Jamani eti naye anataka kunizalia mtoto

Galadudu

JF-Expert Member
Jun 23, 2014
2,305
772
Ni mdada mmoja hivi jirani yangu ni mzuri kwa kweli na kwa sasa yuko single, habari yenyewe iko hivi:

Nina watoto wawili wote wa kiume na wote wamefanana sana na mimi mchezo unaanzia hapo.Kwa kuwa ni mtani wangu kikabila na kwa wife pia ni hivyo hivyo maana mi na wife ni kabila moja, utani ukaanzia kwa wife kwamba.

Lazima na mi huyo mwanaume anipe mtoto anaefanana nae. Hayo na mengine mengi ya kiutani yalikuwa yanaendelea lakini wife hakuniambia cause alijua ni mambo ya utani tu.Juzi sasa Jumapili baada ya kutoka church ilipofika jioni nikaamua nikapate vibia vyangu viwili na ka nusu kilo ya kitimoto.

Bahati nae nikamkuta yuko pale tayari ameanza kupendeza kwa kinywaji maana anatokea mkoa ule wa watu wenye itikadi ya kujinyonga wakiudhiwa, nackia wako vizuri sana kwa kupiga kinywaji hawabagui.

Akaniona akanirukia akanikumbatia, tukaenda kukaa alipokuwa kakaa yeye ndio akaanza story sasa:- mtani mi nickufiche nataka nikuzalie mtoto mmoja maana huwa nafurahi sana nikiona jinsi unavyofanana na wanao.

Jana yote nimeshinda nawaza kuwa huyu ni jirani hivi itakuwaje nikimjaza mimba na mtoto akafanana na mimi, cku nzima ya jana tumeshinda ananisumbua mara anipigie mara massege za kuniuliza naendeleaje na kazi full usumbufu.

Wakuu hebu mniambie nimpe tu anachokitaka au.
 
Atakuwa kwenye ovulation huyo...
Subiri kama hadi j'mosi atataka kukuzalia...
..hawa viumbe ni vinyonga, shaurilo!!
 
Katika yale majanga matatu ya taifa kutokana na Mwalimu Nyerere, nafikiri kuna moja linakuhusu moja kwa moja, la ujinga!
 
Ukishajua umeoa unapaswa kufanya maamuzi yanayofaa, tayari wewe ni mume wa mtu na unapaswa kuheshimu ndoa yako.
Tutajua kuwa unaheshimu ndoa yako kwa kutojihusisha na UZINZI au kufanya ngono na mtu ambaye hujafunga nae ndoa.

Sasa iweje jambo kama hilo likuumize kichwa?
Unapaswa kumwambia wazi kwamba nimeoa na sihitaji kufanya UZINZI.

Kumbuka kuwa kufanya nae ngono kutahatarisha ndoa yako lakini pia kutakufanya umkosee mungu (kwani UZINZI ni dhambi nzito)
 
Like zangu 100 zikufike popote ulipo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom