Jamani Housegirl wangu Huyu, Ananitafuta ubaya! (STRICTLY KWA WANAUME TU)

Gugwe

Senior Member
Jul 25, 2011
122
54
Jamani naomba ushauri kuhusu hili.

Mimi ni mume wa mke mmoja na watoto wanne. Hivi karibuni tumepata housegirl mpya kutoka Singida, amemaliza form four hakubahatika kuendelea na masomo kwa sababu ya kukosa sifa za shule za serikali. Ni mzuri wa kawaida, yaani hana muonekano ule wa mahousegirl-naamaanisha muonekano choka mbaya kweli anafaa hata kuwa mke wa mtu. Katika historia yangu sijawahi hata siku moja kutembea na housegirl na mpaka sasa nishaajiri hao h/girl si chini ya 6, huwa niko very serious na sitaki mazoea nao hata kidogo.

Huyu amekuja naona anataka kuniangusha katika msimamo wangu huu. siku ya kwanza kutambulishwa kwake alionekana kushituka sana ingawa na mimi kwa ndani nilimkubali kuwa mzuri. Maisha yakaendelea na siku zikafunguka. Sasa toka siku hiyo amekuwa anakosa sana sana tu confidence ninapokuwa nyumbani, mara atajikwaa, mara ataogopa kuja mbele yangu n.k mbaya zaidi ninapokuwa peke yangu lets say wengine wapo mbali ananichangamkia sana na kutabasamu muda wote kila nitakalooongee yeye anatabasamu hata kama si la kufurahisha, nikimtuma kitu ataniletea wakati napokea anainua kichwa kuniangalia kiuchokozi halafu anatabasamu, basi na mimi nikawa natabasamu. Ikitokea labda nimerudi nyumbani na nahitaji chakula mapema atanipikia vizuri sana wakati mwingine anongeza kitu ambacho hakikupangwa kwenye ratiba ya chakula cha siku hiyo, anaweza kunkaangia mayai au akachemsha chai ya maziwa akaweka na viuongo haraka haraka na kunipatia chakula.

Tatizo, wife keshamshitukia hizo nyendo zake, amekuwa kila mara ananiuliza kuhusu mtu huyu, anasema mbona fulani ukiwepo anakuwa hana confidence nikamwambia mi sijui embu muulize alipomuuliza akamjibu wife kuwa eti ananiogopa kwa sababu aliambiwa na mlinzi mi ni mkali sana achunge asinikorofishe. Lakini ukiangalia mapozi yake kwangu si ya mtu anayemuogopa. Si hizi ameongeza zaidi, kunisalimia/kuniamkia kwake imekuwa ngumu sana ni mara mojax2 sana. Mi kwa ujumla ni mtu nisiyejali vitu vidogo vidogo na nilichojaribu kufanya ni kuwa mbali nae, nimeongeza kuwa serious, na wakatui mwingine nakuwa mkali ninapoongea nae ili awe mbali nami au afute hicho anachofikiri au kukitafuta, Lakini nahisi ananitafuta ubayaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!

Nimfanyeje? au nifenye lakini nahisi kujidhalilisha kwa mah/girl!
 
Mkuu okoa ndoa yako na maisha ya watoto wako wanne. Kumbuka kwamba kosa moja tuu ni noma kwako na kw afamilia yako. Ikimbie zinaa na muombe sana Mungu akuongoze na aondoe huyo shetani ambaye unataka umkaribishe ndani ya kichwa chako ambaye ni tamaa ya kumtamani huyo dada
 
shinda tamaa mkuu...fikiria mke wako na wanao.
umenitisha namna ulivyoandika kwani ni kama wasubiri mazingira yaruhusu umalize kesi.
ukitumbukia kwenye hilo shimo yatakayofuata ni makubwa.
 
Mkuu kwa kweli the way story yako ilivyo ni kuwa wewe ushaona opportunity unasubiri upate chance ya kumaliza jambo. Kama una nia yaepike sana hayo na wala usijaribu hata kidogo kuvuta au kuvutia hali hiyo itokee. Mara nyingi usiruhusu kuwa wawili peke yenu nyumbani bila wanafamilia wengine kuwepo na wala usiruhusu ule ukaribu wake ukuingie. Epuka kujadiliana nae maana hapo ukimpa chance mkuu imekula kwako
 
shinda tamaa mkuu...fikiria mke wako na wanao.
umenitisha namna ulivyoandika kwani ni kama wasubiri mazingira yaruhusu umalize kesi.
ukitumbukia kwenye hilo shimo yatakayofuata ni makubwa.

Thanks mkuu nitajaribu
 
Jamani naomba ushauri kuhusu hili.

Mimi ni mume wa mke mmoja na watoto wanne. Hivi karibuni tumepata housegirl mpya kutoka Singida, amemaliza form four hakubahatika kuendelea na masomo kwa sababu ya kukosa sifa za shule za serikali. Ni mzuri wa kawaida, yaani hana muonekano ule wa mahousegirl-naamaanisha muonekano choka mbaya kweli anafaa hata kuwa mke wa mtu.

mmmh...
Katika historia yangu sijawahi hata siku moja kutembea na housegirl na mpaka sasa nishaajiri hao h/girl si chini ya 6, lakini

Huyu amekuja naona anataka kuniangusha katika msimamo wangu huu. siku ya kwanza kutambulishwa kwake alionekana kushituka sana ingawa na mimi kwa ndani nilimkubali kuwa mzuri.!

kumbe ushamtamani tayari.....

Tatizo, wife keshamshitukia hizo nyendo zake,

Kama wife kamshtukia kwanini useme ni tatizo...? we unataka kumla...

Nimfanyeje? au nifanye lakini nahisi kujidhalilisha kwa mah/girl!

we kuna kauzinzi kako ndani yako tena nahisi ushafanya sema unatafuta watu wa kukutia moyo pumbaaaaaaaaaaaaaaaav.... heshimu nyumba yako kama baba, otherwise furaha ya nyumba yako itapotea na itaku-cost kuitafuta


 
mmmh...


kumbe ushamtamani tayari.....



Kama wife kamshtukia kwanini useme ni tatizo...? we unataka kumla...



we kuna kauzinzi kako ndani yako tena
nahisi ushafanya sema unatafuta watu wa kukutia moyo pumbaaaaaaaaaaaaaaaav.... heshimu nyumba yako kama baba, otherwise furaha ya nyumba yako itapotea na itaku-cost kuitafuta


Sijafanya bado ila mambo yanavyokwenda nona umuhimu wa kuweka mikakati ya kutoanguka katika jaribu hili. Samahani wewe ni mwanaume au mwanamke?
 
Back
Top Bottom