Jamani Housegirl wangu Huyu, Ananitafuta ubaya! (STRICTLY KWA WANAUME TU)

Trust mi huyo kaja purposely kuvunja hiyo ndoa!!
Na navyowajua wa singida,hadi mama zao huwa wanawafundisha kuteka ndoa za watu,na wanatumia sn ushirikina!!
Ukigusa tu ,hutoki imekula kwako!!

Muondoeni,na mshirikishe mkeo,kwa kawaida wamama ambao wapo vzr kiroho angeshajua!!

Naona mkeo kashahisi,na atakuwa anafuatilia kimyakimya ,usicheze kabisa na mwanamke!!
Wanawake wanna hisia Kali we acha tu, hata akijificha vipi otajulkana tu
 
Itakuwa ndiyo tabia yako kutembea na ma/house girl. Kama ulivyosema ushabadilisha zaidi ya ma/house girls sita tofauti, je waliondoka kwa sababu zipi? Mazingira hayo unayatengeneza mwenyewe alafu unasingizia.
 
mkuu heshima kwa ndoa yako na mkeo iweke mbele achana naye usiangamize furaha ya familia yako kwa kitu kidogo ama tamaa ya mwili ya mtu wa kuondoka.
 
Jamani naomba ushauri kuhusu hili.

Mimi ni mume wa mke mmoja na watoto wanne. Hivi karibuni tumepata housegirl mpya kutoka Singida, amemaliza form four hakubahatika kuendelea na masomo kwa sababu ya kukosa sifa za shule za serikali. Ni mzuri wa kawaida, yaani hana muonekano ule wa mahousegirl-naamaanisha muonekano choka mbaya kweli anafaa hata kuwa mke wa mtu. Katika historia yangu sijawahi hata siku moja kutembea na housegirl na mpaka sasa nishaajiri hao h/girl si chini ya 6, huwa niko very serious na sitaki mazoea nao hata kidogo.

Huyu amekuja naona anataka kuniangusha katika msimamo wangu huu. siku ya kwanza kutambulishwa kwake alionekana kushituka sana ingawa na mimi kwa ndani nilimkubali kuwa mzuri. Maisha yakaendelea na siku zikafunguka. Sasa toka siku hiyo amekuwa anakosa sana sana tu confidence ninapokuwa nyumbani, mara atajikwaa, mara ataogopa kuja mbele yangu n.k mbaya zaidi ninapokuwa peke yangu lets say wengine wapo mbali ananichangamkia sana na kutabasamu muda wote kila nitakalooongee yeye anatabasamu hata kama si la kufurahisha, nikimtuma kitu ataniletea wakati napokea anainua kichwa kuniangalia kiuchokozi halafu anatabasamu, basi na mimi nikawa natabasamu. Ikitokea labda nimerudi nyumbani na nahitaji chakula mapema atanipikia vizuri sana wakati mwingine anongeza kitu ambacho hakikupangwa kwenye ratiba ya chakula cha siku hiyo, anaweza kunkaangia mayai au akachemsha chai ya maziwa akaweka na viuongo haraka haraka na kunipatia chakula.

Tatizo, wife keshamshitukia hizo nyendo zake, amekuwa kila mara ananiuliza kuhusu mtu huyu, anasema mbona fulani ukiwepo anakuwa hana confidence nikamwambia mi sijui embu muulize alipomuuliza akamjibu wife kuwa eti ananiogopa kwa sababu aliambiwa na mlinzi mi ni mkali sana achunge asinikorofishe. Lakini ukiangalia mapozi yake kwangu si ya mtu anayemuogopa. Si hizi ameongeza zaidi, kunisalimia/kuniamkia kwake imekuwa ngumu sana ni mara mojax2 sana. Mi kwa ujumla ni mtu nisiyejali vitu vidogo vidogo na nilichojaribu kufanya ni kuwa mbali nae, nimeongeza kuwa serious, na wakatui mwingine nakuwa mkali ninapoongea nae ili awe mbali nami au afute hicho anachofikiri au kukitafuta, Lakini nahisi ananitafuta ubayaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!

Nimfanyeje? au nifenye lakini nahisi kujidhalilisha kwa mah/girl!

Wana mitego hawa aisee
Kama una roho ndogo unaaribu ndoa hv hv.
 

Attachments

  • 1434883015661.jpg
    1434883015661.jpg
    86.4 KB · Views: 297
Back
Top Bottom