Jamani degree pumba za msemakweli ziliishia wapi?

Pawaga

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
1,330
966
Niliwahi kusoma kitabu cha jamaa mmoja anaitwa Kainerugamba. Kati ya mambo mengne mwandishi alitoa orodha ya majina kumi ya watu wenye vyeti bandia (digrii hewa).Baadhi ya MAFISADI wa elim ni viongozi wakubwa serikalini mfano,. Makongoro Mahanga,Lukuvi,Mary Nagu,Kamalla,Diallo na Nchimbi. Pia TCU walitoa tamko na kuwataka walioandikwa wapeleke vyeti vyao TCU kwa uhakiki na udhibitisho wa uhalali au ubandia. Sasa wana JF,..yeyote aliye na taarifa ya TCU naomba anijulishe la hao TCU na pia walioandikwa walichukua hatua gani dhidi ya Msemakweli?. Asanteni sana!.
 
Kitabu kilipigwa vita na baadhi ya hao mafisadi,iliripotiwa kwamba kuna jamaa alikuwa ananunua nakala nyingi ili zisisambae,baadhi yao walimshitaki Msemakweli eg Diallo,nadhani kesi inaendelea,wengine waliuchuna kabisa sijui kuashiria ukweli au kuupuuza ukweli
 
Hata mi naona kinerugaba bora aachane nao mana hamna hata aliyewajibika kwa utapeli huo. Mfano leo kuna dr.aliyetajwa,anafanya PhD mzumbe. Ni mambo ya ajabu ambayo ameachiwa Msemakweli tu wakati ujambazi wa elimu kama huo ilibidi wawe jela,ila kwa kuwa uozo umeanza kuoza tena ,wote wanaona poa tu!
 
Nijuavyo mimi wengi walitishia kwenda mahakamani kama ilivyokuwa katika orodha ya mafisadi ila mpaka sasa hakuna aliyekwenda wote wanatishia hii inathibitisha yupo sahihi
 
Mimi natamani huyo msemakweli

aandike waliopata ubunge na vyeo vingine kwa ngono.....

Nitanunua hicho kitabu
 
angechunguza hata elimu za sekondari tujue akina makamba snior ilikuwaje,makamba junior inaeleweka alisolve fake o level,
 
Back
Top Bottom