Jamani nikaribie?

Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
May 15, 2009
7,323
6,810
Jamani ndani hodini, hamjambo afya zenu
Najiingiza kundini, naomba karibu zenu
Nijipenyeze pembeni, niweze kuwa wakwenu
Mzizi wa Mbuyu laivu, jamiini naingia

Wakuu wa tafakuri, nipeni japo nafasi
Njimwaye na kufikiri, Bongo nilitie chansi
Nizunguke ka tairi, mtandao si nanasi
Mzizi wa Mbuyu laivu, jamiini naingia
 
Ukaribie mara ngapi, mbona tayari uko ndani
Afya zetu maridhawa, tunamshukuru maanani
Karibu sana jamvini, jisikie uko nyumbani
 
Asante mkurugenzi Babu Ataka Kusema, tuko pamoja. Ila naona wengine ushairi umewapiga kachenga, "but I thank you all in this house" nimefurahi sana kuwa ndugu yenu naamini sitawaangusha.
 
Ukaribie mara ngapi, mbona tayari uko ndani
Afya zetu maridhawa, tunamshukuru maanani
Karibu sana jamvini, jisikie uko nyumbani

Umefanya vema kumkaribisha,lakini unaposema ajisikie yuko nyumbani, napaka wasiwasi kwa sababu hatujui nyumbani kwake kukoje. Je kama nyumbani kwake anapigwa ina maana na hapa atapigwa?

Karibu sana.
 
Karibia on your own risk na make sure umesoma sheria za JF vizuri, siyo baada ya post 10 unaaga nakudai kwamba umefanyiwa ndivyo sivyo...

Ushauri wangu:- JF ni jumba ambalo shilingi ina pande zaidi ya mbili.
 
Asanteni tena, ila wengine wanapenda utani sana humu ndani kama huyu Malila, sipigwi nyumbani chifu, naitwa baba. Mambo jambo, na mzee wa "ka-chawa kanakozunguka nimewapata.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom