Jamani nipo Dar, mbona hatutafutani?

Zinduna

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
2,378
3,379
Niko Jijini Dar, tangu juzi, nimekuja kula Krismas, lakini jana nikajisikia vibaya kwani mwili ulikuwa unani-Washawasha. Nikajisemea moyoni, balaa gani hili yarabila-alamina! Nkaona nende kwa Dr. Riwa ili kupata matibabu. Kufika pale akanpima akanambia nina hitilafu kwenye Kongosho kutokana na kuugua Malaria Sugu hivyo akaniandikia Klorokwini. Nikawasiliana na Da' RussianRoulette kumweleza hali yangu, na yeye akawajuza wana JF.

Watu wa kwanza kuja kuniona walikuwa Dena Amsi na Da' AshaDii, walikuwa amenibebea uji lakini ulikuwa na ma-Bujibuji, hata sikuupenda, Pia walinipa salaam kutoka kwa Da' FaizaFoxy. Mara ghafla akaja shoga angu Mwali, akanambia Nyumba Kubwa ninayoishi itakuwa na Mbu wengi sana na akanionya niache Mcharuko nitumie Chandarua chenye kutiwa dawa. Hata hivyo alikuwa amenibebea Chauro ili nitulize njaa, Nili-Smile kwa furaha wakati napokea zawadi zile.

Lakini pia wapo walionitumia salaam za pole kupitia simu yangu ya BalckBerry, mfano Shostito Cantalisa ambaye alikuwa pamoja na Bebii walinitumia salaama wakinitaka ni-Badili Tabia na kuwa Mwanajamiione wa kutunza mazingira ili kuepuka maradhi, walinishauri niwasiliane na The Boss mshauri wa mazingira na afya kwa ajili ya kupata msaada wa kitaalamu juu ya utunzaji wa mazingira na uangamizaji wa mazalia ya Mbu. Nilipowasiliana na The Boss aliniambia yuko kikazi Mkoani Katavi na akaniahidi kumtuma Rejao ambaye yuko Moshi kwenye matambiko atakapo rudi awasiliane na mimi.

Daudi Mchambuzi hakubaki nyuma alinitumia salaam akinitaka niwasiliane na Saint Ivuga au Mti Mkavu kwani wao ni wataalamu wa tiba mbadala, kwani wanaweza kunipa ushauri. MAMMAMIA naye hakubaki nyuma alikuja kuniona na alikuwa na kadi za Get Well Soon kutoka kwa Sabry001, Da' Lizzy, Da'Aminata9 na Preta.

Napenda kuwashukuru wote mlioguswa na longo longo yangu na ningependa kuwatakia Sikukuu njema ya Krismas na Mwaka Mpya……………………………..

Wenu katika ujenzi wa JF

Zinduna
 
Leo ni Siku ya Kutoa na Kuwatembelea Wahanga wa Mafuriko Wakaribishwa Au na wewe unataka Media kama Clouds
 
he he he, pole zinduna
mie niko hapa ubungo ndo nakatisha tiketi za magari
ndo utajua umuhimu wa Kongosho si huwa mnampotezea mnajali moyo na maini
 
vipi mwili bado una WASHAWASHA? bila shaka utakuwa umepandwa na DUDUWASHA. Ikishindikana tafuta MZIZI MKAVU WA MWAROBAINI uchemshe unywe. kama haujameza vidonge hamna tabu unaweza ukanywa TUSKER BARIDIII hata tatu labda ukute mwili umekosa bia. lakini wakati unakunywa hakikisha unakaa INVISIBLE place ili RIWA asiseme umemdharau. hakikisha haunywi pombe za MPITA NJIA usiye mjua coz anaweza kukufanyizia. umeugulia ugenini je umetoa taarifa kwa FIRSTLADY wako? kweli unaumwa unaonekana MPOLEEEE. Mia
 
Eti hii nayo thread? Mtu anataja ID zake ili iweje hasa?

Mwita bana......
wakati mwingine tunahitaji kuondoa stress na kufurahi.....
hata kama ID zote zake....si wakati wake huu.....

Njoo mwaya Zinduna tule makange.....nipo hapa Rose Garden nazimua vya jana.....

 
Zinduna umenikumbusha hatua za ukuaji wa Bongo Fleva. Ubunifu ulipoanza kuwa kigezo muhimu kwa msanii kushine, JMo akaja na "Kama Unataka Demu" wakati huohuo na Misosi akatoka na "Nitoke Vipi". Wote wawili walichokiimba katika hizo nyimbo zao ilikuwa ni kutaja majina. Jambo hili lilimkera sana Mfalme wa Rhymes Suleiman Msindi aka Afande Sele na kuamua kuwadiss kwa kutatataja tu majina katika nyimbo bila kuzingatia vina na ujumbe. Heko maana wewe japo hukumtaja Mwita25 wala Pakajimmy ila vigezo umevizingatia.
 
Waaoooh!
Nipo mtaa wa 4 kama kawa!
Mbona ukapotea sana?...hivi umekuta missd kolz zangu ngapi kwenye cm yako?

Ongea taratibu tusichakachue mada ya huyu mdada!

eeeeh bwana mafindofindo yamenikaba koo hata huwezi ongea na cm....
imekwendaje upande wako
itabidi tutafutane kwa mama Neema aise
 
Mwita bana......
wakati mwingine tunahitaji kuondoa stress na kufurahi.....
hata kama ID zote zake....si wakati wake huu.....

Njoo mwaya Zinduna tule makange.....nipo hapa Rose Garden nazimua vya jana.....

Habari za siku Bi Dada, Umepotea kama mayai ya Chaza!
Ningekuja kuungana na wewe lakini Dr. Riwa kanionya nisinywe Tende, Je kuna Madafu au Togwa huko................
 
Zinduna umenikumbusha hatua za ukuaji wa Bongo Fleva. Ubunifu ulipoanza kuwa kigezo muhimu kwa msanii kushine, JMo akaja na "Kama Unataka Demu" wakati huohuo na Misosi akatoka na "Nitoke Vipi". Wote wawili walichokiimba katika hizo nyimbo zao ilikuwa ni kutaja majina. Jambo hili lilimkera sana Mfalme wa Rhymes Suleiman Msindi aka Afande Sele na kuamua kuwadiss kwa kutatataja tu majina katika nyimbo bila kuzingatia vina na ujumbe. Heko maana wewe japo hukumtaja Mwita25 wala Pakajimmy ila vigezo umevizingatia.

Nilijaribu kuwataja lakini majina yao yakaharibu vina, nilijua tu Mwita25 atamaindi, maana hana dogo!
Mwanaume mlalamishi kaa nini sijui.............. Ghubu tu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom