jamani hii ni halali kweli???

zimwimtu

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
1,988
1,095
Its this my machine operator, anaishi na mwanamke mitaa ya mabibo na wana motto mmoja. (hawajafunga ndoa) jamaa kajitahidi kapata kiwanja CHANIKA. Na kajenga kibanda chake sasa anataka kuhamia ili kupunguza ukali wa maisha, maana kodi za nyumba nazo zinakera.

Mke wake kakataa kwenda chanika kwamba hayuko tayari kuishi porini na kama aking’ang’nia kwenda kuishi huko ndo utakuwa mwisho wao, kila mtu ajue maisha yake. Na wakati anajenga huyo mke wake alikuwa na taarifa na alishafika kuona maendeleo ya nyumba.

Bas jamaa kachanganyikiwa hajui afanye nini. Mke anampenda na amejaribu kuongea nae sana lakini hamuelewi.

Sasa niwaulize wadada, hivi upo tayari kumtosa mpenz wako kisa kaenda kuishi mbali na mji? Ya nni kubaguana kwa sababu ya makazi?

Maoni yenu plz…
 
Huyo anatingisha kiberiti tu amrudishe kwao. Mwanaume rijali hatakiwi kuendeshwa na uke, amenioa au nimemuoa?
 
Huyo anatingisha kiberiti tu amrudishe kwao. Mwanaume rijali hatakiwi kuendeshwa na uke, amenioa au nimemuoa?

Chonde chonde mkuu, uke ndio unaendesha dunia na hao watu hawajaoana so NO legal bind. Kama mamaa alijua kuhusu huo mjengo kwanini akatae sasa, amwambie tu kuwa huo ndio uwezo wake kama anaweza kufatana nae au kama hataki ampe altimatum.

Maana hata akiwa ni mke wa ndoa atakupa shida, ili hali hatafikiria uwezo wako kwa kutaka maisha msiyoyaweza.
 
Mapozi mengine bwana,walipokua wakinunua uwanja mpaka kujenga alikua wapi! I wish ningekua uyo mume,natangulia kwenye makazi Mapya then ni
Nione atachukua mamuzi gani
 
Huyo anatingisha kiberiti tu amrudishe kwao. Mwanaume rijali hatakiwi kuendeshwa na uke, amenioa au nimemuoa?
dem anamaanisha kweli, mpaka jamaa anadhani kuna mtu anamtia kiburi maana aliwahi kuhusishwa kutoka na salesman mmoja hapa kazin!!!!!!!!
 
Its this my machine operator, anaishi na mwanamke mitaa ya mabibo na wana motto mmoja. (hawajafunga ndoa) jamaa kajitahidi kapata kiwanja CHANIKA. Na kajenga kibanda chake sasa anataka kuhamia ili kupunguza ukali wa maisha, maana kodi za nyumba nazo zinakera.

Mke wake kakataa kwenda chanika kwamba hayuko tayari kuishi porini na kama aking'ang'nia kwenda kuishi huko ndo utakuwa mwisho wao, kila mtu ajue maisha yake. Na wakati anajenga huyo mke wake alikuwa na taarifa na alishafika kuona maendeleo ya nyumba.

Bas jamaa kachanganyikiwa hajui afanye nini. Mke anampenda na amejaribu kuongea nae sana lakini hamuelewi.

Sasa niwaulize wadada, hivi upo tayari kumtosa mpenz wako kisa kaenda kuishi mbali na mji? Ya nni kubaguana kwa sababu ya makazi?

Maoni yenu plz…

Hapo red ndo umejinyima ma experience; Changamoto la mume unapeleka kwa wadada?????????
Ashakum si matusi kesi ya ................. unampelekea........................
Fungua uzi mwingine uwasikie wandago..................wachilume....wagosi.....men........wanamume.....l'home
 
Ikiwa alikuwa na taarifa za tangu kununuliwa kwa kiwanja hana haki ya kukataa kwenda. hataki Bandugu PIGA CHINI hana faida hasa mbele ya safari.
 
Hapo bdae ndo yale mambo ya ndoa ndoano, huyo hatak enda mbali kuna m2 atamkosa huku town
 
Amwambie2 natungulia ukitaka kuja utakuja utanikuta asilete upumbavu huyo ana mapepo nini mi nijipinde nijenge we ulete umbumbu wako aisee utaniona mbaya2!
 
Amwambie2 natungulia ukitaka kuja utakuja utanikuta asilete upumbavu huyo ana mapepo nini mi nijipinde nijenge we ulete umbumbu wako aisee utaniona mbaya2!
 
Dah.. Huyo mwanamke nimempendea kitu moja...

Wala hang'ang'anii material stuffs... Mwanamke mwingine hapo,ye ndiyo angekuwa wa kwanza kutangulia.

As kwa mwanaume,swala ni dogo ahame na ndugu yake aishi naye. Kifupi,mwanamke huyo hamtaki. Sasa unaishije na mtu asiyekupenda..
 
Kuna ki2 kinanitaza hapa; alimshirikisha mkewe kweli from the beginning au ndo wale "wa2nza cri" kwa kicngizio ucmwambie vyote kwa sbb hamjafunga ndoa? Sa iv yamemcbu ndo anasema alimshirikisha!?
On the other hand kama kweli mke alishirikishwa na hakutia neno then sasa iv anagoma kuhamia then there must be smthing behind the scene hapo! C ajabu mwanamke anatafuta gear ya kuchukua hamsini zake hapo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom