Jamani tumekufa!!!!!!

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,171
3,346
Serikali kupitia EWURA imeridhia ongezeko la 18% ya bei ya umeme kuanzia January mwakani. Hilo ni pigo kwa mtumiaji na tayari ongezeko hili litakuwa na athari katika uchumi wetu. Wahanga wakubwa ni watumiaji wa majumbani ambao wenyewe hawana wa kumtwisha zigo hilo mtu yoyote tofauti na viwanda ambavyo vinaweza kufidia kwa kupandisha bei ya bidhaa zake.
WanaJF mnalionaje hili?

Source. TBC1
 
Serikali kupitia EWURA imeridhia ongezeko la 18% ya bei ya umeme kuanzia January mwakani. Hilo ni pigo kwa mtumiaji na tayari ongezeko hili litakuwa na athari katika uchumi wetu. Wahanga wakubwa ni watumiaji wa majumbani ambao wenyewe hawana wa kumtwisha zigo hilo mtu yoyote tofauti na viwanda ambavyo vinaweza kufidia kwa kupandisha bei ya bidhaa zake.
WanaJF mnalionaje hili?

Source. TBC1

Si wanasema tumeridhika kukaa na rais Mwizi.
 
Sasa washaanza utumbo hii nchi ni ya kifala sana tuna gesi,makaa ya mawe,uranium,mafuta maporoko kibao ya maji'lakini jk kazi kuharibu dada zetu huyu rais wa ikulu sijui mpaka 2015 sukari elfu 3,bia elfu 3,soda buku,maji yatapanda,mkata mpaka 3000.endeleeni kusema ccm na mungu atawalaani
 
Kumbe jamani wafanyakazi wa tanesco wananunua umeme kwa bei yao ya chini sana jee hapo watamuonea huruma mwananchi?wana uchumi hivi wafanyakazi wa voda,airtel au tigo wawe na bei yao pekee ya vocha jee tra watapelekaje hesabu zenye uhalisia wa kodi?nchi imeliwa vya kutosha jamani
 
Eh MASKINI WATANZANIA, HIRI NI RIKASHESHE!, haka kajamaa kanakoitwa EWURA nako kanafurahia hii ongezeko kwa sababu kale kapercentage kanakopata kataongezeka hata kwao.
 
Take a breath and drink some water bro! The headline error is too scary..hope you mean umeme!
 
Ndio mambo ya kidumu chama cha mapinduzi maana ndio sera ya kuleta maisha bora kwa kila mtz kwa kasi zaidi,ari zaidi na nguvu zaidi.
 
HIVI TANZANIA KUNA SIKU TUTASIKIA HUDUMA AU BIDHAA FULANI IMESHUKA BEI?KENYA KUPANDA NA KUSHUKA HUFANYIKA KUZINGATIA HALI HALISI!HAPA BONGO INAPANDA TUU MWAKA 2005 dumu la mafuta ya kula lilikua sh 18000 leo sh 50 000 wala hakuna anayejali wala kuandamana na hali hii
 
Tena cha kushangaza zaidi umeme sasa hivi kwa mtanzania si huduma kwa jamii tena bali ni anasa kwa mwenye kuweza na mwenye kushindwa aache. Kuvuta umeme nyumbani shilingi laki 5 hakuna nguzo hakuna nini waya 2 tu kuunga kwenye mita laki 5 kuna nini cha gharama hiyo hapo?
 
Back
Top Bottom