Mchaga wa ukwel
Member
- Jul 16, 2011
- 26
- 1
Siku 2 zimeisha tangu nikiwaza umuhimu wa umeme na mafuta ya taa kwa walio wengi. Najua atakaepinga kuwa mafuta ya taa ni zaid atakuwa mwenda wazimu,au amezaliwa gorofani na kukulia forodhani. Kwa mwanakijiji yeyote anaejua historia yake na hali yake kiuchumi,mafuta ya taa ni msaada mkubwa kwake as long as hana uwezo wa kujipatia umeme.na afteral watanzania weng ni maskini. Sasa najiuliza iweje wabunge wapitishe mafuta kupanda bei na wakat umeme unaotumika na asilia ndogo ya watanzania vijijini bajeti yake ikataliwe? Kwanin wasingekataa na ile ya mafuta? Ni kweli wanatuwakilisha walala hoi? Kipato cha kabwela ni dola ngapi? Wabunge wanatumia akili kweli au matope? Tuwaeleweje? Au wanafuata mkumbo,mtu fulan akikataa basi nawenyewe wanafuata? Kwanin mawazo ya wapinzani yanaonekana si lolote ilihali wana ccm hata wakitoa mawazo mgando wanasikilizwa? Ni mara ngapi wapinzani wanatetea wanyonge sauti zao zinazimwa na NDIO ZA CCM? Naombeni mchango wenu wakereketwa!!