Jamani sijielewielewi juu ya my super handsome boss!!! Ushuri please!!!

lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,700
29,111
Nawasalimu wakuu!

Ya jana yamepita jamani nimenusurika BAN, namshukuru mola, ila sijakata tamaa, najua MM the F ana play HARD TO GET, na mimi I HAVE ALL THE TIME TO WAIT, sieti hata nyie wakiume mkimtongoza mtu mara ya kwanza mnajua tu cha mbavu na za uso lazima ila hamkati tamaa? Na mimi nakomaa, mpaka ani PM.

Back to the point, mwenzenu nakofanyia kazi huku kuna Bosi wangu Super Handsome!!!!! afu hajaoa wala hana demu mule ofisini ila mapoziii mengi na hivi karudi kutoka masters U.K kujifanya high class wkt za chini ya kapeti zinadai alikuwa mbeba boxi tu huko majuu cheti kachakachua. Full kuninyanyasa na hiki kielimu changu cha kuungaunga cha UDSM, Sinywi maji! sijambi kwa raha! kabla sijaambiwa YOU HAVENT SEEN THE WORLD! nakuwaje mdogo na hivi hata nairobi sijawahi kufika??

Nilivomuona mara ya kwanza kwenye interview badala ya kuwaza jinsi ya kupata hiyo kazi nijikwamue na njaa kali ya kitaa nikawa nimepagawa mtoto, miswali migumu siiwezi nabaki kumpa killer smile tu! akawa haelewi huyu binti 0 kichwani ansmile nini badala ya kutiririsha utirio, out of kindness tu akawa ansmile back. Hamad kazi nikapewa mie nikaanza na mshawasha kweli!. Nikajua tu hapa hii kazi ushahidi tu kanileta tuburudike amasivyo wale intervieew wengine vilaza zaidi yangu.

Wiki ya kwanza tu baada ya kupewa mishushu na makavu livee oblongata ikatulia sasa nikajua tu hamna kuburudika wala nini mwendo wa kazi tuuu! Ila uvunguni mwa moyo wangu bado ule mshawasha ukabakia ila kila nikipewa shushu unapungua mpaka ukaisha kabisaa. Nikajiaminisha vita nimevishinda na pepo la ngono zembe limeshindwa na limelegea.

Sasa si ndo Boss Super Handsome akaniambia nanifeel na tudate kama i feel him too ( tongoza za deportees hizo hawabembelezi sanaaa) Nikakumbuka mishushu na I HAVENT SEEN THE WORLD nikaona ligi nzito, maji ya shingo siyawezi nikamchomolea. Nikamwambia simfeel wala nini achukue time. Basi nshomile hakunibembeleza wala nini ila akaniomba nisvujishe ishu ofisini kuwa nimempa cha mbavu. Nikamwambia usihofu.


Sasa nimezoea ofisi na nimeanza kupata miumbea ya mule kumbe 90% ya vidada mule vinamzimia kinoma, kila siku kumnunulia chakula, si kumpa lift, si kumualika drinks jioni nae anakula tu vyote, hana hiana! mi huu umbea umeniuma kinomaaa! sijui kwanini wakati kumpenda simpendi, wivu sina ila roho yaniuma! Basi kila nikiwaona wapinzani wanagombea jimbo roho yanitoka! Nimebaki nataka huku sitaki.

KITAALAMU HIVI NINA SUMBULIWA NA NINI? NINI TIBA?

Babu asprini nipe uzoefu wako inaonekana umekula chumvi nyingi umeona mengi!!!!
 
napenda mwandiko wako,unavyojieleza!unajua nakusoma u mtu wa aina gani?
A FREELANDER
unajitambua unataka nini na yu go for it
unajiamini sana
unaamini katika kujitafutia furaha
unaamini katika upekee wako na ur proud of what u are
huangalii mtu mwingine anajisikia nini mradi wewe unafuraha!
 
kumbe ndio habari za ofisini kwetu unazileta huku...makubwa
 
napenda mwandiko wako,unavyojieleza!unajua nakusoma u mtu wa aina gani?
A FREELANDER
unajitambua unataka nini na yu go for it
unajiamini sana
unaamini katika kujitafutia furaha
unaamini katika upekee wako na ur proud of what u are
huangalii mtu mwingine anajisikia nini mradi wewe unafuraha!

maisha mafupi haya jamani! Hili jamvi la kupunguzia stress kitu huwezi kumwambia mtu unaemjua bt huku unakisema black n white na unapata picha ungeomba ushauri phisically ingekuwaje!
 
  • Thanks
Reactions: b2k
Kwani wewe ndo uliemuangukia Maxence Melo pia? Sorry, I rarely remember these kinds of IDs. Manake huenda una pepo la maimuna.
 
Back
Top Bottom