DEVINE
JF-Expert Member
- Mar 11, 2011
- 536
- 86
Jamani hii sio masihara,nimekutana na mbibi mmoja jana jioni wakati natoka miangaikoni,baada ya kumsalimia tukaanza stori kwani wote tulikuwa tunaelekea njia moja. Katikati ya stori akaniauliza kama najua jinsi ya kutabiri kifo.Sio siri niliogopa nikamjibu hapana,sasa baada ya kumjibu tu akaanza lecture. Akaniambia mtu ufa siku chache kabla ya tarehe ya kuzaliwa au baada ya tarehe ya kuzaliwa au inawezekana ni mwezi tofauti ila ni tarehe chache kutoka tarehe ya kuzaliwa au baada,tena anaweza kufa siku chache tangu ajitabirie kifo yaani mtu kesha sema yeye ni wakufa tu yaani ameshakata tamaa ya kuishi.Kama ni msanii ni siku au miezi michache eidha kaimba au kaandika au kaigiza au kachora kifo chake...Dah sikutaka nijue zaidi nilimkatisha yule bibi,lakini akasisitiza labda tu awe amejiua au ameuawa,aisee ilitokea nimebadili njia ilimradi nisiendelee kusikia maneno ya yule bibi...Jamani mie hata sitaki kuamini,ivi yanaukweli maneno hayo ya bibi? Nawasilisha.