumtoa pampasi Hakuna.

Jamani akina Baba mnavyodai sisi wamama tuna midomo au tunawanyanyasa mahousegal ebu na Nyie angalieni Kuna wangu alikuwa likizo ya mwezi mbona ALISEMA huyu msichana wako utakuta nimemchapa mbona yupo hivyo ukimwita akiwa chumbani Kama ameacha mboga kwenye Gesi mpaka vinaungua ukimtuma Dukani harudi mapema.Ila yote kwa yote Kuna kipindi unaweza bahatika akawa mzuri au majanga Kama hayo.

Je, wewe Nyumbani Housegirl wako ninwa Dizaini gani au Unaishije Naye ili wengine tupate kujifunza na tuweze kuishi nao kwa muda mrefu?
 
"Mashikolo mageni"

wengi wao ndio yanawasumbua. Ukiwavumilia na kuwafundisha wanaelewa japo ni taratibu mno.

usipanic jifunze kwanza kuvumilia mapungufu ya wengine.

Mfanye rafiki na mtoto wako. Ajihisi ni mmoja ya mwanafamilia, Usiishi na hausi gel ndani kama mtu tu baki. Mtreat vzur amini nakwambia.
Wafundishe pia watoto wako kumuheshimu bila kujali ana kasoro gani. Mtu akidharauliwa hupata inferior complex anazidi kupoteza kujiamini na hiyo ni mbaya zaidi.
 
Housegirls ni kubahatisha tu....kama tulivyo sisi na mapungufu yetu na wao ni hivyo pia. Na wengine inaongezeka mazingira mapya, vitu vya kutumia kama vya usafi, kutumia bafu na vyoo, majiko haya ya kisasa inakuwa vitu vipya kwao. ni kuwafundisha taratibu na Kwa subra.

Kuna wale ambao hawafundishiki, unaondoa na inabadili Hadi upate mwenye afadhali. Hakuna aliyekamilika
 
Back
Top Bottom